Hii kauli ya Kamishna wa TRA kwa biashara zilizofungwa ni kufanya 'damage control'

Barabara za miji mfano arusha machinga wamepanga bidhaa nje ya maduka ya watu what next,next ni mtu abomoe duka lake aajri vijana watandaze mzigo barabarani na kutembeza mitaani,je unategemea katika mazingira hayo mapato na ushuru vipatikane sio rahisi.Tunaitaji tuwe na mbinu mbadala financial inclusion for women and youth nasio wote kuwa machinga huku awalipi kodi.
 
Mkuu hili bandiko lako nilikua limenifanya nicheke
 
Kamishina kafanya vyema,kutoa taarifa hiyo, undani wake serikali inapaswa sisimua uchumi kwa mikakati madhubuti.Sector kilimo,ufugaji,madini tengeneza mabilionea wa kitanzania.Nashauri hii mikopo midogo ya vijana na kina mama isiwepo tujenge sector binasfsi imara vikundi na mtu watakaotoa ajira za uhakika.Tupunguze machinga na wachuuzi hakuna tija.Tuache siasa kufurahisha kila MTU.
Kuna machinga ambao wana mitaji mikubwa kuliko wenye maduka.unakuta mtu ametandaza vyombo barabarani mtaji wa kma 10m.kuna haja ya kuangalia haya mambo vizuri.tuache siasa.
 
Mkuu hili bandiko lako nilikua limenifanya nicheke
We cheka tu barabara zimejaa bidhaa ukipita na gari unaogopa usipite na mizigo ya watu na kuwakanyaga hata wahindi wamekuwa wajanja biashara mwaga barabarani shabani uza jioni leta hesabu na mzigo uliobaki je katika mazingira hayo kodi unaipataje?.
 
safiri hata ufike rukwa itakusaidia akili yako kujua nchi kubwa km hii haiwezi endeshwa kwa kodi za kumbi za starehe..unavyoandika dhahiri akili yako iko locked!
Mkuu mzunguko wa Pesa ni kitu muhimu katika nchi yoyote duniani,nchi zote duniani zinapigania wananchi wake wawe katika uchumi wa kati,kwasababu wananchi wakiwa katika hali ya kat maisha nguvu za matumizi zinaongezeka,nguvu za matumizi zikiongezeaka biashara zinashamiri,biashara zikishamiri serikali itakusanya kodi ya kutosha..

Mnacho kifanya nini ni kinyume chake,mnawafanya watanzania wawe maskini,watanzania hivi sasa hawana hata wa uwezo wa kununua chakula kwa mama nitilie,maduka yanafungwa kwasababu hakuna mnunuzi,maduka yakifungwa serikali inakosa kodi,..

Nilichozungumza mimi sio serikali kukusanya kodi kwenye kumbi za satarehe,nilichoongelea ni vipi serikali inakata mzunguko wa pesa kwa watanzania,kuanguka kwa mzunguko wa pesa ndio kuanguka wa ukusanyaji kodi kwa TRA,...

Sasa tuseme hao wafanya biashara waliofunga maduka yao wameamua kuyafungua,wale waliokimbiza biashara zao nchi jirani wamerudi,hizo bidhaa zao zitanunuliwa na nani!? wakati watanzania hawana pesa!??,hakuna mzunguko wa pesa..

Mkuu mimi sio kama wewe akili yangu inafanya kazi sana,nimejifunza kufikiri kwa na kuamua kwa uhalisia wa jambo sio kwa hisia zangu,Kuhusu kudsafiri nimesafiri dunia yote,hakuna nisikofika na ndio maana mawazo yangu na yako hayawezi kuwa sawa,hivi sasa niko Tonga,sijui kama hio nchi umeshawahi kuisikia,nakula maisha nitarudi Tanzania baada ya mwezi mmoja..
 
Kufungua biashara hadi uwe na TIN no. na ukiwa nayo hata japo biashara ni ndogo TRA kila siku ni kodi bila kuangalia unapata nini! PIA watoto wako hawatapa mikopo vyuo vikuu! bora kufanya biashara za nyanya tu sasa.

