Hivi Dr Bashiru anajua kuwa chanzo cha watu kutojitokeza kwa uwingi kwenye vituo vya kupiga kura ni CCM wenyewe?

Mbunge ama Diwani umemchagua
Tena kwa changamoto na vishawishi kibao vya kupewa rushwa ukapambana navyo ukawa na msimamo mmoja wa maslah ya Chama na wananchi ukachagua unaemtaka tena kwa mapenzi makubwa ukawashawishi na baadhi ya watu wengine wampigie kura
Mwisho wa siku unasikia mtu kilahisi kilahisi Mimi najiudhuru naunga mkono baada siku kadhaa huyo huyo anatangaza nia ya kugombea tena
Awamu iliyopita Ushagalamika sana
ili yeye ashinde kwa maslah ya Chama chako na wannchi kwa ujumla
Kisha ulud tena ukapige kura ukapige debe ili iweje ukiacha sababu ya usimamizi mbovu wa tume ya uchaguzi vitisho nk,,,
Hii nayo inachangia
 
Nimemsikia Dr Bashiru akilalamikia sana huko Morogoro kuwa watu wanaojitokeza kupiga kura hivi sasa ni wachache sana na idadi hiyo inazidi kushuka kadri siku zinavyosonga mbele

Lakini Dr Bashiru amejiuliza chanzo cha watu hao wanaopiga kura kupungua kwa kasi hiyo ya kutisha??

Ngoja mimi nimpe jibu la moja kwa moja kuwa chanzo cha kupungua huko ni CCM wenyewe.

Nitajaribu kuelezea ni kwanini CCM ndiyo adui namba moja ya kupungua wapiga kura

1. Unapoenda kwenye uchaguzi ni lazima uyakubali matokeo ya aina 2/ ambayo ni kushinda na kushindwa. Lakini kwa Bahati mbaya sana hivi sasa CCM wanaingia kwenye hizo chaguzi wakiwa na uhakika wa asilimia 100 wa kushinda chaguzi hizo!

2. Tume ya uchaguzi haiko huru katika muundo wake, kwa kuwa kuanzia Mwenyekiti hadi wajumbe wake wanateuliwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa nchi, ambaye chama chake ni mmoja ya washindani, jambo linalofanya wananchi wakose Imani na Tume hiyo

3. Matumizi makubwa ya vyombo vya ulinzi katika chaguzi hizo, hususani Jeshi letu la Polisi, nayo inawanyong'onyeza sana wananchi. Iweje tunafanya uchaguzi ulio huru na haki kuwe na askari wa Jeshi la Polisi walio wengi kama vile nchi iko vitani?

Hizi ndiyo sababu zangu juu za watu kutokwenda kwenye vituo vya kupigia kura na kama hatua za haraka zisipochukuliwa, tusije shangaa katika chaguzi zijazo tukawaona Wasimamizi wa uchaguzi na askari Polisi kuwa ndiyo pekee ya watu watakaoonekana kwenye vituo hivyo wakati wa kupiga kura!

Mungu ibariki Tanzania
Toka aquilina auwawe kwa risasi kwa sababu ya uchaguzi wapiga kura wameacha kwenda kupiga kura ya nini kujitafutia kifo kwa sababu ya kura tu, uhai ni muhimu kuliko kupiga kura ambazo hazidetermine nani atakuongoza.

Kingine haingii akilini mtu mmchague ajiuzulu halafu ajr kugombea tena in few weeks inasound kama usenge Fulani hivi amazing.

Wananchi hawana machaguo tena badala yake mkurugenzi ndiye anayechagua sasa kuna haja gani ya kwenda kupiga kura wakati mkurugenzi ndiye mwamuzi wa mwisho si kupotezeana muda ?

Pesa zote za halmashauri zimehamishiwa hazina hata mnayemchagua kazi yake inabaki kuhuzuria misiba tu mnapofiwa na kumsifia rais kwenye vigenge vya kahawa kuna haja gani ya kwenda kwenye uchaguzi usio na maana.

Japo Bashiru haaminiki yawezekana haya ameyazungumza akiwa anaota tu sijui lakini
 
kwa tume hii anayekwenda kupiga kura ana moyo. wasimamizi wote ni makada. hiyo ndo inaitwa tume. kwa tume hii ya makada toka lumumba wanaccm wakapige kura wengine tutakuwa majumbani na makazini tukipambana na hali zetu...
 
Bashiru mjanja na anautumia ualimu wake kupata majibu hapa ya kwanini wapiga kura wanazidi kuingia porini!
Kama kweli ana nia njema na taifa hili awashawishi ccm wakubali katiba mpya ambayo itatoa mwanya wa kuunda tume huru ya uchaguzi na kinyume chake atulie ale posho na marupurupu manono!
 
kwa tume hii anayekwenda kupiga kura ana moyo. wasimamizi wote ni makada. hiyo ndo inaitwa tume. kwa tume hii ya makada toka lumumba wanaccm wakapige kura wengine tutakuwa majumbani na makazini tukipambana na hali zetu...
Kwa kweli hamna haja ya kupiga kura, katika mazingira ya sasa

Kwa "combination" yao CCM ya kupata ushindi ambayo ni Polisi+wasimamizi wa chaguzi+maDC&maRC........

