Hili jambo limeniumiza sana

Manun'guniko

Senior Member
Jul 23, 2014
155
59
Habari zenu jamani

Katika familia yangu tumezaliwa wawili Mimi nikiwa ndiye mtoto wa kwanza alafu akafwata midogo wangu ambaye tayari ni marehemu mwezi sasa umepita.....nimebaki Mimi na mama yangu baba alishafariki miaka imepita.

Kabla ya mdogo wangu kufariki alikuwa ni kipenzi cha mama sana hilo halikuwa linanisumbua niliona kawaida sana pia hiyo ilitokana na mahusiano ya mpenzi niliekuwa nae mama hakumpenda sana jambo hilo lilifanya Mimi na mama yangu tusiwe na maelewano.
Kitu kilichokuja kuniumiza na nimuone mama tofauti ni siku mdogo wangu alipofariki mama alikuwa akilia wa nguvu na huku akilitaja jina la mdogo wangu na Mimi.......nanukuu( BORA USINGEONDOKA WW KIPENZI CHANGU ANGEONDOKA DADA YAKO (yani mimi)INGEKUWA AFADHARI.
Maneno hayo halikuwa akiyarudia kuanzia mwanzo wa msiba mpaka anazikwa jambo hili liliwashangaza wengi na liliniumiza sana mpaka Leo nikikumbuka Yale roho inaniuma sana nashindwa hata kumuangalia mama yangu naishia kulia.
Pengine nimemkosea mama yangu sana lkn sikutegemea kama anaweza kuombea Mimi kufa imeniumiza sana.
Amekuja leo na baadh ya ndugu akiomba msamaha sijasema chochote nimeishia kulia.nataman niende mbali kwasababu nimejua Mimi si chochote kwake.

Mwenye ushauri au mawazo yoyote kisaikolojia siko sawa.
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga walisema: mpe mchawi akulelee mwanao...

Joseverest samahani kwa kuchukua kiti chako.
 
Pole sana mkuu..jitahidi kuifuta hiyo kumbukumbu kichwani (japo ni ngumu; angalau kidogokidogo) na umsamehe Mama yako...

Pia jaribu kutafuta mtaalam wa Saikolojia akusaidie
 
Mama si mungu na hawezi kuwa mungu wala mzazi yeyote hawezi pata nafasi ya umungu kwa namna yoyote
hekima ya mungu haipimiki hata kidogo na mungu hawezi fanya makosa ya dhihaka namna hiyo, mungu hafikiriki
mama yako ana makosa sana na imeniuma kwa kweli
 
Huyo mama ni katili kama mchawi hastahili kufananishwa na Mungu wake duniani hastahili hiyo heshima kuu.
 
Mama ni Mungu wa Pili katika dunia hii. Hakuna kitu kibaya kama kumchukia Mama. Unachopaswa kufahamu kuwa hakuna mwanadanu aliyekamilika. Hivyo uambie moyo wako kuwa huyu ni mama yangu na vyovyote itakavyokuwa atabaki kuwa mama yangu. The rest mwachie Mungu. Hata kama utaamua kumchukia haitasaidia. Nakusihi mlipe kwa wema hadi ajue kama wewe unampenda hata kama yeye hakupendi. Ukifanya hivyo Mungu ipo siku atakufanyia wepesi katika mambo yako na familia yako kwa ujumla.

Wahenga wakisema: mpe mchawi akulelee mwanao...

mtanzania halisi, wanafiki sana watanzania
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom