Historia yetu, upotofu wetu na rai ya kujisahihisha

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
577
Sasa mamodi sijaelewa, nimeleta asubuhi mchango wangu na ukatokea na kupotea. Kwa kawaida mnasema kama ni kitendo cha makusudi. labda kichwa kilikuwa kibaya. kwa kuwa bado nadhani mawazo yangu yanafaa kuyatafakari kwa nia njema kabisa na kujengana kwa kuikuza amani ya nchi yetu na ili kujiletea maendeleo kwa kutumia vizuri fursa tupatayo, mtanitendea haki kutoiondoa thread yangu, kwani hapa ni mahali huru kutolea maoni ili mradi sheria haivunjwi. Kama inakugusa mod binafsi basi ni busara zaidi kuheshimu mawazo ya wengine. Hakuna tusi na wala thread haimlengi mtu binafsi au kikundi ali ni ukweli halisi kwa lugha nyepesi ambayo mtu yeyote anaweza kuielewa. Muda mzuri umetumika kuandaa mawazo hao. Kwa kuwa sielewi kwa nini habari imeyeyuka, labda ni kwa bahati mbaya, naomba kuileta tena.

Sijadili udini hapa, lakini ukitafakari kidogo tu utagundua kwamba waislam hupoteza fursa nyingi zinazopatikana kwa kutumia jazba zisizo na tija. Heri kurudi nyuma kutafakari na kujipanga upya namna ya kuendelea mbele kama kweli kuna lengo lenye maana kwa nchi na watu binafsi.

Wakati wa Nyerere Uislam ulipewa kipaumbele kwa kuhakikisha nafasi za kusoma katika mashule mbalimbali hata ya kikristo zinapatikana kwao. Hata baadaye Nyerere akaamua kutaifisha shule za misheni ambazo nyingi sana zilikuwa za kikristo, ili serikali iwe na nguvu kubwa zaidi kimaamuzi juu ya shule hizo. Nyerere alikazania sana kila mtoto anayefikisha umri wa kwenda shule aende kusoma hata kama hana hela, ili lengo la usawa litimie kwa watanzania wote. Nakumbuka watu wengi sana kama Prof Malima alisoma Minaki na kuwa kiongozi katika shule hiyo ambayo ilikuwa ya Anglican Church. hata hao kina prof Lipumba na prof Kapuya na wote unaowasikia leo walipita kwenye mashule hayo na kuishi kwa amani na wakristo pasipo misuguano mikubwa. Hata hivyo waislam waliendelea kulalamika kupitia vyombo ambavyo kimsingi, serikali ilisaidia sana kuanzishwa ili kuunganisha nguvu za waislam katika kutafuta na kutumia fursa mbalimbali. Ikafika hata waislam kulaani serikali kwa madai kwamba inawaundia vyombo kwa manufaa yake. Kiasi chake ni kweli, kwani serikali ilikuwa inatafuta namna rahisi ya kuwasaidia waislam ambao katika nyanja nyingi walikuwa nyuma ukilinganisha na wakristo.

Alipoingia Mwinyi, hapo ilikuwa kama vile kufungulia nyuki, waislam wakakunjua makucha yao kwa vile sasa Ikulu ambayo walikuwa daima wanaiona kama kanisa sasa imegeuka msikiti. Lakini kwa vile Nyerere alikuwapo akionya na kukemea sana mienendo yenye kuashiria uharibifu wa nchi, Mwinyi alikwama kuridhia mambo mengi yaliyokuwa yanashinikizwa kwake na waislam, mfano Tanzania kujiunga na OIC. Kipindi hicho prof Malima akiwa waziri wa Elimu aliitumia nafasi hiyo kuimarisha dhana potofu ndani ya waislam akiwahimiza waziwazi na kwa vimemo vilivyonaswa mara kwa mara, kwamba waislam washike nafasi nyeti nyingi na kuondosha ukristo maeneo hayo, kwa kuhakikisha nafasi za shule za nje ya nchi analazimisha wakuu wa idara zinazoshughulikia ziwapeleke waislam. Kwa kweli ni Mungu tu aliinusuru Tanzania wakati huo, labda upole wa wakristo na uvumilivu wao unachangia kuwa hapa tulipo bila kugeuka Bosnia Herzegovina. Mungu Ibariki Tanzania. Kipindi hicho cha "Mzee Ruksa" mikakati mingi ilikuwa kuigeuza Tanzania kuwa ya kiislam, misikiti ilijengwa sana, lengo likiwa kila 100m kuwapo msikiti. Bahati mbaya au kwa kukosa kibali cha Mungu, kipindi cha Mwinyi kilipokwisha kiliacha misikiti mingi ikiwa haijakamilika. Hapo udini ulichukuwa nafasi sana. Badala ya kuitumia kwa tija fursa hiyo kwa mafanikio, ikapita kwa malalamiko u, japo Mwinyi alilazimika kila mara kuwaambia waislam wasome elm dunia kwa sana wasilalamikie ukristo, akaasa wanaochoma moto vibanda vya nguruwa Mwembechai na kwengineko waache, kwamba anayekula vyura ruksa, nk. bahati mbaya tena historia inaonyesha kwamba waislam wanapenda sana kufanya mambo yao siku takatifu kwao ya Ibada, Ijumaa wakitoka misikitini, na kuichafua siku adhimu waliyojichagulia wao wenyewe kuongea na Mungu wao.

