Hii Ya Katibu wa Mbunge Lema Imekaaje?

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Ndugu WanaJF leo asubuhi wakati naelekea kazini nilikuwa nikisikiliza Radio Free Africa na nikasikia kichwa cha habari kimoja magazetini kikisema Katibu wa Mbunge wa Arusha mjini anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.

Kwa bahati mbaya network huku niliko ikawa down mawasiliano yakawa magumu kwa hiyo sikuisikiliza hiyo habari hadi mwisho.

Imekaaje kwa waliosikiliza ama kusoma gazeti husika.
 
Ndugu WanaJF leo asubuhi wakati naelekea kazini nilikuwa nikisikiliza Radio Free Africa na nikasikia kichwa cha habari kimoja magazetini kikisema Katibu wa Mbunge wa Arusha mjini anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.

Kwa bahati mbaya network huku niliko ikawa down mawasiliano yakawa magumu kwa hiyo sikuisikiliza hiyo habari hadi mwisho.

Imekaaje kwa waliosikiliza ama kusoma gazeti husika.
habari yenyewe inapatikana hapa mkuu isome.
HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
 
Arusha sasa hivi kuna vituko vingi wanatafuta kila njia kuiharibia chadema tusubri tuone leo asubuhi mwenyekiti wa chadema aliulizwa kuhusu hilo alisema anafuatilia Hilo tukio pia huyo Mgonja aliwahi kuwa katibu kwa mda fulani hivo kwa sasa sio katibu hiyo ni kutoka radio 5 Leo asubuhi taarifa zaidi tutapata mambo yakikaa sawa.
 
Haya magazeti yakuogopa sana nhasa haya ya kutoka Mtaa wa LUMUMBA yote habari zake zinatengenezwa watu wanakaa room kutengeneza habari.
 
Habari inaelekea ni ya kweli, ila imeandikwa kishabiki. Msomaji anapata impression ya kuwa Lema anahusika. Hapo ni ushabiki wa kisiasa zaidi ndiyo unaojionyesha.
 
Kama kweli ni Jambazi, basi acha sheria ichukue mkondo wake. Lakini nina wasiwasi sana na hii serikali kwa kubambikia watu kesi. Kama mtakumbuka wale Wauza madini wa Mahenge. Kwa hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa tusishangae tukaambiwa kuwa eti Dr. wa Ukweli, Slaa naye ni Muuza Unga! Maana kila siku tunasikia tu kwenye magazeti ya Uhuru na Habari na Jamba Leo kwamba Majina ya Wauza Unga yametajwa, lakini ukisoma gazeti toka ukurasa wa kwanza hadi habari za michezo, hukuti jina la mtu yeyote lilotajwa zaidi ya jina la Nzowa ambaye alitaka kumbambikia Mtoto wa Mengi madawa ya kulevya. Shame!

Yalianza Tunisia, yakaja Misri, sasa Libya. Baada ya hapo.................

Mkweree na Majambazi wenzio mjishike!
 
huyo katibu ni binadam na anaweza kuwa jambazi

Nakubaliana na wewe kabisa, kwa sababu kuna jina la Mh Lema tu magazeti ya gamba wanalivalia njuga mbaya lakini list za majina ya wauza unga zinatajwa tu bila majina halisi kuwekwa hadharani.
 
Magazeti mengine, angalia hii. Ni kweli tunamshikilia kwani watuhumiwa wa ujambazi waliokamatwa wamemtaja kuwa aliwakodishia gari na limekwenda kufanya uhalifu," alisema RCO Paul. Gazeti hilo hilo cheki hii

Vyanzo vya habari vilidai kuwa polisi waliwabana watuhumiwa wengine wa ujambazi ambao ni wakazi wa Sekei na kumtaja Katibu huyo wa Mbunge kuhusika kuwabeba na kushirikiana katika matukio hayo ya ujambazi, lakini alifanikiwa kukimbia.

Likaendelea tena. Hata hivyo, habari zaidi zinadai kuwa Mgonja ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo na alikimbia baada ya kufanya uhalifu na kuwatosa watuhumiwa wengine na kutokomea kukimbia kukamatwa na polisi.
Huu uandishi gani wa habari za kiuchunguzi....?





gazeti lenyewe siyo la kuaminika sana!wenye ukwel watujuze zaidi
 
Back
Top Bottom