Hii kero ya matrafiki Arusha imezidi

Kuwapa rushwa tunataka wenyewe...
Hakikisha gari lako halina kasoro yeyote...
Na ukiendesha fuata sheria za barabarani, hakuna trafic atakayekugusa...

Tusiwahukumu kwa kujaa barabarani, mto NDURUMA na kwa mrefu kiutawala ni maeneo tofauti, kwa refi huwa wanakaa upande wa kushoto ukitokea Moshi ili kuhakikisha usalama kwa magari yanayoingia kadhalika kwa maretu, ukiona wamezagaa kuna jambo wanalolifuatilia na huo ukaguzi ni zuga tu, tusiwazuie kufanyakazi. Rushwa ni utashi binafsi na hao Takukuru wamechoka kwa kukosa meno, kesi ya nyani umpatie tumbili haiwezekani, tumechoka ila tusiwagonge
 
Hicho ndiyo kitu kinachowafanya waone rushwa ni halali yao.
Hiki kitengo cha trafiki ni cha kufutwa kabisa Arusha. Huu uzi napropose uwe live stream ya trafiki wa Arusha.
Wanasumbua haswa yaani ni kero, kuna siku walinisimamisha Cedha hapohapo wakalazimisha kuniandikia notification kosa ni matumizi mabaya ya taa za barabarani wakati nimepita greenlight zikiwa zimeruhusu.
Ni tatizo kwa kweli hawa viumbe kwa hapa Chuga

Mkuu nikuchukua hatua
 
Kuwapa rushwa tunataka wenyewe...
Hakikisha gari lako halina kasoro yeyote...
Na ukiendesha fuata sheria za barabarani, hakuna trafic atakayekugusa...

Hata gari likiwa jipya hawakosi kasoro juzi walinitoza faini eti wheel nut moja haipo, upande mwingine kulikuwa na mdada pembeni wamemkamata wanamkomalia Kwa nini yuko mwenyewe kwenye gari wakati ni gari la watu wanne, nkabaki nacheka tu
 
Hahahahaaaaa eti kwanini uko peke yako mamaeee
 
Hata gari likiwa jipya hawakosi kasoro juzi walinitoza faini eti wheel nut moja haipo, upande mwingine kulikuwa na mdada pembeni wamemkamata wanamkomalia Kwa nini yuko mwenyewe kwenye gari wakati ni gari la watu wanne, nkabaki nacheka tu

Ha ha ha ha ha ha!!! Hawa watu ni wapumbavu sana.

Juzi walikuwa wanakamata taxi bubu sasa jamaa wa taxi fulltime vioo juu lock ndiii, kuna katraffic kamoja ndiyo kalikuwa kingozi incharge wa hiyo kazi ktk kamatakamata.

Jamaa akaanza kuvunja vioo vya magari ya watu na kutukana wenzake matusi makubwa haswa kwamba kwanini na wao hawavunji vioo vya magari na kukamata hao madreva.

Yaani hii ndiyo serikali ya mkwere yenye utawala wa sheria. Poor govt.
 
Tusiwahukumu kwa kujaa barabarani, mto NDURUMA na kwa mrefu kiutawala ni maeneo tofauti, kwa refi huwa wanakaa upande wa kushoto ukitokea Moshi ili kuhakikisha usalama kwa magari yanayoingia kadhalika kwa maretu, ukiona wamezagaa kuna jambo wanalolifuatilia na huo ukaguzi ni zuga tu, tusiwazuie kufanyakazi. Rushwa ni utashi binafsi na hao Takukuru wamechoka kwa kukosa meno, kesi ya nyani umpatie tumbili haiwezekani, tumechoka ila tusiwagonge

Traffic police akae kw maretuu kuzuga au kutafuna rushwa? Hakuna check point hata ya mabasi useme wanaangalia time table, hakuna ukaguzi wowote zaidi ya kukwambia, nipe leseni, unaenda wapi, huyu ni mkeo, gari yako ni ya rangi ya kijivu lkn hapa kwenye kadi imeandikwa gray hapo ndipo utasikia aroo arufonso Im.m. m. a muandikie huyu erfu serasini.

Hamna chochote wanachoangalia pale zaidi ya rushwa.
 
Ntaanza kuwataja Kwa majina kuna Juma Mmbongo na huyo Imma wa Usa hafai kabisa.... Malisa siku hizi katulia baada Ya kugongwa hapo kijenge
 
Ni kuwamalizia barabarani tuu, malitha ana bahati alikoswakoswa pale kanisa road mwenzake akapaishwa kwa baba straight.
Yuko usa siku hizi ila kwa mwwendo huu wanaokwenda nao lazima watafia wengi rodini.

Pipo are tired na huu usumbufu wao
 
attachment.php

Au tuwakolimbe kuwapunguza mzuka wa rushwa hawa watu?!! Mungu apishe mbali;
Ndugu yanhgu Jembe Afrika una hoja kubwa sana hapa na ya maana sana lakini; hawa ni ndugu zetu tu; shida ni mfumo wenyewe!! kama trafiki anapewa lengo (target figure) akusanye pesa kiasi fulani apeleke ama ofisini au kwa mkubwa fulani kwa sababu zake; trafik atafanyaje jamani?! hata wao ni binadamu; kazi ndizo zinatuweka mijini; wana familia kama sisi na malengo ya maisha mengine kama sisi?! kama huko juu wanakula rushwa kama panya!!; wao wafanyeje jamani au kanuni ya uadilifu inawahusu wao tu "foot soldiers on the beat"?!

