Hivi Malezi yamenishinda?

condorezaraisi

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
225
116
Wadau msaada wa malezi ..
Nina kabinti kangu kana miaka 4...naamini nimekuwa nakalea katika mienendo mizuri anapokosea namfundisha na kumwambia ukifanya hivi si vizuri mama baba pia mungu hapendi ..kwani shuleni kwenu mnafundishwa kukosea katasema sorry mamy
Kesho kanaweza kurudia kosa lile lile bado naendelea kumfundisha kwa upole nikiamini 4 years bado mdogo sana anahitaji mapenzi na muongozo..
Kimbembe kiko kwa baba yake..kama mjuavyo mtoto anaweza kuwa anakula mara kashika hiki mara kamwaga maji..mara anakula anataka amlishe na mdoli wake..
Baba yake unaweza kushangaa anakapa kibao tulia nimesema sitaki utundu au anakafokea kwa ukali sana jamani..
Jana kalikuwa kanacheza kanarukia huko mara kametoa vitambaa mezani baba yake akamchapa vibao nikiwa zangu jikoni .....mtoto alilia weee ananiambia mama dad mbaya kwanini ananipiga piga kila saa mie si mtoto eti mama? ,Masaa yakapita mtoto akanyamaza nikawa nimemtuma kwa baba yake chumbani kagoma kwenda kwa dady yake anasema mie siendi namuogopa dady mkali sana huku analia namwambia nenda kagoma...
Leo asubuhi namtuma tena kwa dad anasema no mamy dad atanichapa

Nikimzuia dad na kumwambia amfundishe kwa upole ananiambia namdekeza mtoto.

Roho unaniuma jamani ..ni mie ndo nakosea kumlea huyu binti??
 
Malezi sio kupiga vibao
Mtoto wa miaka minne bado mdogo sana kuelewa kuwa anachokifanya ni wrong u ni sahihi
bado anahitaji kufundishwa kwa upole na kuambiwa hili ni baya au zuri na hata akirudia rudia makosa bado sio sahihi kumzaba vibao kuwa ni mtundu
Mweleze huyo baba wa mtoto kuwa malezi sio hayo na wala hapo hakuna kudekezwa
Aende na mtoto taratibu na kwa upole amweleze kwa upole kuwa hili ni kosa na usifanye tena
Anaweza kuchukua mkaa akachora chora nyumba nzima ila unampeleka pale alipofanya kosa unamwambia kuwa hii si sahihi
Sijui na mimi nakosea
 
Asante sana Mr Rocky

Mie mwenyewe nadhani mtoto yuko katika kipindi cha kujufunza jema na baya sijui kwa nn baba yake hamuelewi mpaka mtoto kaanza kumuogopa.
 
Asante sana Mr Rocky

Mie mwenyewe nadhani mtoto yuko katika kipindi cha kujufunza jema na baya sijui kwa nn baba yake hamuelewi mpaka mtoto kaanza kumuogopa.

Tena itakuwa mbaya sana kwake mtoto akimuogopa maana hayo sio malezi
Anatakiw akuwa karibu na mtoto amfundishe na kumwelewesha mambo ambayo anatakiwa kufanya na yale ambayo hatakiwi kufanya
MAlezi sio kupiga vibao au fimbo maana ataishia kuwa sugu na kukuogopa
Hata akiwa na shida atashindwa kuja kukwambia au jambo lolote likimtokea atashindwa kumwambia baba yake kwa kuwa anamwogopa
Mtoto hatakiwi kuwa mwoga kwa mzazi haswa kipindi anakua maana atakuwa na mawazo hayo mpaka mwisho kuwa baba ni mkali
 
Dada umesahau enzi zile baba akikohoa tu watu wote mpo uvunguni
lakini baba kuwa mkali sometimes inasaidia
wengine tungekuwa neti humu

