Hili ni tatizo gani?

Ihayabuyaga

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
413
479
Habari wana JF Afya.

Nina watoto 3 wa kiume (5, 3, 1.5 years). Ilianza kwa mkubwa kokwa moja ya korodani upande wa kushoto IKAPANDA juu mpaka sasa imepotea haionekani. Alipopelekwa hospitali daktari akasema kwamba labda ni uumbaji wa Mungu.

Wa pili naye kokwa ya upande wa kulia imeanza kuvimba na kupanda juu.

Wa tatu kokwa moja ya upande wa kulia nayo imeanza kuvimba na kupanda juu.

Swali: je hili ni tatizo gani?
Je athari zake ni nini kama kokwa zikipotelea huko zinakokwenda?
Je kuna suluhisho?

Aksante
 
Suala la kokwa kupotea laweza kuhuaishwa na hernia/tundu kwenye eneo ambalo zilipita wakati zinashuka kwenye kirodani.

Kokwa kawaida hutengenezwa tumboni na kabla ya mtoto kuzaliwa hushuka.

Inapotokea zimepote ni muhimu kufanya hata altrasound na kuona zilipo.

Baridi ni moja ya kitu kinachofanya kokwa kuusogela mwili na kama kuna tundu, basi kokwa huweza kupitiliza na kurudi ndani.

Si vyema kokwa kukaa ndani ya mwili, kwani zikikaa tumboni kwa muda mrefu, joto huweza kuharibu afya ya kokwa husika.

NB: Watoto wafikishwe kwa daktari hasa wa watoto au mwenye uzoefu ili kutizamwa vyema na kuwapa ushauri sitahiki.
 
Habari wana JF Afya.

Nina watoto 3 wa kiume (5, 3, 1.5 years). Ilianza kwa mkubwa kokwa moja ya korodani upande wa kushoto IKAPANDA juu mpaka sasa imepotea haionekani. Alipopelekwa hospitali daktari akasema kwamba labda ni uumbaji wa Mungu.

Wa pili naye kokwa ya upande wa kulia imeanza kuvimba na kupanda juu.

Wa tatu kokwa moja ya upande wa kulia nayo imeanza kuvimba na kupanda juu.

Swali: je hili ni tatizo gani?
Je athari zake ni nini kama kokwa zikipotelea huko zinakokwenda?
Je kuna suluhisho?

Aksante
Madakitar wa siku iz wamchongo sana hata kukwambia itakuwa ni hernia ameshindwa
 
Back
Top Bottom