Ushauri wa bure;
Option I:: Kuna dhana hii: if you can not fight them; better join them or else you will be the looser!; shauri yako Jembe Afrika; jiunge na mfumo; befriend or be polite to them utaiona Arusha kama free way za California au Autobhan za Ujerumani na kwingineko in the first world ambako mifumo na taasisi ziko so transparent kiasi kwamba kero kama hizi za hovyo hovyo huwezi kuziona huko Ughaibuni.

Option II: Jiunge na VuguVugu la mabadiliko; tuliondoshe hili Zimwi linaitwa CCM; Ukoo wa panya; lililovurugavuruga mifumo ya uwajibikaji likatufikisha hapa tulipo; Vilio kulia na kushoto, vilio juu na chini; Vilio katikati, magharibi, kusini mashariki na kaskazini; kila mahali ni UUUUUUUUUUUwiiiiiiiiiiiiiii!!
Jembe Afrika join the movement for reforms and reconstruction of mother Tanzania; that is UKAWA 2015
 
Hata Mwakyoma ni tatizo akipelekewa malalamiko Ya askari wake hafanyii kazi.... Dawa ni kuwafanya round about tu
 
Yaani ni shidaa. Kuna jamaa anaitwa Imma. Jamaa anadai hadi laki kwa kosa la taa ya plate namba. Ukigoma lockup. Wanadai askari ni wachache kumbe kituo kizima kimejaa matrafick.
Qmbao kimsingi ni waomba rushwa tuuuu.
 
Hata kama huna kosa lolote, usipowatoa lazima wakubambikizie, hawashindwi hata kukuwekea bangi kwenye gari waseme ni ya kwako kwa vile tuu hukutoa kitu. Na mimi nilishaapa nitamgongo mmoja. Ipo siku.
Yaani wakiona gari tu wanakuwa kama machangudoa wameona mteja.
 
Yaani ni shidaa. Kuna jamaa anaitwa Imma. Jamaa anadai hadi laki kwa kosa la taa ya plate namba. Ukigoma lockup. Wanadai askari ni wachache kumbe kituo kizima kimejaa matrafick.
Qmbao kimsingi ni waomba rushwa tuuuu.

Mi nilibishana naye hadi kutaka kushikana nae nikaishia lockup USA badae askari mwingine akaja kunitoa hawaogopi hata wakubwa wao
 
Usalama barabarani wao wanaangalia magari tu. Barabara unakuta ina mashimo tena yale hatarishi lakini hawatoi taarifa hata huko TANROAD. Maana kama wao ni maafisa wa usalama barabarani wanatakiwa kuhakikisha hata barabara ziko katika usalama wa kuweza kutumiwa
 
Traffic police akae kw maretuu kuzuga au kutafuna rushwa? Hakuna check point hata ya mabasi useme wanaangalia time table, hakuna ukaguzi wowote zaidi ya kukwambia, nipe leseni, unaenda wapi, huyu ni mkeo, gari yako ni ya rangi ya kijivu lkn hapa kwenye kadi imeandikwa gray hapo ndipo utasikia aroo arufonso Im.m. m. a muandikie huyu erfu serasini.

Hamna chochote wanachoangalia pale zaidi ya rushwa.

Aisee atakua mura huyo
 
Usalama barabarani wao wanaangalia magari tu. Barabara unakuta ina mashimo tena yale hatarishi lakini hawatoi taarifa hata huko TANROAD. Maana kama wao ni maafisa wa usalama barabarani wanatakiwa kuhakikisha hata barabara ziko katika usalama wa kuweza kutumiwa

Kweli mkuu
 
Ni kuwamalizia barabarani tuu, malitha ana bahati alikoswakoswa pale kanisa road mwenzake akapaishwa kwa baba straight.
Yuko usa siku hizi ila kwa mwwendo huu wanaokwenda nao lazima watafia wengi rodini.

Pipo are tired na huu usumbufu wao

Siku hiyo nilikuwa Kanisani pale Christ Church, nilisikia bang, kinaendelea na ratiba ya ibada. Nilipotoka nilikuta gari lililowagonga na viatu pembeni, niliwaonea huruma lkn ndo hivyo ishatokea.

Ukweli Traffic police wa Arusha na Manyara (barabara ya Arusha-Babati) ni shida.

Miaka kadha iliyopita nilikuwa natoka Arusha Alfajiri kwenda mkoa. Nilipofika karibu na Magugu trafiki Polisi akanisimamisha. Nilipoondoka tu, kilometa moja mbele, nikamkuta trafiki mwingine akiwa anaendesha baiskeli, aliponiona akasimamisha baiskeli yake na kunisimamisha. Kwa hasira nikamwambia yaani mwenzako amenisimsmisha hapo nyuma kidogo nawe unanisimamisha! Akaona aibu akasema 'nenda'. Inaonekana alikuwa anatoka kukesha kazini na alikuwa anatafuta hela vitafunwa vya kwenda navyo nyumbani kwake.
 
Yaani ni shidaa. Kuna jamaa anaitwa Imma. Jamaa anadai hadi laki kwa kosa la taa ya plate namba. Ukigoma lockup. Wanadai askari ni wachache kumbe kituo kizima kimejaa matrafick.
Qmbao kimsingi ni waomba rushwa tuuuu.

Huyu imma ndiyo alikuwa anavunja vioo vya magari akidai ni taxi bubu.
Na anajitapa hamtamfanya kitu, nadhani atakuwa ametumwa na wakuu wake coz agizo hilo lilitoka kwa mkuu wa mkoa na afisa mmoja wa polisi ngazi za juu Ar
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom