Hiace zenye bomba au chuma dirishani ni hatarii

samakinchanga

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
2,016
1,220
Nimeona zipo nyingi za Arusha,dodoma,mwanza zimewekewa bomba au chuma kinachozuia kioo kwa ndani mi nasema matrafiki hawaoni je ikitokea ajali ya moto au vinginevyo abiria watatokea wapi hivi Sumatra mpaka yatokee ya kutokea ndo mshtuke.zikagueni hizo daladala na muwaambie watoe mavyuma hayo hatarii.
Basi.ni Mimi mpanda daladala
 
nimeona zipo nyingi za arusha,dodoma,mwanza zimewekewa bomba au chuma kinachozuia kioo kwa ndani mi nasema matrafiki hawaoni je ikitokea ajali ya moto au vinginevyo abiria watatokea wapi hivi sumatra mpaka yatokee ya kutokea ndo mshtuke.zikagueni hizo daladala na muwaambie watoe mavyuma hayo hatarii.
Basi.ni mimi mpanda daladala

kweli ni hatari sana.....sio hiace tu,ht baadhi ya coster zipo zenye hayo mabomba
 
Nimeona zipo nyingi za Arusha,dodoma,mwanza zimewekewa bomba au chuma kinachozuia kioo kwa ndani mi nasema matrafiki hawaoni je ikitokea ajali ya moto au vinginevyo abiria watatokea wapi hivi Sumatra mpaka yatokee ya kutokea ndo mshtuke.zikagueni hizo daladala na muwaambie watoe mavyuma hayo hatarii.
Basi.ni Mimi mpanda daladala

Naunga mkono hoja.
 
Gari hazina mikanda, watakumbukaje kuwa kuziba dirisha ni hatari? Nyumba karibu zote Tanzania, zina madirisha yaliosukwa nondo na mageti milangon. Matokeo yake kila siku kufa kwa moto. kwa ufupi suala la safety bado lipo nyuma sana Tz
 
Yaani hizi hiace and daladala tunazotumia ni Mungu tu anatulinda. Kwa kweli ni hatari sana, kwanza huwa hazifanyiwi service yoyote ya maana zaidi ya kumwaga oil, hawaangalii matairi, na mara nyingi huwa wananunua matairi vipanda ndo wanaweza, hapo boss yuko nyumbani anasubiri elfu 50 yake tu kwa siku. Watu tunajazana kwenye kihiace mpaka gari unaona kabisa imezidiwa mzigo na imepinda upande mmoja. Hiace nyingi utakuta hata vioo vyenywe havifunguki hasa vile vya karibu na nyuma na hapo konda analazimisha mkae wa4 wa4. Yaani mateso tupu. Kuhusu hilo suala la yale machuma ndo shida kabisa. Ebu wahusika siku moja moja wapitie kukagua hivi vyombo muhimu kwa sisi watanzania tulio wengi, na vile vile wamiliki wa haya magari wawe na huruma japo kidogo kwa kufanyia marekebisho magari yao, yaani inasikitisha sana pale unapoona gari lina kutu ndani na kuna mavyuma kama yameng'oka kiasi kwamba hata dereva akifunga brake ghafla basi itakuwa madhala makubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom