Kifupi nakerwa na namna wa bongo wanavyoyachukulia mambo. Sijui lipi bora afanye Mh Nyarando. Ndio maana hawa viongozi hawajali wala kuogopa lolote kwakua wanajua aina ya fikra za Wabongo wachache wapenda kuchalenge vitu bila kuta fakari ili kujiona wamesema tuu na akili zimekalia kila kiongozi hafai hafai. Ukimpekua mtu kidogo yeye mwenyewe hata kusimamia familia yake hawezi. Wanadamu wote siwakamilifu na waadilifu ndani ya makundi ya waovu wapoo. Kila mtu asijifanye ni minzani ya mwenzake bila kujipima na yeye kwanza. Ni kweli Chama Cha Mapinduzi kina aina ya mapungufu yake lkn sidhani kama ndio dhamira ya Sera zake. Kutawla si jambo jepesi kiasi cha kila mtu kudhani anaweza ila kukosoana kwa misingi ni jambo labusara ktk kujenga nchi na sikushika Dola.
Usilazimishe watu kufikiri kama unavyotaka,hatuwezi kuwa na fikra sawa jenga hoja zenye mantiki juu ya utetezi wako kupata uhalali wa kuungwa mkono.
Fikra ndizo zinazojenga nchi na utekelezaji wa jambo lolote huanza kwenye fikra,busara ni kuambiana ukweli na kutambua ukweli sio kusifiana kinafiki.