Hivi Dr D.W Slaa alihama CHADEMA kwa sababu Lowassa alihamia au aligombea urais kwa tiketi ya CHADEMA?

Wanajamvi,

Balozi Dr Slaa, ambaye yumo humu lakini sijamsikia zaidi ya kuona akitoa likes kwa wana ccm wenzake, alisema kuwa kitendo cha Lowassa kuhamia chadema ni sawa na “choo kuhamishiwa sebuleni”, na hivyo akaondoka chadema na kujiuzulu siasa!

Lakini Sasa Lowassa amerudi ccm, Slaa yumo humo,(anaitumikia serikali ya ccm) hivyo yuko chooni na hapo hapo sebuleni.
Hii ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe. Kwamba alipo Lowassa ni sawa na choo kikiwa sebuleni. Ni kwasababu aliamini ni fisadi kama sikosei.

Kuna wanaodhani kuwa sasa atarudi chadema. Na hii imefikia hadi kwa mwana jamvi maarufu na mdau mkubwa wa chadema humu, Salary Slip kuanzisha mada inayosema kuwa “ije mvua lije jua, Slaa asiruhusiwe kurudi chadema”. Lakini pia kuna wanajamvi wanaodhani kuwa si rahisi kwa Slaa kuachia “Keki” kwasababu ya ubalozi aliopewa na Maghufuli mara baada ya kum sapoti kwenye mbio za urais na kukipinga chama alichoshiriki kwa kiasi kikubwa sana kukijenga!

Ni wazi kuwa kurudi kwa Lowassa ccm kuna consequences zake. Mojawapo ni issue ya Dr Slaa. Sana sana ni kwasababu ya legacy yake, pamoja na jasho lake kwenye chama, na jitihada zake dhidi ya mioango ovu, na mbinu chafu za ccm. Kama ni kweli hakuwa na tamaa ya urais, na alihama chama kwasababu tu ya Lowassa kuhamia, basi shurti atoke ccm. Great thinker anayeitwa barafu , alisema kauli inayofanana na hii kuelekea kwa Dr Slaa akasema “Sasa Dr Slaa huko alipo, asiyempenda kaja”. Alimaanisha kuwa sasa wako timu moja! Na kwasababu alimkimbia kule chadema na sasa kaja ccm! Hivyo kuonyesha msimamo hapa ni muhimu sana kwa Dr Slaa na legacy yake hapa nchini!

Lakini kama alihama kwasababu alipoteza ile nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, basi ni wazi itabidi awaombe msamaha wanachadema, wanajamvi wenzetu humu ambao nao walijitoa kindakindaki kumsapoti na hata kuwa na mawazo hasi kabisa kwa baadhi yao dhidi ya chadema! Mfano Mzee Mwanakijiji ambaye kwasasa anao sapoti ccm moja kwa moja na upinzani anauogopa kama Ukoka! pamoja na MTAZAMO .

Lakini mkuu idawa yeye kidogo alikuwa bado ana “balance”! Pamoja na great thinker mwingine Nguruvi3 . Lakini msimamo wa JokaKuu pamoja na Mag3 ,hawakubadilika.

Ningependa kusikia maoni yao kuhusu hilo. Pamoja na ushauri wowote kwa Dr Slaa kama wanao!

Nisiseme mengi kwa sasa.
Slaa hakuihama chadema. Bichwa lako la habari linapoptosha.

Slaa aliihama CCM kuhamia chadema, illikuwa kama Lowassa tu lakini ngazi ya ubunge.
 
Mnafiki huyu na msaliti mkubwa kumruhusu huyu kurudi Chadema ni makosa makubwa sana ambayo ni lazima yaepukwe kwa kila hali si mtu wa kuaminika tena huyu hata kwa sekunde moja.
Makovu yanawaka moto
I tell you.Hata mimi uchungu na hasira ningesema kama wewe.
 
Kama una mapenzi ya kweli na Tanzania na unaona dhuluma na maovu mbali mbali ya dikteta na dhalimu wa magogoni yanavyoivuruga nchi na maisha ya Watanzania basi huwezi kuona tofauti.

Makovu yanawaka moto
I tell you.Hata mimi uchungu na hasira ningesema kama wewe.
 
Ukiwasoma wafuasi wengi wa Chadema humu wanapenda sana kuona Dr Slaa akirejea Chadema.

Ila hawapo tayari kuonyesha hisia zao hadharani kulingana na jinsi walivyomtenda.

Wakijenga hoja kuwa mbona aliemkimbia amerudi ccm...

Kwa kuweka kumbukumbu sawa, Dr Slaa alitangaza kuachana/kustaafu na siasa za vyama kwa maana za majukwaani...

Pili hajawahi kurudi CCM, hakuna kiongozi yoyote yule wa CCM aliempokea kama ilivyotokea kwa viongozi wengine waliorejea.

Na hata akitaka kurudi siasa za majukwaani sidhani kama anaweza kurudi Chadema..

