Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 1,706
- 3,355
Kuna wakati ilikuwa ukienda hospitali ikakutwa na maambukizi walikuwa wanakwambia uwape majina ya ulioshirikiana nao tendo hlf wao kwa muda wao wanawatafuta kwa ajili ya upimaji na tiba. Sina hakika kama utaratibu huo bado upo.
Kwa sasa bado kuna watu wengi tu huku mitaani unakuta mtu ana maambukizi lakini kwa sababu anazojijua yeye haendi kuchukua dawa za kufubaza maambukizi. Wengine wakidai wameombewa na wachungaji huko kwenye nyumba za ibada na kwamba kwa sasa wamepona!
Mimi naamini watu hawa ndo chanzo kikubwa cha wimbi la maambukizi mapya ya ugonjwa huu maana kama kila mhusika angekuwa anafuata utaratibu wa matibabu hayo maambukizi mapya yangetoka wapi?
Nashauri Wizara ya Afya Tanzania iweke utaratibu wa jamii kuwaripoti watu kama hao maana wengine unakuta kwa namna moja ama nyingine wanajulikana kwenye jamii zao kuwa ni waathirika lakini wamekataa kuchukua dawa.
Hii itasaidia kupunguza au kuondosha kabisa maambukizi mapya hasa kwa vijana wadogo ambao mara nyingi wanaishia kupata maambukizi kutoka kwa watu wazima ambao kwa sababu wanazozijua wao wamejiweka nje ya mfumo wa matibabu.
Vinginevo haya maambukizi hasa kwa vijana wadogo hayataisha kamwe.
Hlf kuwe na utaratibu wa wageni wanaotoka nchi zingine kupima maana km nchi tunapokea wageni kutoka kila engo ya dunia hii na hakuna upimaji wowote. hawa nao wanaingia na kuchangamana na wananchi wazalendo. salama iko wapi hapo? Kuwe na utaratibu wa kupima hawa wageni kabla hawajaingia nchini tuweze kulinda vizazi vyetu vijavyo.