Hii mikataba mibovu tatizo ni UDSM

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Nimefuatilia kwa Karibu. Nimegundua Tz kuwa masikini kwa miaka zaidi ya 60 chanzo kikuu ni aina ya Graduates tulio nao. Na viongozi wengi na wenye vyeo vikubwa nchi hii ni Graduates wa UDSM.

Mfano wa viongozi wabovu ambao ni mazao ya UDSM ni Prof. Mkumbo. Ana Uprofesa wa mchongo. Anatetea huu mkataba mbovu utadhani siyo Profesa.

Mwezi wa 5 , 2023 Bungeni akawa anapinga mfumo wa Ajira wa Utumishi wa Umma vyuoni, eti nafasi zirudishwe kwa vyuo. Ili waingize watoto wao pekee. Tiyari BoT, na TRA wamejiengua utumishi wa umma. Wanajitangazia kazi wao na kuajiri. Watoto wa maskini ajira za BoT na TRA bye bye!

Pia, nilistushwa sana na tangazo la kazi mwaka huu 2023. Nafasi za Economists (Bunge), eti sifa uwe Graduate wa UDSM! Rubbish! Kwa uchumi huu wa kusukuma troli miaka 60 na UDSM? Na ukifuatilia hata hao washauri wa Rais, Wanasheria wengi, na Makatibu wakuu wa Wizara ni Graduates wa UDSM.

Watanzania, adui wa Tanganyika ni UDSM.
 
Ni maoni yako, anbayo sidhani kama yana ukweli wowote.

Yaani mtu uende chuo na miaka 19 umalize na miaka 22, ukae chuo miaka mitatu halafu eti useme tabia yako ya wizi imetokana na chuo ulichosoma?
 
Chuo kina changia. Kama ilivyo mobpsychology kwa vijana.
 
Ni maoni yako, anbayo sidhani kama yana ukweli wowote.

Yaani mtu uende chuo na miaka 19 umalize na miaka 22, ukae chuo miaka mitatu halafu eti useme tabia yako ya wizi imetokana na chuo ulichosoma?
Kwa hili niwatetee UDSM Alumnus, wapo waliosimamia taaluma na maadili kama akina Assad ila mwisho wa siku walifukuzwa. Nchi yetu siasa ndio machinery ya kuendesha nchi na sio taaluma. Ukijifanya una misimamo yako na elimu yako utaishia kuwa Junior servant huko maofisini na wakikuonea huruma sana utapelekwa huko vyuoni ukafundishe. Hii nchi wewe ukitaka kula nenda na tune ya kusifia tu wala usikosoe. Hapo utapata teuzi kwenye bodi za mashirika, utapata teuzi za ukatibu na ukurugenzi n.k

Mwisho wa siku hao wasomi wanaamua kuwa watumwa tu wa wanasiasa ila mkono uende kinywani (njaa haina baunsa) huku kijikikundi kidogo cha elites wakiitafuna nchi kwa kadri wanavyoona kipi kianze kuliwa na kipi kifate. Baada ya kuuza kila kitu chetu kilicho chini ya ardhi sasa tumehamia kuuza vilivyo juu. Kazi ipo!!
 
How? Tuwe specific na realistic.... Nachokiona hapa ni mihemko.

Kwanini udsm kwanini sio Udom?

Kama ni lawama basi, familia za watanzania ndo zilaumiwe
Ulisha wahi kufanya tafiti yoyote duniani hapa?
 
Kwa hili niwatetee UDSM Alumnus, wapo waliosimamia taaluma na maadili kama akina Assad ila mwisho wa siku walifukuzwa. Nchi yetu siasa ndio machinery ya kuendesha nchi na sio taaluma. Ukijifanya una misimamo yako na elimu yako utaishia kuwa Junior servant huko maofisini na wakikuonea huruma sana utapelekwa huko vyuoni ukafundishe. Hii nchi wewe ukitaka kula nenda na tune ya kusifia tu wala usikosoe. Hapo utapata teuzi kwenye bodi za mashirika, utapata teuzi za ukatibu na ukurugenzi n.k

Mwisho wa siku hao wasomi wanaamua kuwa watumwa tu wa wanasiasa ila mkono uende kinywani (njaa haina baunsa) huku kijikikundi kidogo cha elites wakiitafuna nchi kwa kadri wanavyoona kipi kianze kuliwa na kipi kifate. Baada ya kuuza kila kitu chetu kilicho chini ya ardhi sasa tumehamia kuuza vilivyo juu. Kazi ipo!!
Hata mimi namshangaa mtoa mada kulaumu UDSM akati anajua wanao run show ni wanasiasa.
 
Back
Top Bottom