Hii inakuaje? Mke/mme wako ama mpenzi kuwa baraka au mkosi kwako?

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,587
Hamjambo wadau!

Napenda leo tujadili hili jambo la kiutu uzima!

Nimewahi kusikia watu mbalimbali wakisema kuwa unaweza oa mwanamke halafu ukajutia kumuoa sio kwasababu anakusaliti, la hasha! ila kwasababu tu anakuwa kama mkosi flani maana tagu ulipomuoa hupati vyema riziki japo unapambana vilivyo kutafuta hela au kwa lugha nyingine tunasema kuwa ‘unapishana na gari la hela!’.

Eti wakati mwingine unaweza pata dili la hela au kazi ila unapokaribia kulifanya linayeyuka ghafla na kupewa mtu mwingine.

Au wakati mwingine unakutana na mikosi mikosi kibao baada tu ya kumuoa huyo mwanamke au kuwa nae katika mahusiano ya mapenzi kiasi cha kukufanya ushuke kiuchumi au kifedha.

Wakati mwingine unaanza kupata mikosi kazini kwako au ulipoajiriwa sambamba na kupata hasara kadha wa kadha zinazokufadhaisha.

LAKINI pia niliwahi kusikia kuwa waweza oa mwanamke au olewa na mwanamme akawa ni mmbaraka kwako kiasi kwamba, ukawa unapata riziki kwa fujo hadi ukashangaa, mara dili la hela hili hapa, mara mchongo wa kazi huu hapa ama familia inakuwa na utulivu kiafya, yaani kwa ujumla unabarikiwa.

SWALI? UTAWEZAJE KUMFAHAMU MWANAMKE/MWANAMME AMBAYE ATAKUWA NI BARAKA KWAKO NA SIO MIKOSI KWAKO?

LAKINI PIA HALI HII YAWEZA KUJITOKEZA KWA WACHUMBA NA WAPENZI AU NI KWA WANANDOA TU?

PIA, JE NI KITU GANI KINASABABISHA HALI HII?



Karibuni wajuzi.
 
Nyota ndo kila kitu kwa mfano ww nyota yako moto ukaoa mwenye nyota ya maji uwa anakuzima kinyota moto Uendana na upepo udongo uendana na maji zaidi ukitaka kujua ni pm
 
Hakuna kiunganishi Kat ya Hilo unalolizungunzia tatizo ukishaweka Imani kama hiyo, mfano mwanaume umeoa ukaanza umalaya na mabint tofaut ukishuka kiuchumi utasema huyu mwanamke niliyeoa ndio mkosi wakat mabint wanakumalizia Ela nafikir ukitaka Baraka tendea familia yako haki ukianzia mke, mume na watoto, kama kila cku unamtesa mkeo na watoto na kila cku wanalia hivyo unazan utapata rizik wakat wako unaowaliza kila cku wanaume mnaotafuta mabint wa risik utasota Sana, rizik ya mtu ipo kwa mungu, tatizo linakuja we muhusika inakuja unaitumiaje hiyo riziki
 
Kuna X wangu mmoja huyo K yake cjui mungu aliiweka nini?:cool::cool:
Yani ilikuwa kila nikikutana nae farangha haziishi cku mbili lazima nitapiga dir moja matata sana.nina mmisi popote alipo..

Huyu wa sasa hivi yeye kanijaria mtoto ASANTE kubwa sana kwake.
 
Kama ni baraka au laana inategemea na akili ya mtu uliyenaye. Ukiwa kwenye mahusiano unaweza kugundua kwamba mwenza wako atakuwa baraka kwako au laana
mmh! Kwahyo akili pekee huleta baraka au kuna vitu au mvuto wa asili wa kukufanya upate riziki zaidi unapokuwa na mme au mke flani. Fafanua zaidi tukuelewe.
 
Kuna uzi niliuwekaga wa vifungo vya nafsi soul ties. Mnapofanya ngono, mnakuwa mwili mmoja au nafsi zenu zinafungamana. Unaungana na mavitu yake yote, iwe ni baraka au laana/mikosi. Ndio maana mnashauriwa kuacha uasherati. Kama unataka kufunga ndoa, inabidi mjitenganishe na miunganiko yote ya nyuma iwe ya kurithi au ya kuitafuta (kwa waganga ulipochanjwa michale au kupitia ngono); ili muwe afresh. Hii hufanyika kwa toba na sala (deliverance), kwa wakatoliki ndio maana kuna kutubu kabla ya kufunga ndoa. Shida watu uelewa mdogo hutubu juu juu tu bila kumaanisha, kujuta wala kutafakari.
 
Kuna X wangu mmoja huyo K yake cjui mungu aliiweka nini?:cool::cool:
Yani ilikuwa kila nikikutana nae farangha haziishi cku mbili lazima nitapiga dir moja matata sana.nina mmisi popote alipo..

Huyu wa sasa hivi yeye kanijaria mtoto ASANTE kubwa sana kwake.
duh! Kwahyo mkuu huyo wa sasa uliyenaye hupati pati dili matata kama zamani? Twambie unafikiri kwanini ilikuwa inakutokea hivyo wakati ukiwa na X wako na je kwanini isikutokee hivyo kwa sasa?
 
mmh! Kwahyo akili pekee huleta baraka au kuna vitu au mvuto wa asili wa kukufanya upate riziki zaidi unapokuwa na mme au mke flani. Fafanua zaidi tukuelewe.
Ukiwa na mpenzi ambaye yeye anapenda starehe na kuspend pesa tuu kila fashion mjini anataka aende nayo unadhani ukimuoa akawa mke utapata baraka au laana
 
Nyota ndo kila kitu kwa mfano ww nyota yako moto ukaoa mwenye nyota ya maji uwa anakuzima kinyota moto Uendana na upepo udongo uendana na maji zaidi ukitaka kujua ni pm
mh! Mambo ya moto na maji plus udongo! Dunia ina mengi.
 
Back
Top Bottom