Hivi mwanamke bora katika ndoa ni yupi shostito...?

[/COLOR]
Hapo Sipo umekosea, katika kipengele cha heshima inapasa kila mmoja amuheshimu mwenzako.
Asanteni mada nzuri sana hii, hivi jamani eti unakuta wewe unampa mmeo heshima zote, hajawahi kukufumania na mtu wala nini. Ila cha ajabu yeye anapenda sana kusikiliza mambo ya nje au rafiki bila kudhibitisha kama ni kweli. Ambapo huzua na kusababisha miungomvi kila siku bila mpangilio wowote. Sasa mme kama huyu nae aendelee kupewa hio heshima tuu.
 
Asanteni mada nzuri sana hii, hivi jamani eti unakuta wewe unampa mmeo heshima zote, hajawahi kukufumania na mtu wala nini. Ila cha ajabu yeye anapenda sana kusikiliza mambo ya nje au rafiki bila kudhibitisha kama ni kweli.

Kama uko huna hatia yoyote hata hayo maneno ya nje hayatakuwepo!!
 
Kama uko huna hatia yoyote hata hayo maneno ya nje hayatakuwepo!!
Hamna bwana NN, binadamu ni watu waajabu sana, yani wanaweza kukuzulia jambo mpaka wewe ukashangaa yani. Kuna wale wasiopenda kuona mwenzao anafurahia maisha wanafanya kila hali ili kuharibu tuu.
 
Hamna bwana NN, binadamu ni watu waajabu sana, yani wanaweza kukuzulia jambo mpaka wewe ukashangaa yani. Kuna wale wasiopenda kuona mwenzao anafurahia maisha wanafanya kila hali ili kuharibu tuu.

Mara nyingi mtu ukizushiwa kitu basi kitu hicho lazima kitakuwa kimefanana fanana na hali fulani iliyopelekea kuzushiwa kitu hicho.

Kwa mfano, watu hawawezi kuzusha tu eti Mrs. Mtaba anamegwa na NN....wataanzia wapi? Lakini wakianza kumwona NN na Mrs. Mtaba beneti kila mahali hapo ndo uzushi huanza.
 
...mbona 'hauz-geli' anaweza?

Huo ni usanii.
Anaamka mapema kweli ..anajifanya busy hadi wenyewe wanapoondoka kwenda kazi ...kisha anarudi kulala tena chumbani kwa wenyewe.Akiamka anapata b/fast ya nguvu... anafanya shughuli ndogondogo... kisha anajiandalia lunch. Mchana anapata siesta hadi kwenye saa 9-10. Anaamka kabla wenyewe hawajarudi... usiku kwa vile mchana kutwa alikuwa kalala... anakuwa hana usingizi... anajifanya busy tena hadi anaposikia usingizi...anaenda kulala! Hii ni hali halisi kwenye nyumba nyingi.Wapo wachache wanaofanya kazi...hasa wale ambao mother house hafanyi kazi za kuajiriwa zenye kuhitaji kuamka asubuhi sana na kurudi jioni sana.
 
Anayejua kuvaa, anayejua kujikwapua, anayejua kujishau, anajua kujichubua au anayejua kula hela ya mumewe vizuri...!?
Kwa mujibu wa wataalam wa mambo haya mwanamke bora katika ndoa ni ....

1.Anayejua mumewe anataka nini.
Wanasema mke mwema ni yule anayejua kumsoma mumewe na akamjua ipasavyo.

Unajua mara nyingi hawa wenzetu wanatarajia wafanyiwe mambo sahihi, na pale wanapotenda yale ambayo hayakongi hisia zao, hujawa na hasira au kuvunjika moyo. Ukijifunza kumjua na kujua mazuri na mabaya katika mapenzi yake utasimama tofauti kati ya wale anaokutana nao barabarani na wewe uliye mkewe.

2. Anayekubali kujishusha
Kila mtu ana asili ya kujiona yeye ni bora kuliko mwingine, lakini lazima ufahamu kuwa kujishusha hakumaanishi kuwa unapunguza ubora ulionao. Wanaume wanapenda kujihisi wao ni kichwa katika nyumba. Mpe nafasi hiyo, ikibidi kujishusha ili yako yakwendee ...Hewallwa. Kujifanya mbishi na mjuaji unamfanya aamini alikosea kukuchagua wewe kuwa mkewe. Upo shosti.

3. Anayeridhika na alichojaaliwa...
Si busara kumnanga mwanamme wa watu kila siku kwa kile ambacho ameshindwa kukufanyia.

Wapo wanawake ambao huamini kuwa kwa kumkera mumewe kuhusu vitu fulani wanaonyesha uhodari waojuu yao. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kama huridhiki na ulichojaaliwa nacho huto kaa uridhike.

4. Anayejua kunyenyeekea... Wanasema unyenyekevu ni mbolea ya mapenzi, kila mwanamme angependa arudi kwake akute faraja na si karaha. Unyenyekevu hapa hucheza nafasi nzuri katika mapenzi kwa kuonyesha hisi zako wa mwenzako na kumfanya ahisi kuwa yeye ndiye yeye.

Mithali 31, anatoka kwa Mungu, msikilize Mwaitege
 
Huo ni usanii.
Anaamka mapema kweli ..anajifanya busy hadi wenyewe wanapoondoka kwenda kazi ....

...mydear, kipindi cha uchumba na fungate tulifanyiwa usanii huu, unapewa ufalme wa nyumba! Ukiamka kila kitu ushaandaliwa,...halali mpaka wewe umelala

siku hizi mnh! chai jipikie mwenyewe, ...usiku unajikuta peke yako sebuleni, ukichungulia chumbani mwenzio tayari anakoroma!...

Heri huyu mrembo Jamiiforums, ...'yeye' hachoki, hata usiku wa manane nikiamka yupo tu macho ananisubiri...I love you JF ...:*
 
Umejaribu kushea naye about your feelings au nikulalama tuu hapa JF. Wewe mwenyewe ndie uliyembadilisha penda usipende. Mimi naimani kuwa sisi wanawake hubadilika haraka sana kutoka na mtu mwenyewe anavyokuchukulia. Hebu jichunguze utapata jibu mwenyewe tuu.
 
Mke bora awe mkarimu,flexible,wise na msikivu.
Tough kumpata unaitaji msaada wa mola otherwise waweza vagaa mkenge ndoa ikawa chungu
 
Umejaribu kushea naye about your feelings au nikulalama tuu hapa JF. Wewe mwenyewe ndie uliyembadilisha penda usipende. Mimi naimani kuwa sisi wanawake hubadilika haraka sana kutoka na mtu mwenyewe anavyokuchukulia. Hebu jichunguze utapata jibu mwenyewe tuu.

...ohhh, nilidhani mnaukubali ule usemi Tabia haibadiliki!
 
...ohhh, nilidhani mnaukubali ule usemi Tabia haibadiliki!
Hubadilika sometimes, especially ukikuta umeingia with two legs then ukakuta mwenzio yuko with one leg out...sasa hapo na wewe utafanya nini! uendelee kung´ang´ania with your two legs.
 
Back
Top Bottom