Historia ya Wanyakyusa kufahamika zaidi kuliko Wasafwa ambao ni wazawa halisi wa Jiji la Mbeya

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
WASAFWA NDIO WAZAWA HALISI WA WILAYA ZA JIJI LA MBEYA, KILITOKEA NINI MPAKA WANYAKYUSA WA WILAYA ZA NJE YA JIJI KUFAHAMIKA NDIO WENYEJI?

Yani hii Tanzania nzima ukiuliza jiji la Mbeya linakaliwa na kabila gani, fasta mtu anakujibu wanyakyusa lakini ukweli ni kwamba wasafwa ndio wenyeji na hata hili jina la Mbeya lina asili ya kisafwa. si ajabu mtu anaweza asijue kwamba waoambnaji wakuu na matajiri wengi wa mbeya wenye maduka mengi, mahoteli, viwanda na makampuni ni wakinga lakini ukimuuliza swali mwenyeji wa hapa mbeya ni nani, atakujibu fasta tu mnyakyusa, kilotokea nini hadi ikawa hivi?

ni kwamba nchi ilipopata uhuru kulikuwa kuna wanyakyusa wengi wazawa wa wilaya za rungwe na kyela walianza kuja na kuhamia wilaya ya Mbeya mjini (kwa sasa jiji) ambako ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya, wageni wengine nao pia walikuja kuhamia mjini kupata huduma za kijamii, kusoma, kufanya biashara, n.k.

Muda huo wakazi wa mbeya mjini wengi walikuwa ni wazawa ambao ni wasafwa kundi la wamalila, shida ikaja kwamba wasafwa wakiona wageni walikuwa hawataki kuchangamana nao walikuwa wanahamisha makazi kwenda sehem ambayo wapo peke yao, mji ulizidi kuchanganya na kufanya wanyakyusa na wageni wazidi kuja mjini na ikawa usumbufu kwa wasafwa kuhama hama mji unavyozidi kupanuka, ikafikia kipindi wengine wakaanza kukimbilia maeneo ya mbali zaidi hata milimani.

matokeo yake hapa mjini makabila ya ziada yaliyokuja kama wanyiha, wandali, wakinga, wahehe, wangoni, wabena, n.k. wao wakawa wanajua huu mji ni wa wanyakyusa maana wasafwa wengi walikimbilia milimani ikawa vigumu kuwajua wao ndio wenye mji.

Laiti wasafwa wangebaki kwenye huu mji huenda wangekuwa na maendeleo sana kuzidi hata wanyakyusa, mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini hii bahati wakaichezea na ni ngumu kurudi tena. wasafwa waliletewa hivi vitu vizuri hapa mjini ila wakavikimbia.

-hapa mjini serikali ilijenga shule nyingi ila wasafwa walizikimbia

-ajira nzuri enzi hizo zinahitaji elimu hata za shule ya msingi au form 4 zilikuwepo mjini wao zikawa zinawapita

-mji ulianza kujaa na kukawa na fursa za biashara ambazo wasafwa wangeweza kupata pesa lakini kujitenga kwao kukaliacha soko wazi kwa wageni.

-madaraka, vyeo na teuzi serikalini za kuongoza mji huu wakawaachia wageni ambao nao walitumia bahati hii kuwekana maofisini na kupeana vyeo.

-viwanja vingi waliviacha ama kuviuza na kukimbilia milimani kusiko hata na huduma za jamii, n.k.

-baadhi ya wasafwa waliorudi hapa mjini ama waliobaki maeneo ya karibu wakaanza kujitambulisha ni wanyakyusa kwa kuogopa aibu na wengine kufikia hatua ya kufuta majina ya ukoo ili kuepukana na aibu, hii tabia hadi sasa inaendelea.

Ni historia yenye kusikitisha ila ina funzo kubwa sana, mkataa kwao hugeuka mtumwa.

Mwisho kwa kuhitimisha naweza kutoa ushauri kwa wasafwa kwamba historia haiwezi kubadilika itabaki kwajili ya kujifunza lakini mnachoweza kubadilisha ni muda wa mbele (future) kwa maamuzi mnayoweza kuanza kuyatekeleza sasa ili angalau mrudishe hadhi, mapendekezo yangu kwenu:

- wasafwa mzingatieni sana elimu pambanieni na ikibidi mjinyime watoto wasome.

- mjipanue na kutafuta fursa mpya za kibiashara na kujiajiri, Mbeya ni jiji lina watu wengi wenye mahitaji mengi muangalie ni sehemu zipi mnaweza kuchota pesa.

- muwe na bidii ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na uongozi kwenye huu mji wenu, mpambanie nafasi za kupaza sauti ya kero zetu wageni wa mbeya na zenu wazawa halisi wa mbeya.

-msaidiane na kubebana ili walio chini nao wawe na maendeleo, roho za umimi na ubinafsi haziwezi leta maendeleo.

