Elections 2010 Hivi ccm ina dhamira ya kweli?

Masauni

JF-Expert Member
Aug 15, 2010
386
58
Nimekuwa nikifatilia mambo ya siasa, hasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi. Nimekuwa najiuliza sana nini dhamira ya CCM. Kama CCM ina dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Kwa nini inazuia vyombo vya habari (Television,magazeti na nk) kutangaza kwa ukweli mambo ya upinzani??

Kwa nini hawataki wananchi wote wafahamu na kuvisikiliza vyama vyote ili wananchi wapime ni chama gani kinachotufaa? Kama kweli CCM ingekuwa inataka kuleta maendeleo ya kweli na wanaamini wanachokifanya ni sahihi sidhani kama kunahaja ya kuzuia vyombo vya habari kusema ukweli, na kuwatisha wananchi.

Nakumbuka miaka ya nyuma Mzee wangu aliwahi kutishwa na CCM na kuambiwa ukionekana unakubaliana na sera za upinzani, utakiona cha moto,tutakapochukua nchi, na kweli mzee wangu(nikitaja jina unamfahamu) alichukuliwa hatua kali sana, ikiwemo kushushwa cheo, na baada ya kuretire mpaka leo anasumbukia mafao yake. Nauliza swali Je, hawa ndo watu wenye kuleta maendeleo ambao mnataka kuwapa nchi tena? Tuache mambo ya ushabiki, tuangalie mustakabali wa nchi yetu.

Tatizo naloliona ni kwamaba hata wananchi wengi wanafurahia hali ya rushwa na ufisadi. Nakumbuka nilipokuwa nafanya kazi katika wilaya fulani huko tanzania, wafanyakazi wengi walimchukia Dr. silaa(mwenyekiti wa kamati ya bunge ya LAARC) Simply because hawapi nafasi halmashauri ya kula fedha na anafuatilia sana mambo kwa undani!!!
 
Back
Top Bottom