Hivi mahakama ya mafisadi iliyokuwa pale Mawasiliano bado ipo? Imefanya kazi kwa mwaka 2023 mbona hakuna kesi iliyoripotiwa kutoka ukanda huo?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Magufuli aliamini mapambano dhidi ya rushwa ni kuunda mahakama maalum. Lakini alisahau kwamba wala rushwa na watoa rushwa ni watawala na siyo wananchi. Wakati anatawala watawala waliokuwa wanapelekwa mahakama ya mafisadi ni wale waliokinzana kimtazamo na yeye na utawala wake.

Kwa bahati mbaya baadhi ya mafisadi walioundiwa mahakama walikuwa viongozi wa Mahakama. Kwa kuwa mahakama hiyo haikulenga kupambana na rushwa bali kupambana na wapinzani wa serikali rushwa ilizidi kuwepo na inaendelea kuwepo.

Kwa sasa baada ya utawala wa JPM tulitegemea mafisadi wafikishwe mahakama yao lakini tumeona ukimya wa mahakama hiyo kwa mwaka 2023. Hizi ni tafsiri kwamba muda na uhai wa mahakama hii umeisha hadi pale wanasiasa watakapokorofishana. Wasipokorogishana kifisadi mahakama itakwenda likizo kama ambavyo leo hii tunaona ipo likizo.

Swali, wanaofanya kazi katika mahakama hiyo wanafanya kazi gani? Kwanini wasipangiwe vituo vingine vya kazi? Yale majengo wanaweza wakapewa hata hospitali ya Sinza kupanua huduma za afya.
 
Swali zuri sana Mkuu.

WAHUSIKA NADHANI WATAKUJIBU SWALI LAKO.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Kuna wanaomini Magufuli aliwahi kupambana na mafisadi. Ukweli ni kuwa Magufuli Hakuwahi kupambana na ufisadi wowote, zaidi ya kulipa visasi kwa matajiri waliomdharau kipindi ni waziri. Sana aliishia kupambana na matumizi ya neno fisadi ili kuhadaa umma kuwa kamaliza ufisadi.
 
Magufuli aliamini mapambano dhidi ya rushwa ni kuunda mahakama maalum. Lakini alisahau kwamba wala rushwa na watoa rushwa ni watawala na siyo wananchi. Wakati anatawala watawala waliokuwa wanapelekwa mahakama ya mafisadi ni wale waliokinzana kimtazamo na yeye na utawala wake.

Kwa bahati mbaya baadhi ya mafisadi walioundiwa mahakama walikuwa viongozi wa Mahakama. Kwa kuwa mahakama hiyo haikulenga kupambana na rushwa bali kupambana na wapinzani wa serikali rushwa ilizidi kuwepo na inaendelea kuwepo.

Kwa sasa baada ya utawala wa JPM tulitegemea mafisadi wafikishwe mahakama yao lakini tumeona ukimya wa mahakama hiyo kwa mwaka 2023. Hizi ni tafsiri kwamba muda na uhai wa mahakama hii umeisha hadi pale wanasiasa watakapokorofishana. Wasipokorogishana kifisadi mahakama itakwenda likizo kama ambavyo leo hii tunaona ipo likizo.

Swali, wanaofanya kazi katika mahakama hiyo wanafanya kazi gani? Kwanini wasipangiwe vituo vingine vya kazi? Yale majengo wanaweza wakapewa hata hospitali ya Sinza kupanua huduma za afya.
Ufisadi hufanywa na high profile citizens... sio wananchi au vibaka!

Afrika jinai kwa high profile citizens tafsiri yake hutegemea na nani yupo ikulu.
 
Back
Top Bottom