Hili tunda kwa lugha ya kwenu mnaliitaje?

Last edited by a moderator:
Naona wote wanakujibu kwa kiswahili...sijui ni wote hawana lugha za kikwao (kikabila)? au ndo lengo lako mkuu kupata jina la kiswahili? anywayz kikwetu linaitwa ekimansimansi

Mkuu wewe ndio hujaelewa anachokitaka, amesema kwa lugha ya kwenu, siyo kabila la kwenu, lugha ni kama kiswahili, kichina nk ila kabila ndio kibena, kigogo nk
 
Mkuu wewe ndio hujaelewa anachokitaka, amesema kwa lugha ya kwenu, siyo kabila la kwenu, lugha ni kama kiswahili, kichina nk ila kabila ndio kibena, kigogo nk
Yaani wewe ndio unajichanganya kabisaaaa!
lugha ni kama kiswahili, kichina nk ila kabila ndio kibena, kigogo nk
Kwahiyo unataka kutuambia kuwa hicho Kibena / Kigogo hakina / siyo lugha?! ... vipi Mkuu ndidudila


Kwa mujibu wa KAMUSI ya kiswahili : Lugha nm [i-/zi-] language; speech

Maana ya neno "lugha"

Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zilizokua katika mpango maalum na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.


Mara chache neno lugha linatumika kwa taratibu za kuwasiliana za wanyama. Lakini taratibu hizo ni tofauti sana: Katika lugha za wanyama, sauti moja ina maana moja tu. Lakini katika lugha za binadamu, sauti nyingi zinaunganishwa kutengeneza maneno, na maneno mengi yanaunganishwa kutengeneza sentensi. Hivyo mnyama ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini tofauti anaweza "kusema" mambo ishirini tu. Kwa upande mwingine mtu ambaye anaweza kutengeneza sauti ishirini, anaweza kusema mambo zaidi ya millioni.

Tabia za lugha

  • Lugha huzaliwa
  • Lugha hukua = (kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa).
  • Lugha hurithiwa
  • Lugha huathiriana
  • Lugha lazima ijitosheleze
  • Lugha hufa

Sifa za lugha


  • Lugha lazima iwe inahusu binadamu
  • Sauti-sauti hufanywa na mwanadamu
  • Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, c, h, d, z
  • Lugha huwa na mpangilio maalumu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu ---> Silabi ---> Neno
  • Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi.

Dhima za lugha


  • Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari.
  • Lugha hutumika kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii.
  • Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii.
  • Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia).
  • Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila/jamii au taifa fulani.

Aina za lugha

Kimsingi lugha ni moja. Uwasilishwaji wake ndiyo huigawa katika tanzu/aina kuu mbili:

  • Lugha ya mazungumzo
  • Lugha ya maandishi

Lugha ya mazungumzo

Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya mazungumzo ya mdomo - na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mazungumzo. Lugha ya mazungumzo ni kongwe, hai na halisi zaidi ya mzungumzaji na ina maana nyingi kwani mzungumzaji na msikilizaji ua ana kwa ana katika mazingira mamoja.
 
Sawa sawa na Kiswahili. Unajuwa neno shawishi lina msingi wa Kiarabu?
Kuna maneno karibu ya 4,000 ambayo Kiswahili imekopa kutoka Kiarabu.

NA si Kiarabu tu ... hata Kiportuguese tumekopa

Dancador - DANGURO - Brothren
Vinyo - MVINYO - Wine
Carta - KARATA - Cards
Copas - KOPA - Heart
Pao - PAU - Club
Sete - SETI - Seven
Trunfo - TURUFU - Trump
Mandioca - MUHOGO - Cassava
Tabaquerra - TUMBAKU - Tobacco
Bibo - BIBO - Cashew
Pera - PERA - Guava
Bandeira - BENDARA - Flag
Bomba - BOMBA - Pump
Boia - BOYA - Buoy
Buli - BULI - Teapot
Foronha - FORONYA - Pillow case
Caixa - KASHA - Box
Copo - KOPO - Pot
Caraco - KOROSHO - Cashew nut
Lenco - LESO - Scarf
Mesa - MEZA - Table
Padre - PADRI - Priest
Peca - PESA - Coin
Roda - RODA - Pulley
Sapata - SAPATU - Slipper
Sombreiro - SHUMBURERE - Hat
Trombeta - TARUMBETA - Trumpet

Anyway angalia haya baadhi ya Kiarabu

 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom