Historia ya wimbo uitwao Ni Salama Rohoni Mwangu (It is Well with my Soul)

Kyatsvapi

JF-Expert Member
May 15, 2009
317
196
Wakuu,

Heshima mbele.

Nimeguswa sana 'kushare' nanyi historia ya wimbo huu unaoitwa Ni Salama Rohoni Mwangu.

Si mara ya kwanza historia hii kuandikwa hapa jamvini. Kuna mdau mmoja (Elli) alifanya hivyo mwaka 2011. yeye aliandika kwa kiingereza. Kwa upande wangu, nimetafuta tafsiri yake katika lugha ya kiswahili ili watu wengi zaidi waweze kuifahamu. Nitaweka pia vyanzo mbalimbali vya taarifa zangu sababu hakuna kitu ambacho nimetunga, bali nimevikusanya tu toka sehemu mbalimbali ili watu wengi zaidi waweze kupata uhafamu huu.


Mwanzo wa stori:

Mwandishi na mwenye kisa cha wimbo huu anaitwa Horatio Spafford na aliishi miaka 60 kati ya mwaka 1828 hadi 1888. Mtunzi wa wimbo anaitwa Phillip Bliss (Huyu sintomzungumzia kabisa katika stori hii) Horatio Spafford, alikuwa mwanasheria na alikuwa tajiri sana. Aliishi na kufanya biashara zake huku Chicago, Marekani. Alikuwa na familia ya watoto watano, mabinti wanne na mvulana mmoja. Pia alikuwa ni mkristo na mwanafunzi mzuri wa maandiko matakatifu.


Majaribu yanaanza:

katikati ya mafanikio yake, Horatio alimpoteza kijana wake mwaka 1870 aliyefariki kwa ugonjwa uitwao scarlet fever unaosababishwa na bakteria. Akiwa bado anaendelea kuomboleza kifo cha mtoto wake mpendwa, tarehe 08 Oktoba 1871 (Jumapili) majira ya saa tatu usiku, moto mkubwa uliopewa jina la Moto Mkubwa wa Chicago (Great Chicago Fire), ulianza na chanzo chake inasemekana ni ng'ombe aliyepiga teke taa ya mafuta iliyokuwa katika banda lake. Moto huo ulisabisha vifo vya watu takribani 300 na uliteketeza eneo la karibu kilomita za mraba 9 (9 kmSQ) na uliacha watu zaidi ya 100,000 bila makazi. Ni katika ajali hii ya moto, bwana Horatio alipoteza mali zake nyingi sababu aliwekeza sana katika eneo hilo la Chicago.


Katikati ya Majaribu:

Wakati biashara za Horatio zinaanza kukaa vizuri, janga lingine likampata. Mwaka 1873, biashara zake zikakumbana na anguko kubwa la uchumi lililoendelea hadi mwaka 1879. Anguko hili la uchumi lilisababishwa na sababu nyingi ikiwemo Moto mkubwa wa Chicago wa mwaka 1871.

Kutokana na matatizo yote ambayo familia yake ilipitia, Horatio aliamua kuipeleka familia yake nje ya Marekani kwa ajili ya mapumziko na kubadilisha upepo. Wakaamua kwenda Uingereza ambako pia rafiki zake Moody na Sankey walikuwa wanafanya huduma ya kuhubiri injili. Muda mfupi kabla ya safari yao, alipata udhuru na ikambidi abaki ili kushughulikia masuala yaliyokuwa yamejitokeza katika biashara zake. Kwa kuwa muda wa safri ulukuwa umekaribia sana, aliiruhusu familia yake itangulie na kwamba yeye angefuata baadaye. Tarehe 15, Novemba 1873, familia yake (mke na watoto wanne), walianza safari kutoka New York kuelekea Ufaransa na meli iliyoitwa Ville du Havre. Tarehe 22, Novemba 1873 majira ya saa nane za usiku, wiki moja baada ya kuanza safari, wakiwa ndani ya bahari ya Atlantiki, meli ya Ville du Havre iligongana na meli nyingine iliyoitwa Loch Ear. Watu 226 kati ya 313 waliokuwa ndani ya meli ya Ville du Havre, walipoteza maisha yao. Miongoni mwao wakiwemo watoto wote wanne wa Horatio. Tarehe 1, Desemba 1873, Horatio alipokea ujumbe toka kwa mkewe ambaye alinusurika katika ajali hiyo akimweleza, '...Ni mimi tu nimesalimika...'. 'Ijapokuwa kuna mali na vitu nimepoteza, nina furaha sababu bado namwamini Mungu'. Haya ndiyo yalikuwa maneno ya Horatio baada ya kupata ujumbe toka kwa mkewe.

