Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,641
- 46,283
Sababu mojawapo tasnia ya bongo movie imekuwa dumavu, mbovu na isiyofanya vizuri kwa muda wote tangu nchi ipate uhuru inaweza kuwa ni kutokana na kutawaliwa na watu/waigizaji wa pwani na kusini zaidi. Upande wa maudhui na mazingira ni hivyo hivyo pia, ni ya kipwani, Kusini na Uswahili zaidi.
Kinachotakiwa sasa ni wadau wafanye jitihada binafsi kuifanya sekta hiyo kuwa jumuishi zaidi na yenye uwakilishi mpana kwa kuhakikisha watu wa jamii nyingi tofauti zaidi kama Wahaya, Wasukuma, Wakuria, Wambulu, Wamasai, Wanyakyusa, Wasafwa, Wakinga n.k wanashiriki katika kuigiza bongo movie ili kutanua wigo wake, kuvutia watu wengi zaidi na kuongeza ubunifu na tija.
Pia wajaribu kufanyia kazi zao katika mazingira tofauti na ya Dar au pwani. Nchi kubwa kama hii ni ujuha kazi zote za bongo movie kuigizia mazingira ya ki'Dar es Salaam na Kipwani tu. Igizieni hata huko Katavi, Mbeya, Arusha, Kigoma, Mbeya, Mara, Mwanza.