-mjivunie asili yenu ya usafwa, kuna baadhi ya wasafwa hufuta majina yao ya ukoo na wengine kukana kabila lao, huu ni ujinga, jivunie kabila lako, nyumbani ni nyumbani kwa jirani sio kwako.

bila kufanya haya hakuna kitachobadilika..
 
images (16).jpeg
 
ni kwamba nchi ilipopata uhuru kulikuwa kuna wageni wengi walianza kuja na kuhamia hapa jijini kwenye makao makuu ya mkoa wetu wa Mbeya, wageni hawa kwa kiasi kikubwa walikuwa ni wanyakyusa, shida ikaja kwamba wasafwa wakiona wageni walikuwa hawataki kuchangamana nao walikuwa wanahamisha makazi kwenda sehem ambayo wapo peke yao, wanyakyusa walizidi kujaa hapa mjini na ikawa usumbufu kwa wasafwa kuhama hama ikafikia kipindi wengine wakaanza kukimbilia milimani waishi kivyao vyao.

matokeo yake hapa mjini makabila ya ziada yaliyokuja kama wanyiha, wandali, wakinga, wahehe, wangoni, wabena, n.k. wao wakawa wanajua huu mji ni wa wanyakyusa maana wasafwa wengi walikimbilia milimani ikawa vigumu kuwajua wao ndio wenye mji.

Laiti wasafwa wangebaki kwenye huu mji huenda wangekuwa na maendeleo sana kuzidi hata wanyakyusa, mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini hii bahati wakaichezea na ni ngumu kurudi tena. wasafwa waliletewa hivi vitu vizuri hapa mjini ila wakavikimbia.
Karne hii watu bado wanazungumzia makabila,
 
Sababu kubwa ni kuwa wanyakyusa ni wengi. Na waliwahi kutoka nje ya mbeya.

Hivyo wakati wa kujitambulisha wakawa wanasema wanatokea Mbeya.

Kumbuka wanyakyusa ni wenyeji wa wilaya mbili.. RUNGWE na KYELA. Wasafwa ni wachache kwa ujumla wao. Hata huko milimani unakosema walikimbilia bado ni sehemu ya jiji.

Wakinga wana tabia ya kuitana na kushikana mikono ndugu.. Naona wametawala hiyo mbeya.
 
Sababu kubwa ni kuwa wanyakyusa ni wengi. Na waliwahi kutoka nje ya mbeya
Sababu kuu ni wasafwa kupenda kuishi peke yao, wao ndio walikuwa wenyeji wa jiji la Mneya, walipoona wageni wapya wanaanza kuja hasa wanyaki, wao wakawa wanaenda kuishi sehemu za mbali zisizo na wageni. wanyakyusa ni wazawa wa rungwe na kyela.

hadi leo sijajua hii strategy ya wasafwa walikuwa wanataka kufikia malengo gani, mji wako unaukimbia vipi yani
 
historia ina impact kubwa sana kwenye future, hawa wasafwa ndio ilibidi wawe na title yao ya kuwa wenyeji wa jiji lakini waliwaachia hio title wanyakyusa bure kabisa kwa kuwapisha wageni ili waishi peke yao sehemu za mbali.
Mkuu..... unadhani chambuko la wanyakyusa Ni wapi Kama siyo hapa mbeya
 
Mbeya ni yetu sisi wanyakyusa....
wazawa watabaki kuwa wazawa mkuu, hata hili jina la Mbeya lina asili ya kisafwa, kule mteremko wa mbalizi na mlima wa nyoka, magari yanapopata sana ajali wanaofanya mila ni wasafwa, watu wakizama kule ziwa ngosi ni wasafwa ndio hufanya mila kuwapata, bila mila hamuwezi kuipata hio maiti. wasafwa walichokosea ni kukimbia maeneo wakiona wageni (hadi leo wanataniwa kwa jambo hili)

ila kwa idadi ya wakazi naweza kusema ni wanyakyusa japo nao wana kubarua kizito cha kujikwamua kiuchumi hasa kwenye utafutaji, wanyakyusa wengu ukifatilia wamejazana maeneo yenye maendeleo ya chini ama kawaida kama nzovwe, mamajoni, n.k. zile sehemu zenye maendeleo kama forest, block t, isyesye, n.k wamejazana wakinga pamoja na wageni wengine.

uzuri ni kwamba angalau wanyakyusa shule inawabeba wanapata ajira lakini sikuhizi kuna tatizi kubwa la ajira linalowalazimu vijana wageukie kujitafutia, ubaya ni kwamba kwenye utafutaji wa biashara na kujiajiri wanyakyus hapa wapo nyuma, ukifika sehemu kama mwanjelwa na kabwe maduka mengi yanamilikiwa na wakinga na wageni wengine.
 
wazawa watabaki kuwa wazawa mkuu, kule mteremko wa mbalizi na mlima wa nyoka, magari yanapopata sana ajali wanaofanya mila ni wasafwa, wasafwa walichokosea ni kukimbia maeneo wakiona wageni (huwa nacheka sana hapa)

ila kwa idadi ya wakazi naweza kusema ni wanyakyusa japo nao wamejazana maeneo ya nzovwe, mamajoni, n.k. zile sehemu zenye maendeleo kama forest, block t, isyesye, n.k wamejazana wakinga ambao ndio madoni wa jiji hilo oamoja na wageni wengine,
Nakumbuka ukiwa blot T Kutokea hapo fanya unakwenda shule ya sec ivumweee juu huko mlimani
Wasafwa walikuwa wengi huko milimani.....
Kitu kikubwa wasafwa walichonqcho ni uoga na upole
Hivi kwa sasa kuna Don mbeya msafwa

