Elia
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 3,425
- 567
Jamaa anademu wake ambaye wamefahamiana sio zaidi ya miezi miwili iliyopita, katika kumwaga sera jamaa alimhakikishia dem kwamba yupo serious na relation ikiwezekana izae ndoa. Katika kuweka mambo sawa, juzi alikuwa na second date na huyo dem wake siku ilikua nzuri sana anavyo dai, tatizo lilianza njiani wakati anamrudisha, Demu aliomba apewe mdori aliyekuwepo kwenye gari ya jamaa, jamaa alimwambia atamtafutia mdori mwingine ikiwezekana anayefanana na huyo lakini demu alikomaa anataka huyo huyo kama kununua anunue wake. Mwisho wa safari Dem aliposhuka kwenye gari hakumuaga. Jamaa ni Rafiki yangu sana ameniomba ushauri kuhusiana na mpenzi wake huyu ambaye anategemea kuoa Mungu akijaalia Naombeni ushauri wana JF