Hili la Ukosefu wa Ajira tatizo lilianzia hapa kwenye D2, wazazi tuwaambie vijana ukweli, vyuo vya ovyo ovyo elimu ovyo!

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
4,722
14,253
Ndugu wazazi wenzangu wasalamu,

Kuna jambo nataka niwaeleze, na hii ni pamoja na vijana wenzangu, wanaopata maisha ya tabu kwenda kusoma miaka zaid ya 18 kutegemea ndoto ambazo hazitimii.

Nitaeleza kidogo:
Hapo zamani kidogo, chini ya miaka ya 2000s ilikuwa ni lazima mtoto afaulu Darasa la nne ndio aendelee na masomo ya Darasa la 5 hadi la saba, kuanzia miaka ya 2000 hivi, hali ikabadilika, wakasema wote waendelee, watu kimya...

Hadi kufikia mwaka 2002, kwa "waliobahatika" kuendelea na secondari FORM 11 ilikuwa lazima upate wastani wa ngalao alama 30, nao ukafutwa, awali ilikuwa 21, yani angalao D flat,

Kuendelea secondary, yani form 3 had 4, ilikuwa ni kaz sana kupata Div 1, ili ufaulu kias hicho lazima uwe mtu smart sana yani sana, yani sana, saivi yani Single Digits kawaida sana.

Kipindi hicho Kupata Div ONE au TWO, lazima uwe umepata D hesabu, otherwise huwezi pata DIV 1 ukiwa na F ya hesabu, kwa sasa hivi mambo ni tofauti kabisa, hata uwe na F ngap wewe ni Kijiti tu
Hiyo haikuishia hapo, ikaja kwenda Chuo, kuna wanasiasa wanataka vyuo vikuu viwe kila wanapotoka

Kuna chuo kikuu kinajenga matawi kila mkoa na wilaya
Kuna chuo kikuu kina tawi Kizumbi, Simiyu, Msata, Dodoma, na maeneo mengine mengi tu kutaja machache,

Coz zinazofundishwa huko ni zile zile, Laws, Accounting, BAs, Education, Business Admins, Compyuta etc.

Kuna wimbi la vyuo vya elimu ya afya ya D2, yani ukiwa na D2 za biology na Chemistry , una chance ya kuwa mfamasia au Daktari....

Ili kusoma chuo kikuu zamani, kupata coz ilibidi ufaulu wa hali ya juu sana, kuna kipindi UDSM ilikuwa kupata Laws lazima upate Div 1 ya 3 au 4 mwisho, sikuizi hata E 2 NA D1 Unasoma Laws,

Zamani bila form 6 au Cheti kisafi cha Dip huwez kwenda Chuo kikuu, sikuizi ni D4 TU, zinatosha.

Turudi kwenye vyuo vyenyewe,

Zamani ilikuwa ukifaulu kwa daraja zuri la 2, au tatu unapangiwa vyuo, kama chuo cha maji, Arusha Tech, Dip ya Afya nk.

Sasa hivi ni mwendo wa D4 tu, na wengine wameacha kutoa elimu ya ufundi wanatoa Degree.. yani ni mwendo wa kufyatua tu Bachela.

Coz kama IT, Computer Science and Engeneering, Forests, ects lazima uwe mwanafunzi mwenye mchepuo wa sayansi, na shule nyingi zilikuwa na maabara , sasa hivi mtu ana A ya chemistry hajawahi ona Spatula kwa macho, au hajawahi hata kufanya titration.


Chanzo ilikuwa ni moja,

Wanasiasa wengi waliona fahari kusifia ufaulu bila kujua madhara yake kwa taifa, jiulize kila mwaka ufaulu unaongezeka?? how is that?

Wanasiasa wengi wakaanza kujinasibisha na degree za uwongo nk..( ref Msemakweli)
Wengine na ma PHD ya kubumba hadi kwa viongozi wa dini... hadi wafanyabiashara,... jina DOKTA likabamba sana....

Matokeo yake;

AJIRA AJIRA AJIRA AJIRA>>>>>>>>>AJIRA 8000, mara Mil 8, Mara elf 5 Mara elfu Moja,

Utaajiri wote kwenye serikali ipi?

Nani afanye kazi zinazohitaji skills za kati kama ufundi.

