Hii Yanga ya Gamondi ndio timu bora zaidi kuwahi kutokea hapa nchini

babu onyango

JF-Expert Member
Jan 12, 2023
334
813
Yanga na Simba kwa nyakati tofauti zimewahi kulitawala soka la Tanzazni na kuwa na mafanikio makubwa, ila hatujawahi kuona mojawapo ya hizo timu zikitandaza soka maridadi kama la hawa vijana wa Gamondi.

Yanga ya Gamondi wanapiga mpira wa level za juu sana, Mpira mkubwa, mpira wa kiwango cha juu sana kiasi ambacho wapinzani kufungwa goli 5 wanaona ni kitu cha kawaida..

Uchezaji wa hii timu unaweza kuifananisha na ile barca ya pep ilipokuwa ikitawala soka la ulaya kwa kutandaza kabumbu maridadi sana

Hata kipofu atakubaliana namimi yakuwa kwa mpira huu unaopigwa na Yanga ya Gamondi, ndio mpira mtamu zaidi kuwahi kuonekana katika ardhi ya Tanzania.

Kama unakumbukumbu kuna timu yoyote imewahi kucheza soka tamu kama hili hebu tiririka hapo chini......
 
Uko sahihi.

Japo ubora wa Yanga hauna mchango wowote mkubwa kwa timu yetu ya Taifa. Almost wanaowika karibu wote sio waTz

Ile barca ya Pep iliingiza zaidi ya wachezaji 5 first eleven ya Spain national team. Wakachukua Euro 2008, World Cup 2010 na Euro 2012.

Kiufupi kama Taifa hatufaidiki
 
Siyo kazi ya Yanga kujenga timu ya Taifa, hayo ni majukimu ya TFF kuunda Academy nyingi.

Yanga tunahitaji heshima ya club.
 
Na hata ikitokea gamondi kaondoka, nadhan Bado team itapata mwalim mzuri over wachezaji wenye viwango.
 
Yanga na Simba kwa nyakati tofauti zimewahi kulitawala soka la Tanzazni na kuwa na mafanikio makubwa, ila hatujawahi kuona mojawapo ya hizo timu zikitandaza soka maridadi kama la hawa vijana wa Gamondi.

Yanga ya Gamondi wanapiga mpira wa level za juu sana, Mpira mkubwa, mpira wa kiwango cha juu sana kiasi ambacho wapinzani kufungwa goli 5 wanaona ni kitu cha kawaida..

Uchezaji wa hii timu unaweza kuifananisha na ile barca ya pep ilipokuwa ikitawala soka la ulaya kwa kutandaza kabumbu maridadi sana

Hata kipofu atakubaliana namimi yakuwa kwa mpira huu unaopigwa na Yanga ya Gamondi, ndio mpira mtamu zaidi kuwahi kuonekana katika ardhi ya Tanzania.

Kama unakumbukumbu kuna timu yoyote imewahi kucheza soka tamu kama hili hebu tiririka hapo chini......
Kulikuwa na ile Simba ya Kishingo, ile nayo ni Moja ya timu iliyopiga mpira mkubwa mnoo.
 
Back
Top Bottom