Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 24,055
- 57,353
Kwema Wakuu!
Nimekua nikisikia hizi kauli kwenye majukwaa ya kisiasa. Lakini moja ya viongozi wa juu niliowahi kuwasikia wakisema kauli hiyo ni pamoja na Spika mstaafu Mzee wetu Job Ndugai.
Sasa kila nikisikia au kusoma ujumbe wenye maana ya nchi kuuzwa ninajikuta ninamaswali.
Miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na;
1. Kihistoria kuna nchi iliwahi kuuzwa?
2. Je ni utaratibu upi upo kisheria iwe za kitaifa au kimataifa kwa nchi kuuzwa?
3. Je wakati nchi inauzwa inaweza kuwa utashi wa viongozi au wananchi wanaweza kuamua nchi yao iuzwe kwa kupiga kura kisha iuzwe?
4. Je Madeni yanaweza kuifanya nchi Iuzwe? Au kuna sababu nyingine kubwa?
5. Kama kauli hiyo ni propaganda, kwa nini hiyo kauli hufikiriwa mara kwa mara kwa kujirudia?
6. Kwa nini wanaohofia nchi kuuzwa mara nyingi hawapo kwenye Ulaji? Je hutumia kauli hiyo kuchochea wananchi kuhusu jambo fulani?
Natanguliza shukrani kwa heshima na taadhima. Wenye majibu naombeni mje.
Wasalamu
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi