Hivi majiko ya mafuta ndivyo yalivyo au langu tu?

G M S

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
502
53
Wadau mie nna jiko la mafuta(wengne wanaita la mchina) nikizima tu moshi chumba kizima nimewahi kubadili tambi lakini bado hivi ni majiko yote au?
 
Nani kakwambia upike chumbani, mnatafuta madakesi wenyewe. Kawaida mchina haaminiki.
 
Wadau mie nna jiko la mafuta(wengne wanaita la mchina) nikizima tu moshi chumba kizima nimewahi kubadili tambi lakini bado hivi ni majiko yote au?

unapikia chumbani kuogopa kukaribisha majirani!!!ama kweli maisha yamekuwa magumu,siku hizi watu hatupikii jikoni!!!
 
zamani zilikuwepo wakiziita stovu, ck hizi hazipo. bali ni hatari sana kupikia chumbani ni heri ukumbini hata kama unakalangiza dagaa ucjali, mjini huulizwi umekula nini waulizwa umevaa nini.
 
badilisha tambi na uhakikishe hizo tambi hazishiki maji. Halafu ukitaka kulizima litoe nje maana moshi wake sio mzuri kiafya. Tahadhali usiliweke chini ya kitanda
 
wakati mwingine mafuta yanakuwa yamechakachuliwa kidogo...zimia nje acha mambo ya ajabu ya kuzimia ndani. ule moshi sio mzuri kwa afya kabisa.
 
Uwe unazimia nje! Na kwanini wapikia chumbani jamani? Moshi wowote sio mzuri kiafya!
 
Nadhani mafuta
yanachangia
nimenunua gas
ajili nilichoka
sufuria zlikuwa
km napikia kuni!
Af kwanini wapikia ndani? Nyie ndo
tunakutana daladalani mnanuka
mafuta na mamoshi
ya mchina!
 
Nadhani mafuta
yanachangia
nimenunua gas
ajili nilichoka
sufuria zlikuwa
km napikia kuni!
Af kwanini wapikia ndani? Nyie ndo
tunakutana daladalani mnanuka
mafuta na mamoshi
ya mchina!

daladalani?mamoshi?Bakita hawana maneno hayo katika kamusi ya kiswahili sanifu!
 
Uwe unazimia jiko hilo nje,sufuria zenyewe zinakuwa nyeusi ka unapikia kuni.
Ndivyo yalivyo,nimebadilisha kwa kudhani ni mabovu mpaka nimechoka nimeamua kununua jiko la gesi.
 
Wadau mie nna jiko la mafuta(wengne wanaita la mchina) nikizima tu moshi chumba kizima nimewahi kubadili tambi lakini bado hivi ni majiko yote au?

Nilijaribu kutumia haya majiko ya mafuta ya taa nikashindwa, ukipikia chochote kinaleta harufu ya mafuta ya taa.
 
daladalani?mamoshi?bakita hawana maneno hayo katika kamusi ya kiswahili sanifu!

zamani maneno hayo
hayakuwapo,kwa sasa
yapo na mengine mengi
tuu!! Umeelewa
lakini unataka
kukataa sikulazmishi!
Endelea na kamusi
yako ,na mi nakamatia
yangu!tutatoboa
tuuu!
 
Ukijua kutumia Jiko la Mafuta ya Taa wala hutapata shida, ukitaka Sufuria zisichafuke unatakiwa uwashe jiko likishawaka unachukua muda kama Dakika Mbili bila kubandika Sufuria, baada ya hapo ukibandika Sufuria yako haitachafuka kamwe.
 
Back
Top Bottom