Smile kuna umri wa kuwa mkali
Kama binti amekuwa kigoli au kaka ameshaanza kumtamani house gal hapo baba anaruhusiwa kuwa mkali
Ila miaka minne bado sana hapo anaapply ukali wake kusiko kabisa
 
smile kuna umri wa kuwa mkali
kama binti amekuwa kigoli au kaka ameshaanza kumtamani house gal hapo baba anaruhusiwa kuwa mkali
ila miaka minne bado sana hapo anaapply ukali wake kusiko kabisa
samaki mkunje angali mbichi kaka
unamjua yule lulu mimi namfahamu baba yake kabisa .amelelewa na mama yake lakini baba yake alikuwepo na alikuwa rafiki yake kweli
mbona alikuja kumkana hadi kwenye gazeti hamsikii kwa lolote
baba lazima uwe mkali bwana ila isiwe too much
mtoto akileta jeuri piga ngwara ,mateke ,vibao mi naona poa tu
kwa nini alishe mdoli uji bwanaaa? na keshaambiwa aache mara nne kama sio ngwara anataka ni nini?
 
Smile duh umenichekesha aise
Alishe midoli uji si ndio akili zake zilikomtuma bana
Bora huyo wa kulisha midoli kochi lako hapo sebuleni linakuwa ubao wa kujifunzia kuandika
Au gari yako nje inakuwa sehem ya kujifunza kuandika alichojifunza shuleni
Au ukuta wako unakuwa sehem ya kujifunzia kuandika
 
Wadau msaada wa malezi ..
Nina kabinti kangu kana miaka 4...naamini nimekuwa nakalea katika mienendo mizuri anapokosea namfundisha na kumwambia ukifanya hivi si vizuri mama baba pia mungu hapendi ..kwani shuleni kwenu mnafundishwa kukosea katasema sorry mamy
Kesho kanaweza kurudia kosa lile lile bado naendelea kumfundisha kwa upole nikiamini 4 years bado mdogo sana anahitaji mapenzi na muongozo..
Kimbembe kiko kwa baba yake..kama mjuavyo mtoto anaweza kuwa anakula mara kashika hiki mara kamwaga maji..mara anakula anataka amlishe na mdoli wake..
Baba yake unaweza kushangaa anakapa kibao tulia nimesema sitaki utundu au anakafokea kwa ukali sana jamani..
Jana kalikuwa kanacheza kanarukia huko mara kametoa vitambaa mezani baba yake akamchapa vibao nikiwa zangu jikoni .....mtoto alilia weee ananiambia mama dad mbaya kwanini ananipiga piga kila saa mie si mtoto eti mama? ,Masaa yakapita mtoto akanyamaza nikawa nimemtuma kwa baba yake chumbani kagoma kwenda kwa dady yake anasema mie siendi namuogopa dady mkali sana huku analia namwambia nenda kagoma...
Leo asubuhi namtuma tena kwa dad anasema no mamy dad atanichapa

Nikimzuia dad na kumwambia amfundishe kwa upole ananiambia namdekeza mtoto.

Roho unaniuma jamani ..ni mie ndo nakosea kumlea huyu binti??

Binafsi naona ni sahihi baba kuwa mkali lakini si kuwa mkali wa kupindukia au mkali kwa vitu vidogo vidogo. Kuna makosa ambayo mtoto anaweza kuyafanya ni ya kitoto na anapaswa kuonywa kwa upole lakini kuna mengine yanahitaji viboko vya ukweli vinginevyo tutawaharibu wanetu.

Nafikiri kikubwa hapo ni kupima uzito wa kosa alilofanya mtoto na madhara yake kama ataendelea na tabia hiyo. Hii itasaidia kudetermine aina ya adhabu ya kutoa kwa mtoto. Ila mimi nyumbani kwangu, mtoto akifanya utundu wa ajabu, ni viboko kwenda mbele na hata ukija sasa hivi kwangu hata kama sipo utakuta discipline ya ajabu.
 
kuchapa au kumpiga mtoto siyo njia pekee ya kufundisha mtoto au kumpa adhabu....kwanza ina mfanya mtoto asijiamini ,akuogope badala ya kukuheshimu n.k.
lakini pia wote tumeshashuhudia watoto waliochapwa sana lkn bado hawakufika mbali na tabia zao.
pole sana ,mueleweshe baba yake kiutaratibu sana ,miaka 4 ni umri mdogo sana kwakweli kupigwa kibao.
 
