Hillary Clinton aiumbua Tanzania

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,320
Pamoja na kupigia debe ziara yake alipokuwa hapa mama huyu, na kuwa ameamua kufuta umasikini, Bi Clinton aweka wazi kutokuridhika na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa na Tanzania.

Akitoa majumuisho juu ya ziara yake katika nchi kadhaa za Africa, Hillary alitumia muda mwingi kuisifia na kuipongeza Rwanda, kwa hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa, hatua ambazo zimeipeleka nchi hiyo kuelekea kujiondoa katika nchi masikini. Alizitaja nchi nyingine zilizopiga hatua kimaendeleo kuwa ni Zambia, Mali na Ghana. Hakuitaja kabisa Tanzania katika nchi zilizoonyesha juhudi za kupiga hatua kimaendeleo

Source; ITV
 
Ndo viongozi wetu wajue kuwa maendeleo siyo kulundikana mjini na kusababisha vurugu kila sehemu, foleni barabarani, miundo-mbinu isiyokuwa na ubora wowote. Kazi kubwa ya viongozi wetu kila mwaka ni kuweka mipango, mipango, mipango bila kujua kuna gharama yake kutekeleza hiyo mipango ambayo ni pamoja ni rasilimali watu, kupunguza matumizi ya anasa, kujifunga mikanda huku ukitarajia mambo mazuri ikiwezekana hata kuwafanya watu wapige kazi bila malipo ya ziada, watu wako tayari kufanya kazi ni motisha tu kutoka kwa viongozi wetu ndo inawafanya waache uzalendo.

Lakini viongozi wetu wanataka vyote matokeo yake wanasahau mipango au kwa makusudi kabisa wanatuhadaa.
 
Viongozi na Chama kinachoiongoza nchi ccm hawawezi kutufikisha Watanzania kule tunataka ni ngumu sana
 
Kwa hiyo Chadema-JF, mmejifariji kwa kutoitaja Tanzania?
 
Inabidi Tanzania iige mfumo kama wa Rwanda, wao huwa na mfuo wa kumtathmin kiongozi ikiwa ni mbunge aliadi kuleta maendeleo jimboni kwake huwa wanampa mwaka kwa mwaka malengo uliojiwekea ss kila baada ya mwaka kuisha kuna kipindi cha live kwenye TV yao ya Taifa unaendda pale unajielezea wee ukimaliza wananchi wa jimbo lako wanapiga simu kutoa maoni ama malalamiko huku Mh. Kagame nae akiangalia baada ya hapo Mh. Kagame yy anatoa maoni yake ikiwa utakuwa uko chini ya kiwango ambacho ulitakiwa kufikia ujue kazi huna eitha ujiuzulu mwenyewe ama ufukuzwe kazi na ndio maana wenzetu wamepiga hatua kwenye masuala ya maendeleo.

Kuna mawaziri wawili waliofungwa jela kwa sababu ya rushwa
 
Kwani Bi.Hillary Clinton alivyokuja Tanzania si nasikia alienda Kinondoni manyanya mtaa wa ufipa makao makuu ya Chadema, kuonana na a loser Dk W. W Slaa
 
sure for the USA through AGOA the door is open to any country ..but she put up more response into countries which they showed constructive straitegies and measures to overcome development. I'm sure leo hii tupewe the same fund zaidi,..ya Rwanda or any else..we should stil do nothing..!kwani iye fedha in be corrupted hata kabla haija be matured..!..a.k.a washaichukua kupitia so clled sitting allowance..!cha ajabu sioni wanachofaidi..tunapokaa kwenye follen eti kwa sababu barabara iliyetakiwa imekwishajengwa within a deadline...imetelekezwa kisa waziri or mkurugenzi ana 20% thereafter hakuna atayemuliza mkandarasi na hapo watafukiafukia imeshatoka.....ivi

Wanajamii tujiulize.... ni kweli wote au wengi wetu hatujui nini suluhu yake nini?

Ivi ni kweli wote au wengi wetu hatukuipigia kura ccm tuliipigia chadema...au chama kilichoonyesha nia ya kupewa dhamana?

Hii aina ya kuongoza nchi kupitia kugawa makundi na kuwalinda eti hawa...kundi la epa...wale la dowans ..kule wa rada..ninawaangalia tu na kukaa na kuwasubiri watulete maendeleo wakati huo utata wao utakapokishwa ili twafamu hauwezi kwisha..?even after a centuary i'm sure never to be solved..!

kwa hesabu ya haraka na nyepesi ccm na maendeleo tuwe wakweli hatutoki..!..kwa sababu wao siku zote wanadaiwa kwa kudaiana so kila wakati wanatafuta kwanza jinsi ya kutulizana the ndiyo watuongozee nchi?...when?..Zitto big up?keep it up!
 
