Hivi Mkurugenzi mmoja wa halmashauri kukaa kituo kimoja kwa zaidi ya miaka 3 hakuwezi kuwa sababu ya kutengeneza ufisadi?

Unabishana lete ushahidi mezani,nami ntaweka wa kwangu mezani, kwa hoja zangu zote nilizoorodheaha hapo. twende kwa numbers mkuu
Weka huo ushahidi wa wakulima kupewa pembejeo na hapo halmashauri.Kilichofanyika katika msimu wa kilimo ni kule kujiandikisha kwa ajili ya mbolea ya ruzuku kama ulivyokuwa mpango wa serikali kwa nchi nzima.
Kitu kingine ilikuwa ni kutoa sumu ya kuua wadudu wahsribifu wa mazao ikiwemo panya,na sumu ililetwa na wahisani na iligawiwa karibu halmashauri zote za mkoa wa Morogoro.

Haya hicho kilochotolewa na halmashauri kama halmashauri ni kipi?.Kiweke hapa.
 
Unabishana lete ushahidi mezani,nami ntaweka wa kwangu mezani, kwa hoja zangu zote nilizoorodheaha hapo. twende kwa numbers mkuu
Kwa kupitia T.O wa mchongo,pesa kuanzia za matengenezo ya gari,mafuta,vipuri n.k zinapigwa na magari ni mabovu siku zote.Utaratibu wa kisheria wa ukaguzi wa magonjwa ya gari na matengenezo haufuatwi tena na gari zinatengenezwa mitaani kwa gharama ndogo huku zimetolewa pesa nyingi.

Acha kukwepa kusudio la uzi.
 
Bila shaka
Unamzungumzia Engineer Stephano B. Kaliwa,

mkurugenz halmashaur ya mlimba, Yuko pale tangu 2018 Kama skosei

Jamaa Ni mchapakazi sana na mzalendo Sana. Ukiwa na shida pale ofsin hata usiku wa manane au wikendi Hana noma ukipigia anaweza kuja kukuhudumia kiroho Safi mpk ukaridhika.

Mbali na ya Malalamiko ya mtoa mada,

Ukiangalia vzur kitakwimu,
halmashaur Yake bado ni changa ila inakimbiza balaa kimapato mkoa mzima wa moro ikizidiwa TU moro mjini.

Jamaa Ni Mbunifu mno wa vyanzo vya mapato,Ni msikilizaji mzur wa wawekezaji wa mpunga na maliasili, anabembeleza wawekezaji, anagawa Hadi Mashamba bure Watu walime mzunguko wa pesa uwepo.

japo Kuna MDA anazingua sn ktk ubunifu wa tozo zake ila mnyonge mnyongeni yote Ni Katika kujenga. Ni msikivu na msikilizaji mzuri,mnaweza muita mezani mkayazungumza akalegeza au kufuta kabisa tozo husika mkaendelea kufanya kazi.

Pia kielimu,
halmashaur yake japo Ni changa,
Ila inaongoza Sana kufaulisha level zote kuanzia std4,std7 na form iv kwa mkoa mzima wa moro ikizidiwa TU na manispaa ya Moro.

Jamaa kawapa malengo na mikataba waalimu ya kufaulisha, wanaofaulisha na utoa motisha MBALIMBALI. Ukifelisha utatakiwa kujieleza.

Halmashaur ya jamaa
shule kibao za kata tena ndani ndani huko hata miundombinu ni Changamoto Ila zishafuta division sifuri form 4.
Unabisha kaangalie matokeo ya necta.

Wafanyakazi wengi wa halmashaur ile hawampendi jamaa maana jamaa haendekezi uzembe, ukizingua unawajibishwa pale pale, anaziara kibao za kushtukiza, hajakukuta kazini utapaswa kujieleza. Jamaa anasikiliza sn wananchi na wadau wa maendeleo.

Jamaa hataki kuskia urasimu wa Aina yoyote pale halmashaur, ukienda unahudumiwa chap unaondoka zako.
Vile vibahasha vya kihuni huni na urasimu Kama zamani wafanyakaz wanaanza kuringa na kukuhudumia wanavojiskia pale halmashaur kwake hamna kabisa.

Jamaa akiwepo ofsn huwez kuona mtumish yoyote pale halmshauri anazubaa au kukuchelewesha foleni,mteja unahudumiwa vzur mpk unaridhika unaondoka zako.

Pia wafanyakaz wengi wanamsagia kunguni Ili ahamishwe ili aje mwngn, waweze kurelax, na Kupiga madili yao.

Pia watumish wengi hawapapendi mlimba kule sababu Ni pori na Chaka sana,kila anaeajiriwa kule anataka kuhama kuhamia halmashaur za mijini.

jamaa anabana hataki, umeajiriwa ufanye kazi nchini Tanzania, Kama upataki mlimba-mazingira ni mabaya.
unataka Nani Sasa akakae uko mlimba?

Falsafa ya jamaa Ni hataki kuhamisha wafanyakazi, otherwise una solid evidence.
Watumish wabaki vituo vyao vya kazi wachape kazi halmashaur bado changa ile ipate mapato ya kutosha iweze kujiendesha na kukua.

KITU AMBACHO KWA JICHO LA KIMAENDELEO,JAMAA YUKO SAHII SANA.

Mkuu, mara zote kitanda usichokilalia daima huwezi kujua kunguni wake.
Watumishi wa mahala husika ndo wanaomjua vizuri mkuu wao. Wewe na Boss wao kuna mambo yanayowakutanisha, maslahi ya Serikali na maslahi binafsi.

Mkurugenzi yupo kuhakikisha miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri yake inafanikiwa kupitia aidha mapato ya ndani ama Serikali kuu. Hicho ndicho kipimo cha ufaulu wake, sasa unategemea azinguane na wawekezaji na wadau wake wanao mletea mapato kwa ajili ya maendeleo? Atapimwa kwa kitu gani?

Mtoa mada anaweza kuwa sahihi ama asiwe sahihi, ingawa mara nyingi maslahi hufifisha kanuni na taratibu za jambo husika, na hiki ndicho chanzo cha kutokuelewana baina ya bwana mkubwa na watu wake wanaosimamia kanuni na sheria pasipo kupindisha. Substitution inaweza kufanyika ili uchezwe mdundo sawa, ngoma iflow pasipo vikwazo.
 
Mh:Rais na mama wa taifa,
Asante sana na pongezi sana kwa mabadiliko haya ya wakurugenzi.
 
Back
Top Bottom