Wakati wa Prof Muhongo,wakipigia upatu mradi wa gesi ya mtwara,akisaidiwa na wanasiasa wa vyama vyote mfano akina Zitto,waliahidi kuwa huu mradi ukianza hakutakuwa na mgawo wa umeme tena.
Na gharama za umeme zitashuka sana.
Miaka michache baadae,ni kama nchi ndiyo imepata Uhuru.Mgao sasa ni zaidi ya wastani wa saa 72 kwa wiki.
Mh Magufuli alipoingia,alifikia kuwatuhumu baadhi ya wanasiasa waliotumika kuhujumu suala la umeme,hadi kuamua kuyafungulia maji mabwawa ili maji yapungue wakate umeme.Kusema kweli kwa miaka yake mitano,hakukuwa na shida ya umeme kabisa.
Mara tu Magufuli alipoondoka,wajuaji walianza kukata umeme hovyo hovyo wakimlaumu eti alikuwa hafanyi service ya mitambo.Wao wakaanza service tukiwa gizani.Tukapewa muda wa service na ahadi kuwa umeme hautakatika hovyo tena baada ya service hiyo.Muda ukaisha,matatizo ndiyo yakaongezeka.
Tukaambiwa mabwawa hayana maji.Mungu si Athuman,mvua zilianza kunyesha tena sana,tatizo halikuisha.Tukaambiwa mvua hazinyeshi kwenye mabwawa.Hata hivyo naamini Mungu alichukizwa na akaamua kuleta mvua za mafuriko kila mahala.Bado tatizo halikuisha.
Ndipo Rais akaja mbele ya umma na kuahidi tatizo hili litaisha baada ya miezi sita.Nakumbuka ilikuwa mwezi wa nane ama wa tisa mwaka jana.
Leo miezi sita inaisha hakuna hata dalili ya tatizo kuisha badala yake hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
Katika hali ya kusikitisha kabisa,nimesoma taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa,bunge limewapa serikali hadi mwezi Juni, tatizo la umeme Liishe eti kwa kuwa serikali waliahidi litaisha mwezi Juni!
Hivi watanzania ni mimi huenda sikumuelewa mama alivyoahidi kuwa litaisha baada ya miezi sita na kumbe alisema litaisha mwezi wa sita!
Kama kuna mtu anawaelewa wanasiasa,anisaidie kuelewa maana ninajikuta nikiamini hawa jamaa huenda wana unasaba na shetani kabisa.Ni vigumu kuwaelewa.Wanatumia kanuni ya ku confuse watu hususan tunaotawaliwa.