This is what surprises me, kodi hapa nchini inatumika kama adhabu. Kuna vijana wameajiriwa na TRA nadhani hawana uelewa wa maana ya serikali kukusanya kodi. Wanakuja kwa kutishia kuifunga biashara yako na kupiga mnada ulivyo navyo kama hukubali kulipa kodi waitakayo. Katika hilo kunakuwa na mchanganyiko wa malengo binafsi na ya serikali. Sasa serikali makini inakussanyaje kodi kutoka kwa mfanya biashara mpya ambaye hata hajaanza mauzo ya chochote katoka tuu kuregister, kapata leseni leo, kesho TRA kawasili kukusanya kodi? Hana haja hata ya kuona risiti wala umeajiri nani kufanya kazi, yeye anataka kumridhisha msimamizi wake kuwa amemkamua mfanya baishara kwa kumtishia mpaka amelipa kodi. Msimamizi mpuuzi anajumlisha mapato bila kujua mwezi ujao huyo mfanya biashara hatakuwepo tena. Kwa kweli kuna uzembe na mizengwe mingi mno. Wakati huo huyo mjasiria mali akipondwa hivyo, wengine wanapeta maana wametoka au wana uhusiano na familia za wenye nchi.
 
Hoja yako ni ya msingi. Ukienda Kariakoo (na hata kwenye miji mingine) Machinga wanauza bidhaa ambazo ziko madukani. Mbaya zaidi wanapanga mbele ya maduka. Machinga halipi kodi, lakini mwenye frame analipa kodi ya pango, service levy na TRA wanamkadiria kodi mara tu anapofungua duka. Kwa namna hii unategemea nini? Hao Macinga wana add nini kwenye uchumi wa nchi? Ndio maana wengi Kariakoo wame opt kufunga maduka na kufanya umachinga.
Machinga ni sehemu ndogo sana katika ukusanyaji kodi katika nchi kama Tanzania,ilivyo hasa TRA wawachie hao machiga wasilipe kodi,hizo bidhaa wanaouza machinga tayari zinakuwa zishalipiwa kodi,wewe mkuu unafikri hao machinga hizo bidhaa wanazitowa wap?!

Kama hufahamu,basi unatakiwa uje kuwa bidhaa za Machinga wanazitoa kutoka katika hayo hayo maduka makubwa,wauza maduka makubwa wanakuwa na makubaliano na Machinga,kama wakinunua mzigo wa kiasi flani watawauzia mzigo kwa bei ya ujumla,bei nafuu..

Umeshawahi kusikia kuna ugomvi kati ya machinga na wauza maduka!?hushangai kwanini hakutokei ugomvi hata kama mamchinga kaweka biashara yake mbele ya duka linazouzwa biadhaa hizo hizo anazouza Machinga!??

Mkuu,biashara ya Machinga ni moja katika kuleta mzuguko wa Pesa katika nchi,nchi masikini kama Tanzania mfumo wa machiga ni moja katika kumsaidia mtanzania wa chini,serikali yenye vyanzo vingi vya kukusanya kodi kama Tanzania ilikuwa haina haja ya kuwabana na kuwashughulikia wamachinga

Nchi za ulaya kuna mfumo kama huu wa machinga,mfano, Ugiriki kuna "Sunday market",Uingereza kuna "car boot sale",Svandinavia kuna "Lopper market",hii mifumo yote ni ya kimachinga,raia wanaweka vitu vyao sehemu walioichagua wanafanya biashara bila ya kubugudhiwa,wanachotakiwa ni kulipia ile sehemu kwa ule muda watakaotumia kuuza biashara zao..

Ni akili ya kiafrika tunawaza,tunaamua kwa hisia kuliko uhalisia wa jambo,kutokana na mfumo wetu wa kutumia akili zetu ndio inayotufanya tusifanikiwe katika maamuzi yetu,tafakari
 
Pale bandarini Kuna shida Kuna kontena letu tunahangaika nalo wiki ya 3 hii ushuru umekuwa mkubwa bila sababu ya kueleweka
Hii nchi inaongozwa na vilaza,waliovaa makoti ya PHD,MBA,DKT,wanafikiri kukusanya kodi kwa wingi tu,hawafikirii hasara gani serikali itapata inapoamua kumbana mfanya biashara kwa kodi zisizo na maana,..

Mimi nina rafiki yangu nae yamemkuta hayo hayo,naona hii hali ikiendelea hakuna atakae weza kushusha mzigo bandarini,sasa ndio tunasikia wafanyabiashara wanakimbilia nchi jirani,mwisho wa siku serikali itakusanya kodi wapi!??
 
