Walker Water
JF-Expert Member
- Aug 23, 2022
- 785
- 2,983
Nijuavyo mimi ni kuwa,Mungu si jina bali ni cheo cha juu sana kuliko vyote duniani na ulimwengu wote.Yaani ikitokea chochote/mtu yeyote akaweza kukutimizia mahitaji yako yote pasipo kuzuiliwa na mtu yeyote au kitu chochote kile na pasipo kufungwa na muda,basi kitu hicho au mtu huyo unaweza kumuamini kama Mungu wako.
Kuhusu baadhi ya watu wanaoamini kuwa Mungu hayupo mi naona ni sawa tu na kusema nchi haina Rais na huku Rais akiendelea na kazi zake kama kawaida pasipo kumpunguzia chochote.
Sasa kabla hujajibu swali langu naomba kutoa mfano wangu kidogo; Nikiwa mtoto nilikuwa nasikia tu habari za Mungu/miungu mbalimbali zikitangazwa na kutolewa na kusimuliwa kwa nguvu maeneo mbalimbali,basi ikanibidi nitafiti na mimi kutafuta Mungu wangu maana niliamini kwa nguvu zangu sitaweza kupambana.
Basi,sikumoja nikiwa nimekaa nikasikia sauti ya Mungu wangu,narudia tena, nikasikia sauti ya MUNGU WANGU (si sauti hii ya kibinadamu ndiyo maana nasema ni ya Mungu wangu ninaye mwamini) ikiniambia kuwa nataka kuwa Mungu wako,nikamuuliza wewe unaitwa Mungu nani?,(akanitajia jina),nikamuuliza tena,"Je,wewe ndiye Mungu mkubwa kuliko miungu yote ninayoijua?,maana mimi sipo tayari kuwa na Mungu mdogo",akanijibu kuwa ndiye mkubwa kuliko yote,nikamuuliza tena,"Nitaaminije kuwa wewe ndiye mkubwa kuliko miungu yote?",akanijibu kwa kunieleza kuwa miungu yote hapa duniani ugomvi wao wote ni juu ya kumpigania mwanadamu awe upande wake ili amsujudie na kumwabudu (chunga sana Mungu unayemsujudia na hakikisha unamjua vizuri), hivyo nikiwa upande wake atanipigania vita vyangu vitakavyonijia kwa kumtii/kumsujudia maana miungu yote inaitaka hiyo nafasi.
Nilikubali na kweli vita vikali sana na vya kimwili na vikali zaidi vya kiroho nimeviona na kweli amenishindia vyote,nilivyoshindwa ni vile ambavyo aidha sikutii au sikufuata maelekezo yake kwa usahihi.
Mwisho ndiyo swali langu linakuja,Je, wewe kama binadamu ulishawahi au unaweza kuongea na Mungu wako unayemwamini?
NB;Mungu ni cheo na hivyo ipo miungu mingi sana yenye majina yao na lengo la kugombania cheo hicho ni ili isujudiwe na kuabudiwa na binadamu, yaani wewe ndiye mwananchi unayeamua unampa nani kura yako ili awe Mungu wako.
Ukiamini hakuna Mungu maana yake umegoma kupiga kura.