Kashfa mlizompa 2015 zinatosha sana, endeleeni kukomaa na waliopo Chamani.

Ni mda muafaka sasa kuinua mioyo ya akina Mnyika, Nassari, Salumu Mwalimu na wengineo wenye mioyo na upendo wa dhati kwa Chadema ili kusonga mbele...

Siku Chadema watakapoyatambua mapungufu ya Mbowe ndio siku watakayopiga hatua moja mbele....
Brother hakuna kitu kilichoniumiza kama alichofanyiwa Dk .Leo hii nafikiri cdm wamejifunza jambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine inakuwa vigumu kuamini Chadema hii ya leo ndio ileile ilimpelekesha mputa Jk. Yaani hata kiwango cha ufikiri wa wana-Chadema hivi sasa ni tofauti mno na zama hizo.

Naona aidha mnam-miss Dokta Slaa au aibu imewakolea ndo maana tangu Lowassa atangaze kuhama, jina la Dkt Slaa haliwatoki mdomoni.

Ninyi ni wahuni. Kazi kubwa aliyoifanya Dkt Slaa kwa chama chenu akaishia kuambulia kebehi na matusi. Lakini yeye alivyokuwa muungwana, amekuwa hana muda wa kuongelea mapungufu yenu.

Sasa mmekimbiwa na Lowassa, mwanasiasa ambaye Dokta Slaa aliwatahadharisha kuwa ni LIABILITY, badala ya kukiri makosa yenu na kuyarekebisha, mpo bize kumwandama Dkt Slaa.

Mwacheni Dokta Slaa alitumikie taifa. Pambaneni na hali yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushalipwa hela Yako Na Jahili KINANA?

Sent using YOUR Phone remotely from ME
 
Slaa hakuihama chadema. Bichwa lako la habari linapoptosha.

Slaa aliihama CCM kuhamia chadema, illikuwa kama Lowassa tu lakini ngazi ya ubunge.
Sasa ndo nini hiki umeandika? Kwahiyo kama Dr Slaa ni kama Lowassa, na yeye alirudi ccm?
 
Aliapa hawezi kukaa chama kimoja na Lowasa, sasa sijui atahama? Mh. Mwakyembe nae alitumia air time kubwa sana kumchafua Lowasa kuliko kuelea mipango yake ya maendeleo jimboni, leo wote wanaimba wimbo mmoja, kweli siasa ni unafiki.
 
Sasa ndo nini hiki umeandika? Kwahiyo kama Dr Slaa ni kama Lowassa, na yeye alirudi ccm?
Sasa hivi kaajirIwa na serikali. Sina uhakika alipokuwa chadema kama hakuwa pia serikalini.

Kwani alipohamia chadema alijivua u CCM
 
Dr.Slaa ameondoka CHADEMA baada ya kuona kumbe CHADEMA kipo kwa ajili ya maslahi ya watu Fulani ndio maana mtu akija na mipesa yake anauziwa nafasi ya kugombea uraisi
Hawezi kurudi mwacheni apumzike nyinyi CHADEMA subirini 2020 aje kigogo mwingine na mipesa yake mumuzie kiti cha kugombea uraisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ukweli mchungu unachoma kuliko ncha ya mkuki.Natamani sasa kujua msimamo wa Dr. Binafsi ni miongoni wale waliojetenga na siasa za chadema sababu ya kile alichofanyiwa Dr. Namshukuru Mungu Sana kwa hili lililo tokea maana hata wale wachache waliokuwa wamepoteza imani kwa Dr sasa watakua wanajutia uamuzi wao.
 
Slaa alikubali fisadi lowassa kuhamia chadema, baada ya First Lady mtarajiwa kuja juu na kumlaza nje kuhusu yeye First Lady mtarajiwa kunyang’anywa tonge mdomoni kwa sababu Slaa hakuwa tena mgombea wa Urais kupitia Chadema ndiyo akabadili mawazo kuhusu ujio wa fisadi na malaya wa kisiasa kwa maslahi yake lowassa kwa kupinga ujio wake. Sikiliza kwa makini hii utube link kama una bundle ya kutosha ili uelewe kwa kina.

Huwezi kutumia ushahidi wa Gwajima kueleza mawazo, msimamo au mtizamo wa Dr. Kwanza Gwajima na Lowasa wote ni kapu moja(mshenga) aliongea hayo kuhalalisha maamuzi ovu ya baraza kuu. Ungeruhusu kichwa chako kuelewa maelezo ya Dr. Kuhusu hali ilivyokua usingeweza hata siku moja kukubaliana na hoja mfu za Gwajima
 
Wanajamvi,

Balozi Dr Slaa, ambaye yumo humu lakini sijamsikia zaidi ya kuona akitoa likes kwa wana ccm wenzake, alisema kuwa kitendo cha Lowassa kuhamia chadema ni sawa na “choo kuhamishiwa sebuleni”, na hivyo akaondoka chadema na kujiuzulu siasa!

