TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,774
- 21,270
SGR yetu ya kwanza toka kuumbwa kwa dunia ilijaribiwa kwa mbwembwe pamoja na wadau kuhoji vipi umeme ukikatika itakuwaje?
Mkurugenzi mkuu wa TRC ndg Kadogosa alijibu kwa mbwembwe tuna backups transformers na diesel engine za dharula, pamoja na majibu hayo umbali uliotumika haukuweza kutoa jaribio bora kuliko matarajio.
Nje ya Tanzania huko wanapoanziaga kuunda haya mausafiri as China, Gari la kuruka na kutua kwa wima la umeme lililotengenezwa na kampuni ya wazawa kwa jina; electric Vertical Take-Off and Landing - eVTOL, hivi majuzi lilifanya jaribio lake la kwanza.
Katika kukamilisha safari kati ya miji miwili ya Shenzhen na Zhuhai yenye umbali wa 160km iliweza kutumia dakika 20 pekee, ambapo kulinganisha na safari ya kawaida huchukua dakika 70 kwa boat na zaidi ya saa mbili kwa kutumia gari.
Kwa kawaida usafiri huu hujulikana kama "teksi za angani" magari haya yana uwezo wa kupaa wima, sawa na helikopta, hivyo kuondoa ulazima wa kutumia viwanja vya ndege vya kawaida na kwenye njia za kurukia ndege.
NB. Wakati dunia inasogezwa zaidi kuwa karibu kwa wanaoishi duniani, kuna mataifa mengine wanarudi nyuma au yanajikongoja.
Sisi kama Tanzania pamoja na kwamba yawezekana tusifike kuwa sawa na wachina ila hata kupitia hii SGR basi tufupishe muda wa kukaa safarini.
Hii ni kwa sisi wananchi wa kawaida, juzi imetoka taarifa kuhusu matumizi ya usafiri nchini, imeonekana walio wengi hawawezi kumudu garama kubwa, so kazi kwenu ndg Kadogosa.
Nawasilisha.