Hii Ya Katibu wa Mbunge Lema Imekaaje?

katibu ndani bado yeye

Apparently huyu jamaa ni longtime second hand man na mshirika wake wa muda mrefu. Sasa inawezekana baada ya mh! kuungama kuacha tena kujihusisha na hizi kazi kumbe swahiba wake alikuwa bado anaendelea kisirisiri.

Ninamhurumia sana Kamanda Lema,maana alipashwa awe ameshafanya homework ya kutosha...huyu jamaa anaweza kumharibia sana hasa ukizingatia yeye ni waziri kivuli wa mambo ya ndani. Kaazi kweli kweli.
 
Kuna watu wa anina mbili, wajinga wasio jua ukweli , na wapumbavu wasioamini hata wakiambiwa ukweli.
Chaguo la kundi la kuingia ni la mtu mwenyewe.

Si kila unachokiamini wewe basi kila mtu akiamini,
mnatofautiana utashi kwa hiyo sioni sababu kwanini
umlazimishe mtu akubaliane na kile unachokikubali
wewe. Na hata kama ni kweli lakini uwasilishaji
wake wa kishabiki ndo' ambao watu hawaukubali.
 
Nakubaliana na wewe...
Ilikuwa hivi mara tatu asubuhi TBC
Katibu wa mbunge wa Chadema, Godbles Lema akamatwa kwa ujambazi. yaani Godbless Lema lilisemwa mara tatu na ya nne ndipo akatajwa mtuhumiwa halisi Mgonja. Shame on TBC.
 
Sitashangaa ikiwa kweli.....mbona Msekwa kafanya uharamia kwenye mbuga za wanyama ambao ni zaidi ya ujambazi!!??? Mbona mtoto wa nanilii inasemekana anauza MADAWA YA KULEVYA!!?? Tanzania kila kitu kinafanyika wadau, tatizo ni pale unapokua upande tofauti na wanaohodhi mfumo wa utawala, cha moto utakiona!!!
 
huyo katibu ni binadam na anaweza kuwa jambazi

Your correct, Kama ni kweli huyu atakuwa na tofauti gani na yule katibu wa wizara mwenye skandali inayoelekea kukaliwa, funika kombe mnanaharamu apite. Yaleyale ya kumchoma kibaka moto na kumlamba miguu fisadi, wamelaaniwa baadhi ya waTZ.
 
Kamanda Zombe alishawahi kusema jambo kuhusika kwa Mh Lema na haya mambo.. Je katibu wake anaweza kuhudhihirishia umma juu ya matamshi ya Zombe?
 
huyo katibu mgonja aliashaachishwa kazi na ofisi ya mbunge lema muda mrefu sana na sababu kubwa ilikuwa tabia yake ya kupenda kukopa fedha kwa watu mbalimbali kwa kutumia jina la mbunge alikuwa mtu lifist sana anaye penda nguo za gharama na mambo mengine mengi na mwandishi aliyeandika wa habarileo ana uwezo mdogo sana anafahamika elimu yake darasa la saba
 
Abdala hasan nimependa ulvyochambua habar hii ya kutengeza,tofaut na hapo,mwandishi anasema kuwa kamanda wa polisi mkoa alisema yuko safarini na hajui kuhusu hlo tukio labda mwandishi awasiliane na mkuu wa upelelezi,at da same time mwandishi anasema kamanda wa polisi alithibisha kukamatwa kwa majambazi na kudai walishikwa na bastola,so tuelewe kipi hapo,kwa ushauri wa bure ningependa kuwashauri wamiliki na vidampa wa magamba hata kama ukitengeneza story iendane na wakati na ikidhi matakwa ya uandishi,alafu huu sio mda wake wa kuandaa story kwa kutumia title ya mtu maarufu ili uuze kijarida chako coz watu wameelimika na utaona hata hakuna atakae shtuka na kaheading kenu badala yake wanawadharau.2mpavu zenu.
 
Mimi wala sikuguswa na utuhumiwa wa ujambazi wa Mgonja, bali kusikia neno "Katibu wa Mbunge".
Hivi wabunge wetu wana makatibu? Nilikuwa sijui.

Kila mbunge ana katibu wake au baadhi ya wabunge tu? Ni chaguo lao kuwa na makatibu au kuna sheria/kanuni inawalazimisha? Nani anawalipa makatibu hawa? Mbunge mwenyewe, chama chake au serikali?

Mnaojua, naomba mnijulishe.
 
Si kila unachokiamini wewe basi kila mtu akiamini,
mnatofautiana utashi kwa hiyo sioni sababu kwanini
umlazimishe mtu akubaliane na kile unachokikubali
wewe. Na hata kama ni kweli lakini uwasilishaji
wake wa kishabiki ndo' ambao watu hawaukubali.
Bwana mukubwa, hapa hakuna suala la imani.
We go with the facts.
FACT: Tuhuma za Godbless Lema kuwa na uhusiano na majambazi zimekuwepo muda mrefu(hata kama hupendi, most recent by Zombe)
FACT: Mshirika wa karibu wa Godbless Lema ametiwa mbaroni kwa ujambazi.
It takes only little intelligence to connect the dots, na hapo HAKUNA IMANI, ni bongo lako tu.
 
