Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Wiki iliyopita nilimwona katika TV Profesa Lipumba akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ulioitishwa na Idara ya Maelezo kutoa maelekezo namna ya kurpoti habari katika kipindi cha kampeni.
Akizungumza katika kongamano hilo la siku moja Lipumba, pamoja na mambo mengine, alisisitiza umuhimu kwa vyombo vya habari kufuata maadili na kuandika yaliyo ya kweli, bila upendeleo na ushabiki wa kisiasa.
Tatizo langu na hawa CUF ni kwamba ni zaidi ya miaka 18 sasa tangu chama kingie mambo ya siasa, inakuwaje hakina hata gazeti lake, achilia mbali radio au TV? Mpaka lini chama hichi kitategemea huruma ya vyombo vya habari binafsi (na vya serikali) kuandika habari ya chama hicho bila upendeleo?
Si dhani kama ni tatizo la pesa kwani CUF imekuwa inapata mamilioni ya fedha kila mwezi kama ruzuku lakini hawakuwa na mpango wowote wa kuanzisha angalau hata gazeti – au hata mmoja wa viongozi wake wenye fedha kufanya hivyo.
Kuanzisha gazeti hakuhitaji fedha nyingi sana – Kubenea, mwaka 2006 aliweza kuanzisha gazeti lake na sasa linauza nakala nyingi kila toleo kupita magazeti yote hapa nchini kuachilia yale ya udaku.
Chadema wana gazeti lao – Tanzania Daima – ingawa inaejulikana kama ni la Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho.
Lakini kama tunavyoona sasa hivi, gazeti hilo linakisaidia chama hicho kutokana na propaganda za vyombo vya habari vya serikali na chama tawala pamoja na vile vinavoonekana kununuliwa na chama tawala. Na hivi sasa nasikia linauzwa kama njugu – bila shaka kutokana na kuandika ukweli kuhusu matukio mbali.
CUF ina viongozi wasomi, na waliobobea katika masuala ya siasa na kufanya publicity. Vipi kasoro yao hii hawaioni? Profesa, Maalim, hamad Rashid na Jussa – hela mnapeleka wapi? Msikae kulalamika tu – kuweni na chombo chenu.