Hivi kuna umuhimu wa magari yanayosindikiza misafara ya viongozi kukimbizwa kiasi wanavyofanya sasa?

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Juzi tu tumesikia kwamba msafara wa VP umepata ajali na kwa taarifa nilizosoma leo kwenye gazeti ni kwamba askari polisi wawili wamefariki na wengine hali zao ni mbaya hospitali. Nimekaa nikajiuliza hivi kuna umuhimu kwa haya magari yanayosindikiza viongozi kukimbizwa kiasi wanavyofanya kwa sasa? Je kuna hatari gani ndani ya Tanzania yetu hii ya leo inayowafanya wawe wanakimbizana kiasi hicho?
Kwa maoni yangu sasa hawa viongozi wajifunze kutokana na tukio hili lililosababisha vifo vya watu ambao pengine kuna ndugu zao waliokuwa wanawategemea na kwa sasa wamebaki wakiwa. Sioni umuhimu wowote wa hii misafara kutimua mbio kama wanakimbia vita au ugaidi!
 
Barabara zenyewe zimejaa matuta njia nzima kama ni kuogopa msafara kushambuliwa jamaa si wanavizia sehemu zenye matuta halafu wanafanya vitu vyao? Kwa kweli nami naona ni manjonjo yasio ya lazima kwa hali ya Usalama wa nchi yetu zaidi ya kusababisha ajali kama tulivyoshuhudia juzi!
 
kila nikiangalia hii misafara naona hamna la maana kama mtu akiamua kurusha bomu au kufyatua bazuka msafara mzima unateketea...
 
Waache waendelee kukimbizana tuu gari watembeleazo huwapa nyege ya kuzikimbiza.Huwa wanataka mpaka ile 280 waimalize kabisaa.
Kwa jinsi barabara zetu zilivyo kimeo naombea tuu yaje kumkuta yule ******.
 
Make***de yao,wanakimbizana kwa barabara ipi yenye kiwango?Mapumbavu matupu,nani ana muda wa kuja kuua kiongozi wa ki-nchi maskini namna hii?malimbukeni tu.
 
Wanapataga taarifa za kiinterijensia kuwa al-shabab wapo nchini kwa hiyo wanaona wakimbie vile kama kuna mtu anawafukuza kwa nyuma. Dawa yao nikutegesha mimawe njiani
 
Mimi nadhani kuna sababu kuu mbili
1. Ukosefu wa umakini miongoni mwa viongozi na wale wanaowapangia safari kuhusu distance, ubora wa barabara, traffic jam,makona na milimia. Hii nipamoja namadereva kutojua njia wanayoipitia kujua wanede muda gmwendo gani wa kasiili wafike mahali husika kwa wakatimuafaka
2. Kuna woga hasa miongoni mwa viongozi wenye kashifa -wanaogopasniffers! Just kidding

Leo hii nimetoka Dar kuja hapa Dodoma. Kama mjuavyo kesho bunge linaanza. LAKINI Ungeweza kushuhudia ukimbizaji wa magari -utadhani wako kwenye East Africa Safari Rally! Si mbunge, watu wa usalama, waziri au naibu wake...magari yote yako mwendo kasi! La kushangaza, leo barabara hususani Kibaha hadi Chalize na pande za Morogoro kulijaa trafiki (usalama barabarani) hakuna gari la viongozi (wabunge, mawaziri) limesimamishwa kwa ku-over speed! Sijui hii ni nini!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunasimamishwa sisi wanyonge tu. Viongozi barabara zao na hao matrafiki ni wao pia. Kwa kweli inasikitisha sana kuona roho za watu zinapotea bila sababu ya msingi.
 
Waendelee tu na mispidi yao kitakacho wakuta kibaya iwe furaha kwa wengine
 
Hivi hata huyo Makamu mwenyewe alienda kwenye mazishi ya hao vijana waliopoteza maisha yao kwa sababu ya kijinga ya kukimbiza gari kisa usalama? sehemu yenyewe iilikuwa Tanga mtu mwenyewe Makamu nani ana muda wa kumdhuru mtu asiye na impact yoyote nchini zaidi ya kuwa busy kuzindua sijui shule sijui mabwawa sijui nini??
 
Back
Top Bottom