Machinga ni sehemu ndogo sana katika ukusanyaji kodi katika nchi kama Tanzania,ilivyo hasa TRA wawachie hao machiga wasilipe kodi,hizo bidhaa wanaouza machinga tayari zinakuwa zishalipiwa kodi,wewe mkuu unafikri hao machinga hizo bidhaa wanazitowa wap?!

Kama hufahamu,basi unatakiwa uje kuwa bidhaa za Machinga wanazitoa kutoka katika hayo hayo maduka makubwa,wauza maduka makubwa wanakuwa na makubaliano na Machinga,kama wakinunua mzigo wa kiasi flani watawauzia mzigo kwa bei ya ujumla,bei nafuu..

Umeshawahi kusikia kuna ugomvi kati ya machinga na wauza maduka!?hushangai kwanini hakutokei ugomvi hata kama mamchinga kaweka biashara yake mbele ya duka linazouzwa biadhaa hizo hizo anazouza Machinga!??

Mkuu,biashara ya Machinga ni moja katika kuleta mzuguko wa Pesa katika nchi,nchi masikini kama Tanzania mfumo wa machiga ni moja katika kumsaidia mtanzania wa chini,serikali yenye vyanzo vingi vya kukusanya kodi kama Tanzania ilikuwa haina haja ya kuwabana na kuwashughulikia wamachinga

Nchi za ulaya kuna mfumo kama huu wa machinga,mfano, Ugiriki kuna "Sunday market",Uingereza kuna "car boot sale",Svandinavia kuna "Lopper market",hii mifumo yote ni ya kimachinga,raia wanaweka vitu vyao sehemu walioichagua wanafanya biashara bila ya kubugudhiwa,wanachotakiwa ni kulipia ile sehemu kwa ule muda watakaotumia kuuza biashara zao..

Ni akili ya kiafrika tunawaza,tunaamua kwa hisia kuliko uhalisia wa jambo,kutokana na mfumo wetu wa kutumia akili zetu ndio inayotufanya tusifanikiwe katika maamuzi yetu,tafakari

Hujawahi fika mtaa wa Kongo. Na maeneo yote hayo ambayo kwa ujumla tunaita Kariakoo. Hungeandika ulichoandika. Pita miji yote hata pa kupita hakuna. Acha mbali hoja za msingi hapo juu kwenye mambo ya kodi
 
Mkuu nimekulia kariakoo,mtaa wa Livingstone,vile vile mimi nimeshawahi kufanya biashara kariakoo,marafiki zangu wote ni wafanya biashara kariakoo,na bado wanafanya biashara,kwa upande wangu biashara imenishida,marafiki zangu wanafanya biashara ya kuuza saa,nguo,vitambaa,nk..

Kama huijui biashara ya kariakoo vipi inafanywa,acha nikufahamishe,kuna wafanya biashara wachache ambao waleta mzigo na kuwauzia wengine kwa ujumla,vile vile maduka madogo madogo yanakopeshana mzigo,mafano mnunuzi anataka kitu lakini huna dukani,unamwambia mnunuzi acha nikachukue stoo,kumbe muuza duka haendi stoo anakwenda duka jirani kuchukua ile bidhaa ambayo mnunuzi anaitaka,..ni kutengeneza mzunguok wa pesa...

Kuna maduka yatafungwa na wafanyabiashara watafilisika kama wamachinga watazuiwa kufanya biashara zao,mfumo mbovu wa serikali na manispaa zake ndio unawafanya wamachinga wazagae ovyo ovyo,..

Nakumbuka hapa daresalam,hasa kariakoo Machinga walipigwa marufuku kupanga bidhaa zao barabarani,,,,sasa nani alionda ile marufuku,!??

Raisi wa jamuhuri JPM ndie alieondoa ile marukufuku,kwasababu za kisiasa,CCM waliona watakosa kura,..sasa nani wakulaumiwa,binafsi naona wamachinga wacha wafanye biashara zao lakini kuwepo na mfumo thabiti wa kuwasimamia..

