Elections 2010 Hivi Hapa KIKWETE ana maana gani. WHERE IS TAKUKURU?

Profesy

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
385
13
source - Habari Leo

Kikwete aahidi kutokomeza malaria kwa kuua mbu kila nyumba

Imeandikwa na Mgaya Kingoba, Musoma;
Tarehe: 26th September 2010

MKOA wa Mara utaanza kampeni ya kunyunyizia dawa ya kuua mbu katika nyumba zake zote kuanzia Oktoba mosi, mwaka huu katika jitihada za serikali kupambana na ugonjwa wa malaria unaoua watu wengi nchini.

Akizungumza katika mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi mkuu juzi kwenye Uwanja wa Mukendo mjini hapa, mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kazi kama hiyo imekwisha kamilika mkoani Kagera.


Alisema kupulizia dawa hiyo ni moja ya jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo, baada ya kutoa pia vyandarua vya hati punguzo kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.


"Tulianza kampeni ya kunyunyizia dawa za kuua mbu katika Mkoa wa Kagera na tumerudia mara ya pili…sasa kuanzia Oktoba mosi tunaanza Mkoa wa Mara na kila nyumba itapuliziwa dawa," alisema Rais Kikwete.


Alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015, Tanzania itatangaza kuwa imetokomeza ugonjwa huo, hasa Tanzania Bara baada ya Tanzania Zanzibar kutokomeza ugonjwa huo.


Alieleza kuwa mipango mingine ya serikali ni kujenga kiwanda cha dawa za kuua viluwiluwi wa mbu kwa msaada wa Serikali ya Cuba ili kukabili ugonjwa huo unaoua Watanzania wengi hasa wajawazito na watoto.


Katika masuala mengine, aliwahakikishia wananchi wa Musoma Mjini kwamba Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa itajengwa licha ya kusuasua kwa mpango huo kwa ushirikiano na Kanisa Katoliki, na mzigo huo sasa utabebwa na serikali.


Kuhusu kiwanda cha nguo cha Mutex, aliuagiza uongozi wa Mkoa kufuatilia na kujua nini kimesababisha mwekezaji aliyepewa kiwanda hicho kushindwa kukifufua, na hivyo serikali ifanye jitihada za kukifufua.


Aliahidi kuwa barabara za Musoma Mjini zitawekwa lami; kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama na upatikanaji wa dawa hospitalini.






PS - ALIKUA WAPI MIAKA YOTE MITANO YALIOPITA SAA HIZI NDIO ANAAMUA KUFANYA HIVI?
 
Anaongea as if ana serikali tayari. Hii si kamapeni ya kuomba kuura jamani Au
 
alafu TAKUKURU wanatutumia SMS eti tutoe report ya ufisadi. Hivi hii hapa sio wazi wazi ufisadi?:confused2:
 
Mi ndio maana nampongeza sana Mkapa kutompigia kampeni huyu JK maana anajua atajiabisha kwa midubwana anayoropoka ropoka wakati sheria kaishaini mwenyewe kwa mbwembwe na mabiriani watu wakala pale ikulu kisha kucheza kiduku!!! nchi haina rais hata kidogo
 
Back
Top Bottom