Lakini Sasa Lowassa amerudi ccm, Slaa yumo humo,(anaitumikia serikali ya ccm) hivyo yuko chooni na hapo hapo sebuleni.
Hii ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe. Kwamba alipo Lowassa ni sawa na choo kikiwa sebuleni. Ni kwasababu aliamini ni fisadi kama sikosei.

Kuna wanaodhani kuwa sasa atarudi chadema. Na hii imefikia hadi kwa mwana jamvi maarufu na mdau mkubwa wa chadema humu, Salary Slip kuanzisha mada inayosema kuwa “ije mvua lije jua, Slaa asiruhusiwe kurudi chadema”. Lakini pia kuna wanajamvi wanaodhani kuwa si rahisi kwa Slaa kuachia “Keki” kwasababu ya ubalozi aliopewa na Maghufuli mara baada ya kum sapoti kwenye mbio za urais na kukipinga chama alichoshiriki kwa kiasi kikubwa sana kukijenga!

Ni wazi kuwa kurudi kwa Lowassa ccm kuna consequences zake. Mojawapo ni issue ya Dr Slaa. Sana sana ni kwasababu ya legacy yake, pamoja na jasho lake kwenye chama, na jitihada zake dhidi ya mioango ovu, na mbinu chafu za ccm. Kama ni kweli hakuwa na tamaa ya urais, na alihama chama kwasababu tu ya Lowassa kuhamia, basi shurti atoke ccm. Great thinker anayeitwa barafu , alisema kauli inayofanana na hii kuelekea kwa Dr Slaa akasema “Sasa Dr Slaa huko alipo, asiyempenda kaja”. Alimaanisha kuwa sasa wako timu moja! Na kwasababu alimkimbia kule chadema na sasa kaja ccm! Hivyo kuonyesha msimamo hapa ni muhimu sana kwa Dr Slaa na legacy yake hapa nchini!

Lakini kama alihama kwasababu alipoteza ile nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, basi ni wazi itabidi awaombe msamaha wanachadema, wanajamvi wenzetu humu ambao nao walijitoa kindakindaki kumsapoti na hata kuwa na mawazo hasi kabisa kwa baadhi yao dhidi ya chadema! Mfano Mzee Mwanakijiji ambaye kwasasa anao sapoti ccm moja kwa moja na upinzani anauogopa kama Ukoka! pamoja na MTAZAMO .

Lakini mkuu idawa yeye kidogo alikuwa bado ana “balance”! Pamoja na great thinker mwingine Nguruvi3 . Lakini msimamo wa JokaKuu pamoja na Mag3 ,hawakubadilika.

Ningependa kusikia maoni yao kuhusu hilo. Pamoja na ushauri wowote kwa Dr Slaa kama wanao!

Nisiseme mengi kwa sasa.
Kwanza kilichomtoa Dr.Slaa cdm sio ujio wa Lowasa pekee. Bali ni kukanyagwa kwa demokrasia ndani ya cdm.

Kama ilikuwa lzm sana Lowasa kuwa mgombea basi angalau tungeitisha kura za maoni kwa wote wanaohitaji nafasi ya urais kwa tiketi ya cdm wanachama wakiona inafaa Lowasa atuwakilishe wakamchagua naamini Dr angelizika kuwa wanachadema wameamua lkn si kwa dharau ile aliyofanyiwa even me ningesusa hata Lowasa aliisusa ccm kwa sababu hiyohiyo.

Kuhusu kurudi cdm ni maamuzi yake sasa Lowasa karudi ccm ndio lkn Dr si mwanachama wa ccm hivyo haimhusu kwa sasa pindi akiamua kurudi kwenye ulingo wa siasa za majukwaani pengine kabla ya kuchagua chama atalitazama na hilo la uwepo wa Lowasa ccm but kwa sasa mpeni nafasi atumikie taifa.
Nadhani swali la kujiuliza ni wale waliomfuata Lowasa cdm ambao wengine mpaka sasa wananyazifa kadhaa je watarudi ccm ama watabaki?
 
Gwajima hakuwa pekee yake bali na mlinzi wake katika kuelezea yote yaliyojiri. Ungekuwa ni uongo Dr wa kula mihogo na GF wake wangekanusha. Hali ilivyokuwa huijui wewe ukilinganisha na Gwajima aliyekaribishwa kwenye kikao kile ili kuhakikisha kinafanikiwa na maelezo aliyotatoa hadharani yeye na mlinzi wake hakuna yeyote aliyeyakanusha kwamba si kweli.

Huwezi kutumia ushahidi wa Gwajima kueleza mawazo, msimamo au mtizamo wa Dr. Kwanza Gwajima na Lowasa wote ni kapu moja aliongea hayo kuhalalisha maamuzi ovu ya baraza kuu. Ungeruhusu kichwa chako kuelewa maelezo ya Dr. Kuhusu hali ilivyokua usingeweza hata siku moja kukubaliana na hoja mfu za Gwajima
 
Back
Top Bottom