Wiki chache akiwa njiani kwenda Uingereza alikokuwa mkewe, kapteni wa meli aliyokuwamo aliwataarifu kuwa eneo walilokuwa wanapita, ndipo ilipotokea ajali ya meli iliyouwa watu 226 wakiwapo watoto wake. Kwa majonzi na uchungu mkubwa, Harotio alichukua kalamu na karatasi, akaandika mashairi ambayo baadaye ulikuja kuwa wimbo uitwao 'Ni Salama Rohoni Mwangu' (It is well with my Soul).

Haya ndiyo maneno yake katika lugha ya kiingereza;

When peace, like a river, attendeth my way,
When sorrows like sea billows roll;
Whatever my lot, Thou hast taught me to say,
It is well, it is well with my soul.

Refrain:
It is well (it is well),
with my soul (with my soul),
It is well, it is well with my soul.

Though Satan should buffet, though trials should come,
Let this blest assurance control,
That Christ hath regarded my helpless estate,
And hath shed His own blood for my soul.

Refrain

My sin, oh the bliss of this glorious thought!
My sin, not in part but the whole,
Is nailed to His cross, and I bear it no more,
Praise the Lord, praise the Lord, O my soul!

Refrain

For me, be it Christ, be it Christ hence to live:
If Jordan above me shall roll,
No pang shall be mine, for in death as in life
Thou wilt whisper Thy peace to my soul.

Refrain

And Lord haste the day, when my faith shall be sight,
The clouds be rolled back as a scroll;
The trump shall resound, and the Lord shall descend,
Even so, it is well with my soul.

Refrain


Mwisho:

Baadaye Horatio alibarikiwa watoto wengine watatu, wa kiume mmoja ambaye alifariki akiwa na miaka minne na mabinti wawili. Mwaka 1881, walihamia Jerusalem, Israel na wakaanzisha kundi la kusaidia maskini. Kundi hili lilikuwa sababu ya mwandishi Selma Lagerlof kushinda tuzo ya Nobel mwaka 1909 kupitia kitabu chake cha hadithi kijulikanancho kama Jerusalem. Kuna movie inaitwa Jerusalem ya mwaka 1996, ambayo iko 'based' kwenye kitabu cha mwandishi huyu.

Baadhi ya nyimbo zilizoimbwa:

1.

2. NI SALAMA OFFICIAL HD MUSIC - YouTube



Vyanzo vya habari:

1. It is Well with My Soul, the Song and the Story
2. It Is Well with My Soul - Wikipedia, the free encyclopedia
2. Je Umekata Tamaa? Soma hii Story: Saved Alone
3. NI SALAMA ROHONI MWANGU. | Maisha ya ushindi
4.


Tafakari.
 

Attachments

  • reuben 8.mp3
    4.4 MB · Views: 1,039
  • reuben 7.mp3
    4.3 MB · Views: 618
  • IT IS WELL.mp3
    5.2 MB · Views: 848
  • Shangilieni-Salama Rohoni.mp3
    15.3 MB · Views: 305
Last edited by a moderator:
Asante mkuu,,,,Kwa maelezo haoyo,,,Kiukweli miaka ya Zamani watu walikuwa wanatunga nyimbo nzuri nanyingi zilikuwa zinaelezea matukio halisi ndio maana hata leo ukizickia ujumbe pamoja na sauti Unagusa MOYO,,,!
 
nashukuru mkuu,INaonyesha ni jinsi gani hata tukipata majaribu tusirudi nyuma ..tunaye yeye mwaminifu kwetu yesu Kristo ...ni story inayotufunza kwa kwel
 
yaani ukiuimba unapata hisia wewe mshindi

Ngoja nijaribu kuimba nione..

Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida,
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama moyoni mwangu

Saalamaa(salamaa)
Roohonii(rohonii)
Ni salaama rohoni mwang....

Daah!@miss neddy umeniingiza choo cha wajeda,mbona machozi yanaanza kutoka yenyewe wakati mie silii?ndo hisia za ushindi hizi mtumishi?!aargh!
 
Ngoja nijaribu kuimba nione..

Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida,
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama moyoni mwangu

Saalamaa(salamaa)
Roohonii(rohonii)
Ni salaama rohoni mwang....

Daah!@miss neddy umeniingiza choo cha wajeda,mbona machozi yanaanza kutoka yenyewe wakati mie silii?ndo hisia za ushindi hizi mtumishi?!aargh!

pole i think kuna situation inayokufanya ulie utashinda
 
Back
Top Bottom