Hivi kweli watu wa Bukoba hawawezi kuzikana?

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Ndugu wanajamvi mtakumbuka Mara baada tetemeko kutokea serikali ilikimbia mbio kwenda kuandaa mazishi ya waliokufa ktk tetemeko hilo kitaifa.

Watu wengi tukategemea kinachofuata ni serikali kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo walau tuu hata kufanya upembuzi wa watu wasio na uwezo kabisa ili iwasidie kurudisha hali za maisha yao na utu wao.

Lakini kinyume chake serikali pamoja na kupata misaada mingi na ikijigamba kwamba pesa inazo imewaacha watu wakilala nje na kuhatarisha afya zao ikisema serikali haina mpango wa kumjengea MTU nyumba.

Hivi serikali iliona ni muhimu kufanya maziko ya kitaifa kuliko kusaidia walio hai wasife? Au waliona watu wa bukoba wameshindwa kuwazika ndugu zao?

Je, likitokea tena tetemeko likaua tena watu ambao wapo ktk majengo mabovu serikali itaenda tena kuzika kitaifa?

Ndio tuseme serikali inasubiria na kusaidia wafu kuliko kuwasaidia walio hai? Bila shaka utaona wanafanya siasa ktk maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom