Hivi Mkuu wa Wilaya anaweza kumfuta kazi Mkurugenzi wa Wilaya?

Baadhi ya viongozi wa awamu ya Tano wanatuaibisha Kama nchi ukiangalia DC muro anavyochemka utadhani gangwe Yuko bar mi nadhani mamlaka zilizowateua ziiwasaidie ethics kupunguza show zao . Mkurugenzi nae ni mtu mkubwa kwa nafasi yake kumfokea mbele ya anaowaongoza sijui Kama ina Afya hata kidogo nadhani kuna namna ya kunyoosheana vidole bila kiwango mbele ya wanaoongozwa
Umenena mkuu ni aibu tena wanaonekana hawakujiandaa na wanchokifanya, lakini pia hawana ushirikiana. Huo Ndo ukweli bila kupepesa
 
kwa sababu tu hayo ndo mambo anayoyapenda mh. jiwe na ukizingatia wateule wote wa mh. jiwe wanalichukulia jiwe ndo kama role model wao, sasa usishangae jerry muro baada ya wiki kadhaa ni RC somewhere, kwa wenye uelewa na vichaa haitashangaza.
 
Hii ndio hasara ya viongozi wa kuokotwa barabarani , huyu msela Jerry aliwahi kukamatwa na pingu za wizi .
Jeri Muro ni usalama yule

Soi kwamba alienda kufnya kazi kwa bhati mbaya tbc alinda kwa kazi maalum

Angalia alipoenda yanga kwa kazi mqalumu uliona kilichofuata kwa manji baada ya yeye kuondoka pale

Jifikilie kesi ya pingu iliishaje kwanini akufungwa na kipindi hicho watu walikuwa wakimtetea


Sitoshamga nikisikia pia arumeru kaondolewa kapelekwa kwingine
 
Nafahamu kwamba wote hawa ni wateule wa Rais , lakini inapotokea sintofahamu miongoni mwao Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya anaweza kumuondosha kazini Mkurugenzi wa Wilaya ?


Pichani : Ni kiongozi wa jamhuri isiyofahamika akitangaza majina ya wateule wake mbele ya waandishi wa habari .
Hawezi lazima ampe taarifa Mkuu,ndio Mkuu atoe go ahead,hivi unaweza mfukuza kiti ndugu aliyepewa kiti na Boss wako? Hapana lazima umpe taarifa Boss na atafanya uamuzi..
 
Tatizo wakuu wa wilaya hawajapewa semina elekezi. Niaibu mkurungezi na mkuu wa wilaya kufokeana hazarani,
 
Kweli inaudhi huyu Jeri Muro in msomi gani hii inaonyesha tulivyofeli kwenye elimu tz amesahau TFFwalivyompoteza kweli anga la mpira Na siasa atafanywa vivyohivyo hivi hana hata watu wa karibu wakamkalisha ajue yuko Meru CIO Bagamoyo anafokea wanakijiji ka watoto
 
ukiwa kiongozi jitahidi kuwafanya watu wasijue namna ulivyopata cheo wakijua tu umekwisha
 
Nafahamu kwamba wote hawa ni wateule wa Rais , lakini inapotokea sintofahamu miongoni mwao Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya anaweza kumuondosha kazini Mkurugenzi wa Wilaya ?


Pichani : Ni kiongozi wa jamhuri isiyofahamika akitangaza majina ya wateule wake mbele ya waandishi wa habari .
hahahaaa hao madogo aisee
 
Hawezi kumfukuza kazi, ila anaweza kumuweka ndani masaa 48, akitoka anamuweka tena ndani masaa 48, akitoka anamuweka tena, na tena... Kwa ufupi DC anaweza kumtumikisha kifungo DED kwa muda anaotaka
 
Yaani hapo ni sawa na kusema mtendaji wa kata amfute kazi mratibu kata (afisa elim kata kwa sasa) kitu ambacho hakiwezekani, kuwapa mamlaka ya kusimamia usalama wa wilaya watu wahuniwahuni kama akina Muro ambao hawajui ata nini wanatakiwa kufanya kulingana na nafasi zao, madhara yake ndo hayo ya kupandisha mzuka mbele ya media huku akitaman amfukuze kazi yule DED, kitu ambacho ni sawa na kuvunja jiwe kwa ngumi. ndo maana ata DED alicheka kwa dharau mpaka muro akajishtukia kuwa jamaa kamdharau
 
Back
Top Bottom