Muhimu ni kwa wananchi kutengeneza pesa,ili kuwe na mzunguko wa pesa,ili wawe na nguvu za matumizi,ili kila biashara ifanye kazi,ili serikali ikusanye kodi...,huo ndio mfumo mwema kwa serikali na wananchi wake..tafakari
 
This is what surprises me, kodi hapa nchini inatumika kama adhabu. Kuna vijana wameajiriwa na TRA nadhani hawana uelewa wa maana ya serikali kukusanya kodi. Wanakuja kwa kutishia kuifunga biashara yako na kupiga mnada ulivyo navyo kama hukubali kulipa kodi waitakayo. Katika hilo kunakuwa na mchanganyiko wa malengo binafsi na ya serikali. Sasa serikali makini inakussanyaje kodi kutoka kwa mfanya biashara mpya ambaye hata hajaanza mauzo ya chochote katoka tuu kuregister, kapata leseni leo, kesho TRA kawasili kukusanya kodi? Hana haja hata ya kuona risiti wala umeajiri nani kufanya kazi, yeye anataka kumridhisha msimamizi wake kuwa amemkamua mfanya baishara kwa kumtishia mpaka amelipa kodi. Msimamizi mpuuzi anajumlisha mapato bila kujua mwezi ujao huyo mfanya biashara hatakuwepo tena. Kwa kweli kuna uzembe na mizengwe mingi mno. Wakati huo huyo mjasiria mali akipondwa hivyo, wengine wanapeta maana wametoka au wana uhusiano na familia za wenye nchi.
Kuna wafanyabiashara mitaa ya gerezani wanadaiwa kodi ya mwaka jana 2017 Zaidi ya billioni 1.5 kila mmoja na wamepewa mwezi mmoja kulipa. wao wenyewe hawajui hiyo kodi ya Zaidi ya 1.5B imetoka wapi.
Cha Kushangaza, unaitwa TRA na kuhojiwa na makamishna 8 wakiwemo, polisi 2, TRA 2, afisa usalama 2 na afisa uhamiaji 2. wote wanakuuliza maswali kwa wakati mmoja na kila mmoja na swali lake. Mtu mmoja utamjibu nani??. Kisha baada ya kuhojiwa unaambiwa ukatoe maelezo polisi na kufunguliwa jalada. Hii ndiyo hali ilivyo na ndivyo wanavyofanyiwa wafanyabiashara wa Tanzania. Hayo maduka tena ya wazawa wanauza vifaa vya umeme tu tena vya kawaida vya majumbani. Kwa nini mfanyabiashara asifunge duka? na ikitokea hivyo wangapi watakosa ajira??
kiukweli hali ilivyo ni hatari. Na si kwamba serikali kuu haijui, hapana. Suala ni kuwa kwa hali ilivyo sasa hakuna alternative ya serikali kupata pesa Zaidi ya kuwakamua wafanyabiashara pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafiri. Ndiyo maana kwa sasa ukikamatwa na traffic akachukua leseni yako kisha akakuachia uondoke usidhani amekusamehe. iko siku utasimamishwa na kuambiwa una deni na gari yako kusimamishwa na kutakiwa kulipa deni ndiyo uondoke. Yuko mama aliwahi kukamatwa na kukutwa gari lake linadaiwa 400,000/=. Hiyo ni wastani wa gari yake kukamatwa na kuachiwa mara 7 kwani ukiandikiwa unatakiwa ulipe 30,000. Deni usipolipa lita-accumulate mpaka 60,000/=. kisha kosa jingine litakuja kwa style hiyohiyo. Kwa hiyo hayo Ni maagizo maaalumu kutoka juu. Inakuwaje askari akukamate na kama kweli una kosa asikupe risiti ili ulipie ndani ya siku wiki 30,000/=. Na kwa nini asikujazishe fomu maalum kama ushahidi wa kosa lako??? Ni wizi na unyanganyi unaovuka missing ya sheria ya makosa barabarani.
Na huna mahala pa kulalamika kwani kila mmoja huko ndani anajua kinachoendelea.
Ngoja Tuishi Maisha ya kishetani. Ila wafanyabiashara tunaumia sana.
 
Hatari kulipa kodi imekuwa vita..tusubiri 2020 labda tutapata ufumbuzi wa hizi shida!..
 
Kufungua biashara hadi uwe na TIN no. na ukiwa nayo hata japo biashara ni ndogo TRA kila siku ni kodi bila kuangalia unapata nini! PIA watoto wako hawatapa mikopo vyuo vikuu! bora kufanya biashara za nyanya tu sasa.
Yaani mimi kwenye kitambulisho cha taifa nilitiki kwamba sina kazi kuepuka watoto wangu kutengwa katika sera ya kibaguzi ya mkopo wa elimu.
 
Back
Top Bottom