Ova
 
historia ina impact kubwa sana kwenye future, hawa wasafwa ndio ilibidi wawe na title yao ya kuwa wenyeji wa jiji lakini waliwaachia hio title wanyakyusa bure kabisa kwa kuwapisha wageni ili waishi peke yao sehemu za mbali.
Elimu pia iliwapitia kushoto

Ova
 
Nakumbuka ukiwa blot T Kutokea hapo fanya unakwenda shule ya sec ivumweee juu huko mlimani
Wasafwa walikuwa wengi huko milimani.....
Kitu kikubwa wasafwa walichonqcho ni uoga na upole
Hivi kwa sasa kuna Don mbeya msafwa

Ova
Kwa sasa jiji limepanuka sana limefikia mpaka sehemu walizohamiaga hapo zamani imesaidia nao wawe wanachangamana na wageni, wengine nao wameamua kurudi mjini kutoka huko milimani, mambo ya kukaa peke yao nadhani yaliwagharimu sana hivyo wameamua wajichanganye tu.

kuhusu uoga sidhani ila labda ni ile tabia yao ya kuhama kwenda kuishi kivyao ndio ilileta fikra hii, kwa upole naweza kubaliana na wewe huwaga hawana mambo ya vurugu.

Don wa kisafwa kwa hapa Mbeya sijamjua, kwa wanyakyusa wenye mendeleo angalau wapo wapo hasa walioajiriwa ila sijaona wa kufikia anga za madoni, Madoni wengi wa hapa Mbeya kwa sasa ni wakinga na wageni wengine wanaomiliki maduka makubwa, mahoteli, makampuni, viwanda, n. k
 
Kwa sasa jiji limepanuka sana limefikia mpaka sehemu walizohamiaga hapo zamani imesaidia nao wawe wanachangamana na wageni, wengine nao wameamua kurudi mjini kutoka huko milimani, mambo ya kukaa peke yao nadhani yaliwagharimu sana hivyo wameamua wajichanganye tu.

kuhusu uoga sidhani ila labda ni ile tabia yao ya kuhama kwenda kuishi kivyao ndio ilileta fikra hii, kwa upole naweza kubaliana na wewe huwaga hawana mambo ya vurugu.

Don wa kisafwa kwa hapa Mbeya sijamjua, hata wanyakyusa wapo wenye maendeleo hasa walioajiriwa ila kufikia levo za madon hapo sijaona, Madoni wengi wa hapa Mbeya kwa sasa ni wakinga na wageni wengine wanaomiliki maduka makubwa, mahoteli, makampuni, viwanda, n. k
Inasemekana mwenye Hotel ya silver stone tunduma ni mswafwa

Kuhusu madon mbeya toka kitambo ni wakinga hata hapo block t walijaa sana

Hivi eland Hotel bado ipo hapo block t

Ova
 
Sababu kubwa ni kuwa wanyakyusa ni wengi. Na waliwahi kutoka nje ya mbeya. Hivyo wakati wa kujitambulisha wakawa wanasema wanatokea Mbeya. Kumbuka wanyakyusa ni wenyeji wa wilaya mbili.. RUNGWE na KYELA.. wasafwa ni wachache kwa ujumla wao.. Hata huko milimani unakosema walikimbilia bado ni sehemu ya jiji. Wakinga wana tabia ya kuitana na kushikana mikono ndugu.. Naona wametawala hiyo mbeya.
wazawa watabaki kuwa wazawa mkuu, kule mteremko wa mbalizi na mlima wa nyoka, magari yanapopata sana ajali wanaofanya mila ni wasafwa, wasafwa walichokosea ni kukimbia maeneo wakiona wageni (hadi leo wanataniwa kwa jambo hili) ila kwa idadi ya wakazi naweza kusema ni wanyakyusa japo nao wana kubarua kizito cha kujikwamua kiuchumi hasa kwenye utafutaji, wanyakyusa wengu ukifatilia wamejazana maeneo yenye maendeleo ya chini ama kawaida kama nzovwe, mamajoni, n.k. zile sehemu zenye maendeleo kama forest, block t, isyesye, n.k wamejazana wakinga pamoja na wageni wengine. uzuri ni kwamba angalau wanyakyusa shule inawabeba wanapata ajira lakini sikuhizi kuna tatizi kubwa la ajira linalowalazimu vijana wageukie kujitafutia, ubaya ni kwamba kwenye utafutaji wa biashara na kujiajiri wanyakyus hapa wapo nyuma, ukifika sehemu kama mwanjelwa na kabwe maduka mengi yanamilikiwa na wakinga au wageni wa makabila ya kigeni,,, wanyakyusa wengi utawakuta nyuma ya soko wanauza maparachichi na baadhi mitumba.

Kusema wanyakyusa ndiyo wengi umetumia kigezo gani?🤔
 
Back
Top Bottom