Kwani Bi.Hillary Clinton alivyokuja Tanzania si nasikia alienda Kinondoni manyanya mtaa wa ufipa makao makuu ya Chadema, kuonana na a loser Dk W. W Slaa
Kwa mibwege kama wewe kutakuwa na maendeleo kweli,swala la maendeleo ya nchi yetu sio la chadema na Dr slaa,ni la kwetu wote regardlss of itikadi za chama chako,kwa bahati mbaya au nzuri chama kilicho madarakani ni CCM,so ni lazima tukikosoe ili kiweze kuleta maendeleo kwa manufaa yetu sote,sio unakaa kumbeza Dr slaa.
 
sure for the USA through AGOA the door is open to any country ..but she put up more response into countries which they showed constructive straitegies and measures to overcome development. I'm sure leo hii tupewe the same fund zaidi,..ya Rwanda or any else..we should stil do nothing..!kwani iye fedha in be corrupted hata kabla haija be matured..!..a.k.a washaichukua kupitia so clled sitting allowance..!cha ajabu sioni wanachofaidi..tunapokaa kwenye follen eti kwa sababu barabara iliyetakiwa imekwishajengwa within a deadline...imetelekezwa kisa waziri or mkurugenzi ana 20% thereafter hakuna atayemuliza mkandarasi na hapo watafukiafukia imeshatoka.....ivi

Wanajamii tujiulize.... ni kweli wote au wengi wetu hatujui nini suluhu yake nini?

Ivi ni kweli wote au wengi wetu hatukuipigia kura ccm tuliipigia chadema...au chama kilichoonyesha nia ya kupewa dhamana?

Hii aina ya kuongoza nchi kupitia kugawa makundi na kuwalinda eti hawa...kundi la epa...wale la dowans ..kule wa rada..ninawaangalia tu na kukaa na kuwasubiri watulete maendeleo wakati huo utata wao utakapokishwa ili twafamu hauwezi kwisha..?even after a centuary i'm sure never to be solved..!

kwa hesabu ya haraka na nyepesi ccm na maendeleo tuwe wakweli hatutoki..!..kwa sababu wao siku zote wanadaiwa kwa kudaiana so kila wakati wanatafuta kwanza jinsi ya kutulizana the ndiyo watuongozee nchi?...when?..Zitto big up?keep it up!
Acha uongo, kwenye red
1. Rwanda ni sawa na mkoa wa kigoma tu, kwa hiyo hawawezi
2. Ni kweli chedema walishinda huko karatu, moshi na Arusha kwa urais lakini si tanzania yote. Jakaya won election tuache uongo na ubabaishaji. bila shaka wewe utakuwa mtu wa kaskazini kwa Tz yetu. Nakushauri tembea Tanzania. ni zaidi ya kapo kaskazini ulipo. kuna kusini, magharibi, mashariki na kati pia.
Anyway kama hutaki leave me alone na nenda kapalilie ndizi na kapige dawa mikahawa.
 
Nimesikia minister for foreign affairs yuko tena uswiss,juzi sijuhi alikuwa wapi na nasikia amealikwa sudani keshokutwa...sasa kama rais anahodhi mamlaka zote na kuwa kiguu na njia ni vipi Tanzania itaendelea jamani...Tanzania haina rais bali tuna msafiri kama akina Columbus na Vasco the da Gama
 
Pamoja na kupigia debe ziara yake alipokuwa hapa mama huyu, na kuwa ameamua kufuta umasikini, Bi Clinton aweka wazi kutokuridhika na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa na Tanzania.

Akitoa majumuisho juu ya ziara yake katika nchi kadhaa za Africa, Hillary alitumia muda mwingi kuisifia na kuipongeza Rwanda, kwa hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa, hatua ambazo zimeipeleka nchi hiyo kuelekea kujiondoa katika nchi masikini. Alizitaja nchi nyingine zilizopiga hatua kimaendeleo kuwa ni Zambia, Mali na Ghana. Hakuitaja kabisa Tanzania katika nchi zilizoonyesha juhudi za kupiga hatua kimaendeleo

Source; ITV

Makada wa CCM hawapendoi kabisa kusikia hili wao wanapenda kusifiwa hata kama ni uongo nae anajua kabisa ni uongo lakini wakisifiwa wapo radhi wampe mwaliko tena kwa gharama zao wenyewe angalau waandae kamkutano flani iwe Arusha au Dar
 
Sijawahi kuona hata siku moja ume post point humu. ni upupu from A-Z. Unajitafutia umaarufu wa kijinga.
Mkuu, point kwako mpaka tumsifie Dk Slaa? Halafu nitafute umaarufu wa nini wakati wote humu JF, tupo undercover
 
Back
Top Bottom