Akaja Mkapa "Mr Clean" ambaye alilazimika kufanya kazi ya ziada kurejesha uharibifu mwingi vichwani mwa watzanzania juu ya dini, umoja na maendeleo. Hapo kimya kimya mambo ya udini na nguvu ya uislam wa kuhamasisha vurugu vikaanza kupungua kwa sababu ikulu ilishageuka kanisa tena. Mambo ya udini yaliyopiganiwa sana enzi za Mwinyi yakapoapoa japo kidogo na kwa lazima kwa sababu ya kukosa msisimko kutoka Ikulu. Hakuruhusu upuzi wa kidini Mkapa, iwe kwa wakristo au kwa waislam, kwa wamakonde au kwa wakurya, kwa wazazibara au watanganyika, watu wakamsema sana anawatukana akiwaambia wana "wivu wa kijinga na ufinyu wa kufikiri, akili za kike....." lakini hawakumwelewa sababu hotuba zake alikuwa akizitoa kwa lafudhi ya kimakua alikozaliwa na kukulia, kumbe kule kwao alionekana mpole sana wakati watanzania ambao hawajawahi kuishi Mtwara na Lindi walimwona ni mkali sana kiasi cha wengine kuzima redio zao pale Mkapa anapohutubia. Uchumi ukaanza kubadilika na kuwa chanya, lakin waislam walilaani sana kwamba anawabana mno mambo yao, wakristo nao wakiendelea na harakati zao za uvumilivu, sala na maombi. Hali ya maisha hata hivyo yilibana sana, ngumu na nchi ilienda kwa fimbo ya chuma. tatizo lake kwa sana Mkapa ilikuwa kuweka kipaumbele cha kudhibiti upinzani hata kwa kuua, kama mauaji ya Zanzibar yaliyofanywa na polisi ambao akawapandisha vyeo kwa shukrani zake, kitu ambacho mpaka leo sijapata mantiki yake.

Alipoingia Kikwete, wakristo kwa waislam walijawa na shangwe na vifijo wakidhania mkombozi kaja, kiasi hata maaskofu wengine walikiri hadharani kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu (Kilaini), waislam wakajua kwamba msikiti wao umerudi ikulu ambako wataenda kwa uhuru kumsalimia mwana wao na kuhakikisha sasa mambo yaliyokwamishwa na Mkapa sasa yangeanza kutimua vumbi upya na kwa kasi mpya. Ikaja kugundulika kumbe kila king'aacho sio dhahabu. Ingawa Kikwete anadaiwa sio mwepesi wa kufanya maamuzi magumu kuhusu mustakabali wa nchi, kumbe safari zake nyingi za nje ya nchi zimekuwa zikiingiliana na waislam kufanya miamko ya ajabu huku nyuma ungedhani JK kawaruhusu lakini kwa masharti kwamba wafanye hivyo akiwa angani kwenda nje ya nchi. Nadhani kwa kukosa kuwaambia ukweli waislam kwa kuwaonyesha sura inayomaanisha bali kwa tabasamu linalowapatia waislam ujumbe tofauti na maana yake anayoikusudia (Alisema ndivyo alivyoumbwa lakini). bahati mbaya JK yupo hivyo kwa karibu kila kitu, hata wasaidizi wake wakimchefua ama ananyamaza au naye analalamika kama wafanyavyo raia wengine (labda anasahau kwamba ameshika rungu kubwa), kiasi kwamba wasaidizi wake wanatumia mwanya huo kuharibu zaidi kwa makusudi ili kunufaika zaidi. Walimshawishi akubali kutumia chama chake kuondoa vibano vya viongozi wahalifu waliobanwa kwa miiko ya viongozi chini ya Azimio la Arusha, kwa kuondosha Azimio la Arusha la kijamaa na kujitegemea wakibadilisha na Azimio la Zanzibar la kibepari na utegemezi wa ombaomba kimataifa. Hata Nyerere alililia sana kwa kusononeka kwamba anatembea na biblia na Azimio la Arusha na hajaona kasoro hata kifo chake kilipomnyang'anya nafasi ya kuongea hadharani, lakini zimwi lake linaendelea kusema sana na madhara yake yanaonekana waziwazi - Madini aliyotunza wakati wake wote sasa yananufaisha wageni kwa mikataba dhaifu na 90% inayonufaisha wakubwa. Sasa waislam kwa kisingizio cha ikulu kuingikia hata pasipo kibali wakisahau utaratibu rasmi.


