Mtumishi Wetu,
Miaka ya 2003-2006 wakati nikihusika kwa karibu kwenye sekta ya Utalii, nilipata kumjua Mama mmoja anaitwa Mary Kalikawe. Huyu Mama amefanya mapinduzi makumbwa kuitangaza Kagera akitumia vivutio ulivyoorodhesha kupitia kampuni yake iitwayo KIROYERA TOURS. Na alipata mafanikio makubwa Kitaifa na Kimataifa.
Kupitia jitihada zake alipata vikombe, ngao za Utalii na mchango wake umetambuliwa na kukukabalika UNESCO. Mama Tibaijuka akiwa UNHABITAT naye alijitahidi kumpa ushirikiano Mama Kalikawe. Hivi sasa simsikii sana Mama Kalikawe lakini najua hajakata tamaa. Na kama sikosei anaendesha museum site kule Nyamkazi.
Lakini pia kuna Project nyingine ya ujenzi wa Kikale na Nyaruju ya Mugasha kule Katuruka, Ntoma. Wengi hawajui kwamba tayari utafiti wa mabaki ya kale umethibitisha kuwa ujuzi wa kale kabisa wa kufua vyuma ulipatikana KATURUKA. Ni katika eneo hili ndipo mnara mrefu kabisa sawa na ule wa Babeli ulinza kujengwa kuelekea mbinguni. Na ulipovunjika masalia yake yaliangua mbali sana. Hadi sasa unaweza kuona masalia ya vyuma vya mnara huu pale Kanazi. Kwa bahati mbaya Project hii imeingia dosari baada ya mzungu aliyekuwa anaiongoza kutaka kujinufaisha zaidi bila kuwajali wenye Kikale
Safi sana kijana yaani ambao hawakuisoma hii walimisi vitu vingi..........niliweka hadi part 2
ndiyo maana watu wa pande hizo wa afya sana..maji kwa wingi we acha tu..
Wakora waitu!<script type="text/javascript" src="safari-extension://com.ebay.safari.myebaymanager-QYHMMGCMJR/75b4aaeb/background/helpers/prefilterHelper.js"></script>