Hivi ITV na ‘Kipima Joto’ huwa wanaripoti NBS au COSTECH au huwa hazimtaji Rais ndio maana hazipiti huko?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Nauliza kufaham kila siku ITV wana kipima joto tena na takwimu juu huku wakihodi watu wasiozidi 5 na wapiga kura hawazidi 300 na wanatoa mrejesho.

Hivi hawa huwa wanazipeleka huko kupata kibali kabla ya kurusha au huwa utaratibu ukoje?
 
Kipimajoto ni maoni! Twaweza walisema wamefanya utafiti! Tofautisha kati ya utafiti na maoni dude
 
Swali lako ni la msingi. Tusubiri wanazuoni wa Lumumba waje
 
Subiri hayo maoni yaende kinyume na JIwe,ndio hapo ITV wataanza kupimwa mkojo!
Come on! Acha cheap politics. Unadhani Twaweza wangalisema ni walikusanya maoni kuna mtu angejali? Lakini ukisema utafiti lazima Sheria ya Takwimu ikubane.
 
As far as hawaulizi kama Mwenyekiti ana mvuto au lah, wakiuliza hapo tu ndio Itakua mwisho wao
 
Je kama ni maoni hayawezi kuwa na adhari kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taasisi?
Maoni ni kitu kinachobadilika kulingana na wakati pahala na matukio! Hivyo hayawezi kuwa na adhari ndo maana opinion poll mara nyingi huchukuliwa muda mfupi kabla ya tukio ikiwa ni kiashiria.
 
Come on! Acha cheap politics. Unadhani Twaweza wangalisema ni walikusanya maoni kuna mtu angejali? Lakini ukisema utafiti lazima Sheria ya Takwimu ikubane.
Sawa ndugu,ila nadhani wewe ni mgeni nchi hii!
Utafiti wa Twaweza 2016,ulionesha JPM anakubalika kwa 96%,hatukuona hizi purukushani!
Pia chukua na mifano hii!
1.Baraza la maaskofu wa KKKT
Mara zote baraza hili limekuwa likifanya kazi zake na Mara nyingine hasa wakati wa awali wa awamu ya 4 walisifia jitihada za serikali wao kama baraza,haikuwa shida!Shida ikaja walipotoa maoni yasiyompendeza mkuu,hapo wakalimwa barua na kiumbiwa baraza hilo halitambuliki!

2.Imekuwa kawaida watu wenye maoni tofauti na JPM kukamatwa na kutafutiwa makosa mengine,yaani ufukunyuliwa mpaka upatikane na kosa!Mtu unamkamata kwa lugha ya kumuudhi Rais,halafu unaenda kumpekua nyumbani,unamtaka umpime mkojo NK!Rejea Lissu,Mtatiro,......!

Awamu hii inachekesha sana!
 
Kipimajoto ni maoni! Twaweza walisema wamefanya utafiti! Tofautisha kati ya utafiti na maoni dude
Unachekesha, ina maana hizo takwimu wanazidownload kichwani mwa mtu au yale maoni maoni yake ndo wanayachakata na kupata matokeo??? Kwa nini wamelimwa barua inaeleweka hata kwa mtoto mdogo!!!
 
Back
Top Bottom