Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 551
- 1,222
Habari zenu wakuu?? Natumaini mpo salama kabisa. Okay mimi siyo muanzisha mada humu mara kwa mara ila mara nyingi nimekuwa napenda sana kusoma tu mada, story hata visa mbalimbali viinavyolweta na baadhi ya wadau wenzetu na kama itatokea nikaguswa sanaa basi mara moja moja huwa natupia comment ili mambo yawe swadakta kabisaa.
Sasa bwana mimi mwenzenu nina rafiki yangu (mwanaume ) ambaye huwa tunapeana michongo ya hapa na pale ili maisha yasonge, japo urafiki wetu una muda kidogo lakini mimi mwenzenu kuna kitu huwa sikielewi juu ya huyu mtu, huyu jamaa kama hamna mishe yeye ni mtu wakuchill sanaa ndani mpaka kuna muda huwa namuuliza " we jamaa hivi kukaa ndani peke yako huchoki??" .. yeye atakujibu mbona kawaida tu mkuu .( Hanywi pombe, hashabikii mpira kabisaaaa hata draft siyo mchezaji ni mimo ndiyo huwa namvuta twende kijiweni tukapige danari maana nipo vizuri mno kwenye huu upande basi atakuja tu na kuwa mtazamaji )
Sasa tisa kumi kilichonifanya mpaka nije humu kuwauliza ni hili, ukiachilia mbali kukaa ndani muda mrefu pekee yake. Ana tabia ya kupenda sana kusikiliza muziki, ila sasa yeye usikilizaji wake ndiyo unaonishangaza sana na nakaona nije niwaulizeni . Yaani anaweza kuplay wimbo mmoja tu huo huo akausikiliza hata kwa masaa matano mfano kuna wimbo wa costa titch unaitwa big flexa hapa naandika nimemuacha ameuplay huu wimbo, lakini nje na hapo ni mwezi sasa amekuwa akiusikiliza huu huu non -stop hata kwenye simu yake kama utaangalia most played song ni huu huu nilioutaja hapa, kabla ya hapo alikuwa anausikiliza wimbo unaitwa Dwala lam msaanii anaitwa Dj ksb. Tisa kumi namjua vizuri tu lugha anayoifahamu vizuri ni kiswahili na kiingereza cha tia tia maji ila sasa hizi nyimbo anazozisikiliza ni za kizulu hivyo najua kabisa haelewi kiimbwacho humo. Miaka yake ni 27 kwa sasa.
Sasa je hii hali ni kawaida? Maana mimi najua humu kuna watu mbali mbali ambao pengine mmeweza kukutana na watu wa namna hii na mkaweza kuwaelewa bila shida, naombeni na mimi mnisaidie maana kuna wakati nahisi mwenzangu anapitia wakati mgumu lakini nimeshindwa kujua, lengo ni kujaribu kumsaidia huyu ndugu yangu.. au ili niweze kumuelewa.
Asanteni