Smile duh umenichekesha aise
Alishe midoli uji si ndio akili zake zilikomtuma bana
Bora huyo wa kulisha midoli kochi lako hapo sebuleni linakuwa ubao wa kujifunzia kuandika
Au gari yako nje inakuwa sehem ya kujifunza kuandika alichojifunza shuleni
Au ukuta wako unakuwa sehem ya kujifunzia kuandika
watoto wa dotcom bwana?
wenzie makete huko wanatunza wadogo zao .
huo muda wa kulisha midoli uji hata hana hapo anae na bibi yake mgonjwa anatakiwe ajue anakula nini?
mimi naona huyu dogo sometimes makofi yanamuhusu sana
mtoto bongo bwana?
 
Kweli Smile
Sometime ukiangalia watoto wa hapa mjini na watoto wa huko kijijini unawez apata kichaa
Mtoto wa kijijini hajui cha kuonywa wala nini yeye anafanya yale yanayompendeza kwa wakati huo
Akajichotee udongo wake atengeneze nyumba yake au vyungu
Watoto wa mjini wao na computer na tv muda wote
 
Pole Condoleza malezi magumu sana ila mwenyezi Mungu huwa anabalance! kwa baba na mama lazima mmoja awe strict zaidi! navinasaidia ila asizidishe!
 
Kweli Smile
Sometime ukiangalia watoto wa hapa mjini na watoto wa huko kijijini unawez apata kichaa
Mtoto wa kijijini hajui cha kuonywa wala nini yeye anafanya yale yanayompendeza kwa wakati huo
Akajichotee udongo wake atengeneze nyumba yake au vyungu
Watoto wa mjini wao na computer na tv muda wote
Nasikia siku hizi wanafundishwa
a-for atm
b -for blackberry
c-for condomu
d- for dushelele
utawaweza wapi watoto hao
piga ngwara kabisa
 
Hata kama unataka kumpiga mtoto, vibao si sahihi unaweza uka over do.
Miaka minne saizi yake kichelewa tu.

Ila kuchapa suna, kumwelewesha lazima, vinginevyo atakuletea vibwana kabla hata ya kuanza la kwanza lol
 
Duh! Huyo baba jamani anatisha. Hebu ongea nae umwambie mtoto ameshaanza kumuogopa.
Wewe hukosei.
 
Hata kama unataka kumpiga mtoto, vibao si sahihi unaweza uka over do.
Miaka minne saizi yake kichelewa tu.

Ila kuchapa suna, kumwelewesha lazima, vinginevyo atakuletea vibwana kabla hata ya kuanza la kwanza lol

Unataka kusema mtoto wa miaka mingapi ndo anafaa kuchapwamaana enzi zetu ilikuwa sio kuchapwa tu,mtu ulikuwa unakimbizwa na panga kabisa
Mimi mapanga yalishanikosa kosa sana
Sijui ningekuwa nauzaje sura mjini hapa loh
 
mtoto anapoonywa mara tatu na kurudia kosa anastahili adhabu mbadala, ila huyo baba amchape mtoto kwa kiasi cha umri wake, miaka minne bado mdogo, ujiti wa mbaazi tu unatosha, auchelewa kama alivyosema kongosho, tena unamchapa kidogo.........

Zungumza na babie mwana apunguze kipigo
 
Pole sana baba yake ni Afande nini?
hatakiwi kuwa mkali sana kwa mtoto kuna stage ambazo mtoto anapitia hizo za kulisha midoli na kusambaza vitambaa ni mambo madogo kwa mtoto katika ukuaji
Saidianeni kumfundisha na sio kamwaga maji kibao cha kushitukiza ..Mwisho mtamkomaza mtoto na viboko.
 
Back
Top Bottom