Kamanda Zombe alishawahi kusema jambo kuhusika kwa Mh Lema na haya mambo.. Je katibu wake anaweza kuhudhihirishia umma juu ya matamshi ya Zombe?

Kama ni kweli basi Lema na Zombe walikuwa wakifanya ujambazi pamoja,
hawezi kumshutumu ujambazi wakati yeye alikuwa kwenye mamlaka
ya kuzuia ujambazi, na iweje aje kusema sasa wakati keshastaafu?
 
Mimi wala sikuguswa na utuhumiwa wa ujambazi wa Mgonja, bali kusikia neno "Katibu wa Mbunge".
Hivi wabunge wetu wana makatibu? Nilikuwa sijui.
Kila mbunge ana katibu wake au baadhi ya wabunge tu?
Ni chaguo lao kuwa na makatibu au kuna sheria/kanuni inawalazimisha?
Nani anawalipa makatibu hawa? Mbunge mwenyewe, chama chake au serikali?
Mnaojua, naomba mnijulishe.

Mkuu wabunge wote wanatakiwa kuwa na makatibu/wasaidizi na hao wanalipwa kupitia posho anazochuua mbunge kwa kifupi ni kwamba wanalipwa na Bunge.
 
Kuna watu wa anina mbili, wajinga wasio jua ukweli , na wapumbavu wasioamini hata wakiambiwa ukweli.
Chaguo la kundi la kuingia ni la mtu mwenyewe.

Unachohitaji ni high dose ya CPZ,Chlopromazine maana schizophrenia inakutesa mda mrefu WARD 13 itakufaa pale MIREMBE.

Hii elimu ya sekondari kwa miaka miwili inatuletea matatizo
 
huyo katibu mgonja aliashaachishwa kazi na ofisi ya mbunge lema muda mrefu sana na sababu kubwa ilikuwa tabia yake ya kupenda kukopa fedha kwa watu mbalimbali kwa kutumia jina la mbunge alikuwa mtu lifist sana anaye penda nguo za gharama na mambo mengine mengi na mwandishi aliyeandika wa habarileo ana uwezo mdogo sana anafahamika elimu yake darasa la saba

We unafikiri bila kumtaja Lema nani angeipa umuhimu habari hiyo?
Pia wanatumia kama mtaji kuidhoofisha Chadema huko Igunga...
 
Bwana mukubwa, hapa hakuna suala la imani.
We go with the facts.
FACT: Tuhuma za Godbless Lema kuwa na uhusiano na majambazi zimekuwepo muda mrefu(hata kama hupendi, most recent by Zombe)
FACT: Mshirika wa karibu wa Godbless Lema ametiwa mbaroni kwa ujambazi.
It takes only little intelligence to connect the dots, na hapo HAKUNA IMANI, ni bongo lako tu.

siku ujuha ukikuacha utaacha huu upupu tetesi ndiyo zimekuleta kwenye conclusion hii kwa facts mfu zinazoendeshwa na mshawasha wa hisia.
 
Mantiki inakataa kabisa.
Hivi katibu wa Mbunge (let say it is true ni katibu wake, am not sure, sijasoma habari) ana uhusiano gani na Mbunge ktk mambo binafsi? Je, Katibu wa Mbunge aktoka ofisini ni jukumu Mbunge kujua kama anafanya nini? Wapi? na Nani?. Jina la Lema hapo linaingiaje?. Hivi kesho akimpiga mke wake, akiiba tunamhusisha mwajiri wake Lema tena?

Pili, Ninasikitika kwamba habari hizo zimeandikwa ktk gazeti ambalo si la udaku. Je, Mjomba, shangazi, marafiki zake, majirani, nk mmoja wao akiiba, kichwa cha habari lazima kianze na jina Lema?

Tatu, kwanini habari hizi zianze kwa kasi tangu yeye aliposoma maoni ya upinzani yaliyoichafua sana Serikali ya CCM hasa jeshi la polisi kwa kuua raia bila sababu huku wakishindwa kukanusha hoja ya Lema? Kwanini leo?

Kila ninapowaza mantiki inakataa kabisa. Iko siasa ya hatari ya ccm nyuma jambo hili ambayo inaweza kuvuruga amani yetu. Sitashangaa kesho wakisema Dr Slaa, Mbowe, Mnyika Wenje nk ana hili na lile.

Nimepata wasaa nimesoma hiyo habari kwenye mtandao. Sikwenda mbali nikakutana na maneno haya..... "Alisema taarifa zaidi za tukio hilo zitatolewa leo baada ya upelelezi kukamilika kwani kwa sasa wanakamilisha baadhi ya maelezo kwa watuhumiwa wengine waliokamatwa."

Nimeshangaa kuwa wanweza kuwa wamekamilisha upelelezi leo hii wakati katika matukio mengine huwa kesi zinacheleweshwa kwa upelelezi kutokamilika. Hii basi inaonyesha kuwa Polisi walishafanya homework yao vizuuuri walikuwa wanasubiri tu aingie mtegoni! Au ndio mwanzo wa kufanyia kazi taarifa za Zombe? Mgonja asije akamtaja Boss wake ikawa kitimtim!!
 
Back
Top Bottom