Ukimya wa JK unamgharimu yeye binafsi na nchi, kwa sababu imefika wakati ambapo inakuwa kama hakuna kiongozi, kama majuzi ambapo waislam wameamua kuchoma makanisa ambayo wao wanaona ni adui wao mkuu, wamevamia vituo vya polisi na kufanya uharibifu bila kuogopa kwamba wanaigusa serikali mahali pabaya kuichokoza. Yote hayo ni kwa kutojali wakifikiri mkuu wa polisi naye ni mwana wao, mkuu wa kanda maalum DSM polisi ni mwana wao, Rais na makamo pia wana wao. Kumbe Serikali haina dini, ikawaamka usingizini na kuwashikisha adabu. Kina Ponda na wenzake wakakaribisha wageni waanzishe umoja mwingine wa uamsho unaokinzana na vyombo vingine vya kiislam na kuvuruga nchi kabisa. Hata wanapotoa matamko yao hayaonyeshi mbegu ya umoja wa nchi bali manung'uniko tu juu ya serikali ambayo wanaisingizia kupendelea ukristo ati kwa kumwaga mabilioni kujenga makanisa, kumbe ni malengo ya wakristo wenyewe kuchangiana. Mbona Nyerere alijenga msikiti Butiama wakati yeye ni mkatoliki wanaousema adui nambari one wao? Mbona Mkapa amesimamia ujenzi wa misikiti wakati yeye ni mkristo? Kumbe wangeutumia mwanya huo kuwekeza akili zao katika mambo ya kuwaendeleza wangeenda mbali sana kwa sasa. Angalia Chuo kikuu cha Waislam Morogoro, fursa nzuri ile na sasa wangefungua vyuo vikuu zaidi na sekondari na wahamasishe vijana wao kusoma na kushika nafasi nyingi za uongozi katika jamii.

Badala yake wanahamasisha watu kufanya vurugu kusambaratisha amani iliyopo kwa manufaa ya wachache wao ambayo hata viongozi wao na waislam wengi wenye busara wako kinyume na wenye uamsho. Kadhi wamepata, lakini nadhani fursa hiyo nayo hawajui waifanyie nini kwa tija, bali nayo wameanza kugombania nani anastahili zaidi kuwa kadhi. Ubaguzi wa kidini unaendelea hata ndani yao wao wenyewe hata uwamalize wote. Sasa Ponda anashughulika na ndoo Ukonga, wafuasi wake ati wapo tayari kushughulika na ndoo hadi kufa. Ujinga ni adui nambari moja wa maendeleo ya binadamu. Labda kwa kuwawanakula bure huko gerezani wanaona waendelee hukohuko. Kumuunga mkono mhalifu ambaye taratibu za nchi zinajitahidi kurekebisha mambo ni ufinyu ule ule wa kufikiri. Waislam wanahitaji kuangalia kwa umakini kiwango cha maendeleo katika nchi zote zinazotumia dini ya kiislam kama nyenzo ya maendeleo. Wana bahati mbaya sana.

Nashindwa kupata picha, kama wakristo wangejibu mapigo kwa kila uchokozi ufanywao na waislam sasa hivi sijui tungekuwa na hali gani Tanzania. Waaislam waliosoma sana elimu dunia nadhani ama hawatumiwi sawasawa na waislam wenzao au labda sumu ya ujinga uleule imetawala ndani yao kama ilivyokuwa ndani ya Prof Malima ambaye vimemo vyake kedekede vilinaswa kulazimisha wenye dini kama yeye wapangiwe shule za juu na hasa nje ya nchi na kunung'unikiwa sana wakat wake akiwa wizara ya elimu, na bado haijasaidia kuzima kabisa fursa za wakristo wanazozitafuta kwa bidii, juhudi na maarifa hata kama kwa uchache na ugumu wa kupatikana.

Niishie hapa.
 
Back
Top Bottom