Wapinzani hawana pa kupenyea hapo......

Ndiyo sababu hata RC Makonda, akawapongeza Polisi wa mkoa wa Dar, kwa "kuwapa" ushindi wa kishindo CCM, katika chaguzi zilizopita za Ukonga
 
Na ile kauli kwamba ninakulipa mshara, nimekupa nyumba na gari ya kutembelea alafu umtangaze mpinzani mshindi, ndio kabisa imeua morali ya watu kwenda kupiga kura.
Ingekuwa amri yangu watu wangekuwa wanakitangaza tu chama kikongwe kupita bila kupingwa ili nchi ilingane na marekani kimaendeleo
 
Binafsi nikishaipata hio kadi ya kupiga kura siku ya uchaguzi nitakua na kijana wangu tunacheza Playstation 4 kwenye 65" inches screen yetu....hahahaha
 
Wapiga kura wa sasa hivi wana maslai binafsi ya moja kwa mmoja. Ukiwa neutral sidhani kama unaweza kujianika juani kwa Mara ya pili. Hata CDM ni siwaamini. Nakaa home naangalia TV waache wajasiriasiasa wakapige kura.
 
Sasa kama box la kura linachukuliwa kituoni,linapelekwa kusikojilikana,linajazwa kura za ccm baadae linarudishwa kituoni na kura zake zinaitwa halali,kuna haja gani ya mwananchi kupoteza muda wa kusimama kwenye foleni kuchomwa jua?

Mawakala /Mashahidi wa vyama vya siasa wanabaguliwa,wa chama hiki wanakatazwa kuingia kwenye kituo kwa vikwazo mbalimbali,wanaojifanya wabishi wanapigwa mpaka kujeruhuwa,halafu ikifika saa saba ndio wanaruhusiwa kuingia,sasa hapo watu watapoteza muda kupiga kura wakati msindi ameshaandaliwa?

Dr. Bashiru ukweli wote anaujua,hata alichosema Morogoro alilenga kuibua mjadala wa kudai tume huru ya uchaguzi.
 
Exactly...............

Hakuna haja ya kuendelea kutesana kwenye foleni wakati Wasimamizi wa uchaguzi ni hawa hawa makada kindakindaki wa CCM

Ni bora tu ucheze bao siku ya kupiga kura, kwa kuwa matokeo yanakuwa tayari yeshapangwa kabla kuwa mgombea wa CCM ni "lazima" atangazwe mshindi, iwe kura zimetosha au hazijatosha!
 
usitegemee bunge linalojaa wabunge wanaotegemea kuiba kura au wanaohama vyama kwa hajili ubinafsi wao hili wawe na manufaa kwa taifa.Ndugu zangu watu wa aina hii ni wakuogopa maana kinachowapeleka bugeni ni tumbo sio kutetea wanyonge wanaowakilisha.Bunge liko pale kwa hajili ya ku debate na kufikia muafaka kwa manufaa ya taifa sio kusema HAPANA AU NDIOOO KWA KILA JAMBO
Bora lipumba akishiba akili zinamtoka njaa ikirudi akili zinakuwa sawasawa!
 
Sasa kama box la kura linachukuliwa kituoni,linapelekwa kusikojilikana,linajazwa kura za ccm baadae linarudishwa kituoni na kura zake zinaitwa halali,kuna haja gani ya mwananchi kupoteza muda wa kusimama kwenye foleni kuchomwa jua?

Mawakala /Mashahidi wa vyama vya siasa wanabaguliwa,wa chama hiki wanakatazwa kuingia kwenye kituo kwa vikwazo mbalimbali,wanaojifanya wabishi wanapigwa mpaka kujeruhuwa,halafu ikifika saa saba ndio wanaruhusiwa kuingia,sasa hapo watu watapoteza muda kupiga kura wakati msindi ameshaandaliwa?

Dr. Bashiru ukweli wote anaujua,hata alichosema Morogoro alilenga kuibua mjadala wa kudai tume huru ya uchaguzi.
Aliongea ukweli Mbowe kuwa hao wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wateule wa Magufuli wanapiga kura wao wakati mawakala wa Chadema wametimuliwa kwenye vituo na kuzijaza kwenye masanduku ya kura!

Tujiulize huyo Mkurugenzi wa NEC siku 7 alizompa Mbowe ili akanushe hadharani taarifa hiyo hazijaisha??

Na kama zimeisha mbona huyo Mkurugenzi kashikwa na "kigugumizi" kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya sheria??

Ama kweli Mkurugenzi wa uchaguzi, Dk Kihamia, safari hii kashikwa pabaya!
 
Bashiru ukweli ni huu hapa watu hawajitokezi kwasababu kinacho fanyika SIO UCHAGUZI BALI NI MAAMUZI YA WATEULE KUHAKIKISHA CHAMA TAWALA KINASHINDA IWE JUA AU MVUA LAZIMA CHAMA TWAWALA KISHINDE

Sasa nini kifanyike TOA WATEULE WEKA TUME HURU HATA UKIKAA NYUMBANI DK, BASHIRU UTAPATA MATOKEO MURUUA
 
Back
Top Bottom