Hivi kwanini Watanzania huwa tunarudia makosa yale yale miaka nenda rudi.

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,797
28,467
Ndugu zangu mnajua fika rasmilimali pekee tulizonazo ambazo tungekuwa na viongozi wenye maono zingetutoa kwenye umasikini,Madini,mbuga (utalii),bahari & maziwa na bandari.

Taarifa zinaonesha Rais Mstafu Mkapa alibinafisisha Migodi ya madini ya dhahabu ya Mkoa wa Geita & Mara,Mgodi wa Almas-Shinyanga na mgodi ya makaa ya mawe kwa miaka 99.

Shukrani kwa Magufuli amejitahidi jitahidi kidogo kurekebisha baadhi ya bitu angalau kwa sasa tunapata Mara 4 ya kile ambacho tulikuwa tunakipata mwanzo kutoka kwenye madini kama mapato sijui kama kwenye miaka aliweza kubadili maana hii Nchi kila kitu ni siri.imagine madini yenu but mikataba yake na uendeshaji wake ni siri anazojua Rais na cabinet yake.

Rais Mwinyi na Kikwete wao pia wakaanza kucheza na maliasili zetu,wanyama walianza kusafirishwa kwenda Asia na Ulaya katika kipindi cha Mwinyi na kikwete mpaka twigs wakapanda ndege.tukumbuke huyu Kikwete amewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Nishati katika kipindi cha Mwinyi na Mkapa.yani jamaa alihakikisha anatumia hizo fursa kutupiha vilivyo kuanzia huko kwenye nishati mpaka kwenye wanyama.

Ni kipindi cha Kikwete huyu huyu ndio uvuvi wa meli kuyoka Asia,zilikuwa zinabeba samaki wakubwa matani na matani na kupeleka ulaya na Asia.hapa napo angalau Magufulu alilekebisha angalau Watanzania tukaanza kula samaki wakubwa.

Sasa baada ya migodi,mbuga,bahari na maziwa kote kujaaa uwekezaji wa mkataba ya miaka na miaka.na kwenye nishati tayari makampuni yapo yanakula-tulicho bakiza ni kwenye bandari ndipo fedha zinaweza kupatikana watu wakapa percent Fulani.Jamani kweli unaenda kutoa mkataba usio na kikomo just kwa mtaji wa uwekezaji trillion 4???????? Kwa miaka 100??????

Hivi kwa nini hawa tunaowachagua kuwa Marais wetu,wanatuchezea namna hii na sisi tupo tu tumekunja Nne-Mwinyi,Mkapa,Kikwete wamebinifisha kila kitu na sasa Mh.SAMIA anaend kufanya yale Yale.
 
Ukisema Watanzania, unatuonea! Sema Ma ccm, au Mambuzz! Hayo ndiyo miaka nenda yamekuwa yakiingia mikataba ya hovyo na wageni, kwa manufaa ya matumbo yao! Badala ya manufaa mapana ya Taifa.
 
Tutaendelea kurudia makosa Yale Yale as long as Mafisadi nyangumi, Wala rushwa na watu wasio na uchungungu na Tanganyika wako kwenye vyeo vya uongozi.
Mbalamwizi
Madelu
Kipara Ole maropes
Mchele ngekewa na saboofer.
 
Mwaka fulani shughuli nyeti kama uondoshaji wa shehena za madini na makinikia ,nyara za serikali kwenda nje, Rais Magufuli alichukua hili jukumu liwe kwa serikali .

Hao wakina Lissu na Chadema wakaja kusema kwamba serikali haifanyi biashara yeyote itabidi wapewe private ,huoni akili zao hata hawa wapinzaji ni zero...

Alipoingia huyu mpya akafuta na kubadilisha huu utaratibu serikali ikapokonywa sasa wampewa private.

Hoja yangu wapinzani mbona hawaeleweki na hapo ndo fursa wnaapewa private ,si walisema serikali haifanya biashara bali inatoa huduma.
 
Hayarudiwi kwa bahati mbaya (BUT) on purpose !!! Na itaendelea kuwa hivyo mpaka pale waathirika watakaposema imetosha !!!
 
Back
Top Bottom