hii tabia ya kutupa vitu kwenye madirisha ya daladala mnaionaje?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
wadau hii tabia huwa inanikera kichizi! wadau mnaionaje? au ni ushamba wangu mjini?
 
Vitu gani? Au unamaanisha uchafu? Kama ndo hivyo naona ni utamaduni wetu.. Sisi waafrika huwa sio wasafi sana na hatupendi mazingira yaliyotuzunguka yawe masafi.
 
tena sana hasa ukimuona bibi anafagia wewe unatupa pakiti ya biskuti au ice cream za azam bora hata utupe chupa watu wataokota..

niliwahi kushuhudia mama mmoja akiokota chupa ya maji na kutupia ndani ya gari ambayo dereva wake ndio alitupa chupa nje nikafurahishwa sana na uamuzi wa yule mama.
 
Wabongo sisi wachafu by nature, mkifika nchi za watu mkafanya hizo tabia mtaumbuka maana basi zima litasimama na wananchi wote watakuwa after you, utaumbuka!
 
Samahani kidogo naomba kuweka angalizo lenye msisitizo.Sio watumia daladala peke yake wanaotupa vitu kupitia madirishani hata hao mnaowafikiria wako 'civilized' kwenye VX zao wanatupa pia.
Last week kuna mwehu fulani kwenye foleni pale makutano ya uhuru na msimbazi alitupa container kubwa la Ice-cream alikuwa kwenye Hilux mayai(double cabin) full kiyoyozi(hawa mnawaonaga wastaarabu kumbe vijihela vinawasitiri)ikabidi niliokote nilirudishe kule nyuma paliko wazi akashuka kwenye gari huku akimwaga matusi utafikiri mpiga kampeni wa CCM kumbe pembeni alikuwa amesimama traffic police akamwambia rudi kwenye gari lako haraka akarudi anatweta kwa hasira.
Jamii yote ya watanzania imefanya urafiki na tabia hii ya ajabu.Tubadilike jamani.
 
Ni tabia mbaya tunachafua mazingira yetu wenyewe halafu baadae tunalalamika serikali haitimizi wajibu wakati ni wajibu wetu pia kuhakikisha mji unakuwa safi. Mimi binafsi huwa napambana na mtu anayetupa uchafu nje kutoka kwenye daladala na hata nikiwa kwenye gari binafsi. Kuna siku nilimkoromea mdada mmoja kwenye daladala alinimind lakini ujumbe nilifikisha na karatasi lake la ice cream ya azam akaweka kwenye pochi.
 
Pamoja na kuwa inakera lakini ndio ishazoeleka hivyo. Hata wewe naamini umeshawahi kutupa kitu dirishani mwa daladala.
 
Pamoja na kuwa inakera lakini ndio ishazoeleka hivyo. Hata wewe naamini umeshawahi kutupa kitu dirishani mwa daladala.
Misijawahi tupa bana, nashikia mkonono na kama nichupa naweka kwenye gari wao wnwjua sehemu nzuri ya kupeleka, nimeona baadhi ya magari ya mikoani siku hizi yana distbin ila watumiaji bado wachache, hebu fikiria unakula muhindi ukimaliza ghafla unaona gunzi ni uchafu usiovumilika hata dakika moja unatupa dirishani sasa inamaana ulikuwa unakula mahindi kutoka kwenye uchafu?
 
Samahani kidogo naomba kuweka angalizo lenye msisitizo.Sio watumia daladala peke yake wanaotupa vitu kupitia madirishani hata hao mnaowafikiria wako 'civilized' kwenye VX zao wanatupa pia.
Last week kuna mwehu fulani kwenye foleni pale makutano ya uhuru na msimbazi alitupa container kubwa la Ice-cream alikuwa kwenye Hilux mayai(double cabin) full kiyoyozi(hawa mnawaonaga wastaarabu kumbe vijihela vinawasitiri)ikabidi niliokote nilirudishe kule nyuma paliko wazi akashuka kwenye gari huku akimwaga matusi utafikiri mpiga kampeni wa CCM kumbe pembeni alikuwa amesimama traffic police akamwambia rudi kwenye gari lako haraka akarudi anatweta kwa hasira.
Jamii yote ya watanzania imefanya urafiki na tabia hii ya ajabu.Tubadilike jamani.
aise huyo jamaa harudii tena, vipi hakuwa na gun? maana siku hizi sijui zimeshuka bei au watz ndio wamekuwa na hela!
 
Si tu kwenye daladala, saa nyingine mtu yupo kwenye usafiri wake wa gharama halafu anafungua kioo anatupa fuko limejaa maganda karanga......,mie nashindwa kuwaelewa kwa kweli........

tena sana hasa ukimuona bibi anafagia wewe unatupa pakiti ya biskuti au ice cream za azam bora hata utupe chupa watu wataokota..
 
Mi niliwahi safiri kwa boat nikaona watu wanatupa chupa za plastic na plastic bags ndani ya maji.
Kuna ndoo za taka kila kona ya boat ila watu wanajifanya hawaoni.
na wakisha tupa wanabaki kuliangaliaaaa hadi linapo potea, wanatupa lingine.
Hata wakati ukisafiri na kuvuka a national park, kuna watu wanafanya hivo hivo.
Sijui hii tabia inaweza kukomeshwa vipi ila mimi nikiona hivo hua nawaambia sana tu.
 
Mara zote huwa nachukua hatua ama kumsema alotupa takaa au kumrejeshea kama niko kwenye nafasi poa! Ila nilitaka kupigwa na jamaa baada ya kuokota can ya beer alotupa nikarudishia kwa gari yake!

Huwa inaudhi sana
 
nshashuhudia mtu katema kohozi zito kupitia kioo cha gari ndogo,bahati mbaya kajisahau kama kafunga vioo pata picha niliishia kucheka tu
 
Unatakataka yako ihifadhi hadi utakapopata eneo la mahsusi la kutupia taka.

Kwa Tanzania kusikokuwa na mapipa ya taka barabarani, basi beba taka yako hadi nyumbani kwako.
 
naona ifike kipindi baraza la mazingila NEMC watoe msimamo wao kuhusu hili jambo
 
aise huyo jamaa harudii tena, vipi hakuwa na gun? maana siku hizi sijui zimeshuka bei au watz ndio wamekuwa na hela!

Gun atoe wapi mkuu??Alikuwa bonge fulani hivi nyama uzembe wa kutembea anakula ice-cream njiani sanasana angenivamia hovyohovyo na i would've knocked his lazy bu*t all the way to ICU then start my KS and vanish.Usicheze na jogoo wa kienyeji.
 
Hahahaha, unasema tu, now that he is far from you.
Pale hukumwambia chochote, ukamwacha polisi aseme. lol
 
Back
Top Bottom