Hivi Makamba anawaza nini?Hii ya juzi amenishangaza!

kizazi kipya

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
327
62
Yusuph Makamba Katibu mkuu wa CCM amenishangaza.Ilikuwa wakati akihojiwa na waandishi wa habari katika maandalizi ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM.Ni pale aliposema eti lengo kuu la CCM ni kushinda uchaguzi na kuchukua dola basi.Makamba hakugusia kama CCM ina lengo lolote la kubadili maisha ya mtanzania.Hilo halipo katika CCM.kweli CCM haitufai........tunapaswa kufanya kitu.
 
KK, Hata mimi nilimsikia, nikajiuliza hivi ni kweli hilo ndio lengo la msingi la CCM. Kama ni hivyo nadhani hatuhitaji tena malaika atoke mbinguni aje kutuambia kuwa CCM imekufa sasa.
 
Yusuph Makamba Katibu mkuu wa CCM amenishangaza.Ilikuwa wakati akihojiwa na waandishi wa habari katika maandalizi ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM.Ni pale aliposema eti lengo kuu la CCM ni kushinda uchaguzi na kuchukua dola basi.Makamba hakugusia kama CCM ina lengo lolote la kubadili maisha ya mtanzania.Hilo halipo katika CCM.kweli CCM haitufai........tunapaswa kufanya kitu.

Halafu likaanza kuimbisha kwaya!? Senile dementia bila shaka.
 
Kama hujui njia unakamata usukani wa nini?? ccm wakijashtuka watajikuta katikati ya pori wasijue njia ya kutokea kwa viongozi wenye maono ya namna hii..
 
ndio maana mpaka sasa tz bado tu nyuma kimaendeleo,ccm hailengi kumsaidia mtz badala yake inawaza kuchukua dola.
 
wanapoendelea kuboronga ndiyo wengine wanachukua nafasi,hukumu ni 2015.
 
Kwakuongeza tu pia nilimsikia akisema kua eti kiongozi ambaye hata kidhi mahitaji ya mwananchi basi hana nafasi ndani ya CCM kua kiongozi! sasa hii si kama kula matapishi yake mwenyewe? hizo ahadi walizomuahidi mwananchi je wameshaanza kuyatimiza? Danganya toto halafu akaanza kucheza ile ngoma za kwao mbele ya wale watoto jamani Mkamba kiboko!
 
Yusuph Makamba Katibu mkuu wa CCM amenishangaza.Ilikuwa wakati akihojiwa na waandishi wa habari katika maandalizi ya sherehe za kuzaliwa kwa CCM.Ni pale aliposema eti lengo kuu la CCM ni kushinda uchaguzi na kuchukua dola basi.Makamba hakugusia kama CCM ina lengo lolote la kubadili maisha ya mtanzania.Hilo halipo katika CCM.kweli CCM haitufai........tunapaswa kufanya kitu.
Mara nyingi mwanajeshi mawazo yake ni kushinda haijalishi kaua wangapi njiani.
 
Kumbukeni ndie mtendaji mkuu wa CCM tena kinaongoza dola. Pia mwenyekiti wake JK (tena Rais) aliwahi kuulizwa kwanini Tanzania ni maskini ilhali ina raslimali nyingi akajibu :hata mimi sijui" hahaha sicheki kwa kufurahi ila nasikitika mwenyekiti na katibu wake hawajui watendalo.. Mungu atusaidie
 
na hilo neno dola,anamaanisha wakishaishika waitumie vizuri kuhakikisha kwamba wanajiweka salama ili waweze kutunyonya vizuri,kweli anaturudisha kwenye enzi za machifu,waendelee kumwacha huyu mzee maana anawamaliza taratibu kwa kutokujua kuzisoma alama za nyakati
 
Yap. Mzee kaongea ukweli. kwani ndo lengo la chama chake. Na hili ni kweli kabisa kwani hakuna maendeleo kwa taifa. Mzee kasema ukweli, tumpongeza kwa ukweli wake.
 
Ahhhh!!!
Mnamjadili mtu ambaye ashazeeka kiakili na mawazo......Wazee kama makamba hawana mawazo ya kuongoza nchi katika dunia ya utandawazi now...mambo yamebadilika sana
LABDA....Kama unataka ushauri kama wa kuoa au wa mambo ya familia unaweza kumcheki
 
ahhhh!!!
Mnamjadili mtu ambaye ashazeeka kiakili na mawazo......wazee kama makamba hawana mawazo ya kuongoza nchi katika dunia ya utandawazi now...mambo yamebadilika sana
labda....kama unataka ushauri kama wa kuoa au wa mambo ya familia unaweza kumcheki

safi sana
 
huyo mzee sio mzima, hata kwenye kipindi cha kampeni yao alikua anaropoka ropoka bila kufikiria madhara ya maneno yake
 
jamani uzee kiboko,ni kushindwa kutambua tu .ukiona uzee unaizidi akili yako na hekima ulionao kwa watu nenda kwa wjukuu punzika.
 
Back
Top Bottom