Historia Fupi ya Abu Amina Philips

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,233
8,780
Alizaliwa nchini Jamaica na alisomea nchini Canada, alipata shahada ya kwanza katika biochemistry.

Kwa kuwa anatoka katika familia ya Kikristu, maisha yake ya awali aliishi kama Mkristu.

Wakati akiendelea na masomo yake nchini Canada, alitokea kuvutiwa na itikadi ya Kikomunist. Ni katika kipindi hicho hicho alishuhudia mivutano na mapambano katika mabweni ya Wanafunzi wa kiamerika. Mivutano hiyo ilitokana na ubaguzi wa rangi, Wamarekani weupe wakiwabagua weusi.

"Nilikerwa na maisha haya, niliamua kwenda China kuona maisha ya Kikomunist, nilivutiwa na baadhi ya mambo katika itikadi hiyo". Kwa hiyo niliamua kuingia kwenye ukomunist nikiwa na tamaa kwamba huenda huko kuna mgawanyo sawia wa kiuchumi, anasema Abu Ameena alipokuwa akihojiwa na gazeti la Islamic Voice hivi karibuni mjini Bangalore nchini India.

Aliporejea nchini Canada akitokea China Abu Ameena anasema moja kwa moja alijiunga na chama cha Kikomunist. Hata hivyo hakuridhishwa na undani wa ukomunist.

"Maisha ya viongozi wa Itikadi hiyo hayana nidhamu. Nilisita kujitoa katika chama hicho kwa sababu kulikuwa na matarajio kwamba baada ya mapinduzi mambo huenda yakawa sawa":, anasema Dr. Abu Ameena na kuongeza kuwa alitaka kurejea nchini China kuchukua mfaunzo ya vita vya msituni. Hata hivyo Wachina hawakuwa tayari kumpokea.

"Hili liliniongezea chuki kwa ukomunist, nikajitoa."

Kusilimu

Baada ya kujitoa kwenye ukomunist, Dr. Phillips alibakiwa na hangaiko la moyo huku akichukizwa na dhulma iliyoshamiri. Aliuona ukomunist kama ni mbinu ya wajanja wachache wanaoziteka nyara akili za watu ili wawatumie kufikia malengo yao.

Wajanja hao wanaojifaragua kutaka kuweka mfumo "sawia" huku wakificha makucha ya tamaa na ulafi wao, hawakuweza kukidhi haja ya Dr. Abu Ameena. Baada ya kugundua siri hiyo Dr. Phillips anasema:

"Miongoni mwa wanafunzi waliokuwa katika kundi letu, ni madada wawili ambao walishasilimu wakati huo. Kaka zao halikadhalika walisilimu kitambo. Nilisoma kitabu cha Elijah Muhammad juu ya uislamu, hakikunivutia kwa sababu kilikuwa kimejaa chuki dhidi ya watu weupe. Sikuwa tayari kuwaitakidi watu weupe kwamba ni mashetani. Huu haukuwa Uislamu sahihi.

Kitabu ambacho kilikuwa na athari kubwa kwangu kilikuwa, Islam:The Misunderstood religion" kilichoandikwa na Muhammad Qutb. Hiki kilinifahamisha kwamba Uislamu ni mkamilifu, kwa kweli kilivuta mno akili zangu."

Kitabu chengine ni "Towards Understanding Islam" kilichoandikwa na Maulana Abul Ala Maududi ambacho kilinipa mtazamo mpana na mwelekeo sahihi wa Uislamu.

Vile vile nilisoma vitabu vya historia na nikafahamu nafasi ya Uislamu katika kuyakomboa mataifa ya Kiafrika kutoka ukoloni wa nchi za Ulaya. Nilikuja kufahamu kumbe Uislamu haumfundishi mtu kumgeuzia shavu la pili yule ampigaye shavu moja. Kuanzia hapo nikasimama imara kuutetea uislamu. Haukupita muda mrefu huo hatimaye nilisilimu mwaka 1972.

abu-ameena-bilal-philips-L-zYfeVj.jpeg
 
Endelea Mkuu, mbona unawanyima wengine utamu. Ingia katika hii web. alhidaaya.com.

Au web ya alislaam.com. Utampata mwengine anaitwa Dr. YUSSUF ESTES akielezea jinsi alivyoingia katika Uislam, kutoka katika Upadre.
 
Mbio zooote kumbe Ni kujifunza Vita vya msituni tu. Na wachina waligundua lengo lako so ukomunist Bali Ni kujifunza Vita vya msituni ndio maana walikukataa. Na ndio maana mpaka Sasa wachina na uislam Ni mbingu na ardhi.
 
Mbio zooote kumbe Ni kujifunza Vita vya msituni tu. Na wachina waligundua lengo lako so ukomunist Bali Ni kujifunza Vita vya msituni ndio maana walikukataa. Na ndio maana mpaka Sasa wachina na uislam Ni mbingu na ardhi.
Mbingu na ardhi kivipi??msikiti wa Shanghai huu


images.jpeg
 
Back
Top Bottom