Hivi kipi kinasababisha Vyuo Vikuu Tanzania havipo kwenye vyuo bora 50 Duniani

mzee wa mazabe

JF-Expert Member
May 10, 2016
844
626
Kila nikiangalia vyuo vyetu hapa Tanzania nione katika Ubora wa vyuo bora Duniani hata 100 bora hatupo hivi tatizo nini wadau?
 
Wewe mwenyewe umejitambulisha kwa konyagi harafu unauliza nini??? Nchi iko kama unavyojionyesh a mwenyewe.

Shule iliishagaa na Mw. Nyerere. Siku hizi bora ya zamani. Hamna practicals kuanzia chekechea mpaka vyuoni, utashindana na nani?
 
Vyuo vimeingia siasa,
Wakufunzi wanasiasa,
Wanafunzi wanasias,
Viongozi wa juu wanapenyeza siasa kwenye elimua kuanzia msingi hadi vyuo

Sasa hizo product sijui unategemea zitakuwaje?
 
1. Impact ya research tunazofanya iko kwenye scale ya minor to useless.

2. Hatuna maandiko au machapisho mengi kwenye issues mbalimbali kama waliotuzidi kwa ubora.

3. Ushiriki wetu kwenye mada mbalimbali zinazotaka taaluma hasa katika mitandao ni mdogo au haupo kabisa.

Wewe utakuwa shahidi kuwa ukiandaa midahalo vyuoni hupati watu, labda uwape hela na msosi. Ila ukiandaa disco unaweza kupata hata urais wa chuo.
Mimi nimeangalia sana wanachuo, unaporaise hoja iliyokaa kitaalam au kiresearch unaonekana mnoko. Watu wanataka mjadili mademu na wasanii au movie.
 
Argument zako zina logic,sasa kama leo hii tunaambiwa tuanze jitihada za kuiweka ELIMU yetu sehemu furani hili iweze kujulikana Duniani,je itatubidi tuanzie wapi wadau.
 
Mnawekeza kiasi gani kwenye elimu yenu na utafiti ukilinganisha na nchi nyingine?
 
Nadhani ungeanzia Barani kwetu humu Kabla ya nchini,maana bara Zima hakuna chuo bora miongoni mwa vile 100 bora
 
Tafuta gamba lako mengine waachie elimu bora inaanzia kwenye uwekezaji bora katika elimu kitu ambacho bado hatuna uwezo nacho nawala hamna ulazima wakua bora kidunia.
 
Kila nikiangalia vyuo vyetu hapa Tanzania nione katika Ubora wa vyuo bora Duniani hata 100 bora hatupo hivi tatizo nini wadau?
mi nadhani cha umuhimu tuangalie chuo bora africa and then linganisha na vyuo vyetu alafu tujue nini tunakosea....angalia Rhodes,capetown university na stellenbonsch utajua kua bongo bado sana sana
 
mi nadhani cha umuhimu tuangalie chuo bora africa and then linganisha na vyuo vyetu alafu tujue nini tunakosea....angalia Rhodes,capetown university na stellenbonsch utajua kua bongo bado sana sana
kwani ubora wa vyuo unapatikana kwa kulinganisha nini?
 
Back
Top Bottom