Waliodhani wanasaidia wananchi wakawapoteza moja kwa moja, ikawa sasa shida imekuja kukaa kwa wazazi na vijana wao...tip LOAN BOARD... unasoma degree yako huko ya nini sijui, unawekewa deni MIl 28, hakuna kazi na deni linaongezeka kila siku, na huko tunakoenda lazima watapita na huko bank kujaribu ku recover bad loans.. ni suala la muda tu.


Wazazi hawataki kuelezewa ukweli au vijana wanapenda kujionesha wapo chuo kikuu hata kama ni kupoteza muda...

Fundi AC huwez muona hana kazi
Fundu bomba kila siku kazi
FUndi mchundo kazi za kutosha
Fundi Cherehani kila siku kazi
Fundi rangi kazi za kutosha
Fundi mechanics kazi za kumwaga.. nk nk..

FUNDI DEGREE AMELALA ANASUBIRIA MCHONGO NA KUPERUZI STATUS ZA WHATSUP NA INSTAGRAM. Twende kazi

Wengine wamekalia kusubiria kazi vyuoni, yani degree after degree.. hadi PHD with '0' experience...

Mwisho wa siku serikali inazidiwa na tatizo iliyotengeneza yenyewe........ degree na elimu zenye ufaulu unaoongezeka kila Mwaka....

To you Hon. Ndungai, you cant make real hustlers with this kind of generation come what may.

Sasa hivi mmekuja na mjadala wa kufuta kiingereza kimya kimya, mmeanza na Mahakamani ambapo ndio sehem lugha ya kingereza inatumiwa zaidi, tunawaangalia tu... tatizo liongezeke tuone nini kitatokea.

Disclaimer;
I'm not trying to control the state house neither Ministry of Education, just my few cents on the drama.
 
Bora tuliosoma zaman pamoja na kwamba hatuna kazi lkn tumepata kazi ya kufanya kwa kazi na kubinu mbunu ya kujiishi, me nimeamua sitapelekea mtoto shule nitaungana na ile familia ya kilokole ilokataa kusomesha watoto kwa7 duniani tunapita!

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mtoa Uzi hongera Sana!
Kilichokosekana kwako Ni Takwimu tu kuhusu idadi ya watu wenye shahada inazidi kwa kiasi gani ajira zilizopo serikalini basi.

Lakini nijuavyo Mimi unemployment rate ya Tz inacheza kwenye 2%. Naomba mchumi aje kutusaidia ufafanuzi wa hiyo unemployment rate.
 
Waliopo makazini wanataka kufia kwenye hizo ajira, hawataki kuachia nafasi wengine nao watafute mtaji wa kujiajiri. Mtu ana miaka zaidi ya 20 kazini lkn hata hafikirii kutengeneza ajira, tunategemea wasio na vyeti ndo watengeneze ajira.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Waliopo makazini wanataka kufia kwenye hizo ajira, hawataki kuachia nafasi wengine nao watafute mtaji wa kujiajiri. Mtu ana miaka zaidi ya 20 kazini lkn hata hafikirii kutengeneza ajira, tunategemea wasio na vyeti ndo watengeneze ajira.

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Off point! Hoja hapa ni elimu duni ambayo vyuo vyetu vinatoa hivi sasa. Kwa sababu za kuifanya elimu kuwa biashara vyuo vinadahili wanafunzi wasio na uwezo ilimradi vipate ada yao.

Kuhusu muda wa kiajiriwa na kutengeneza ajira ni hiari ya mtu. Kama mtu anaona kiajiriwa kunalipa zaidi kwa nini ajihangaishe kutengeneza ajira? Isitoshe waajiri wengi wanapenda watu wenye uzoefu ili kupata matokeo bora zaidi kuliko kuajiri mtu asiyejua kitu na kusababisha hasara. Hii si kwa Tanzania tu bali hata kimataifa na ndiyo sababu WTO imeajiri mwanamama kutoka Nigeria wa zaidi ya miaka 65 kuwa mkurugenzi wake mkuu.
 
Sasa hivi mmekuja na mjadala wa kufuta kiingereza kimya kimya, mmeanza na Mahakamani ambapo ndio sehem lugha ya kingereza inatumiwa zaidi, tunawaangalia tu... tatizo liongezeke tuone nini kitatokea......

Andiko zuri sana hili..... kuhusu kiswahili... sasa hv VETA wameshaanza kufundisha kwa Kiswahili...
 
Back
Top Bottom