Bra-joe
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,562
- 986
Tangu tuzaliwe mpaka tumekuwa watu wazima ni 95% nguvu za malezi ya jinsia za kike. Tukianzi nyumbani mtoto siku zote hulelewa na jinsia hii, mama, dada au house girl, tukianza chekechea au day care walimu wengi jinsia ya kike, shule za msingi walimu wengi ni wanawake, hata wakati tunazaliwa wanawake ndio hutoa msaada kwa mama zetu kule ktk chumba cha kujifungulia, hata sasa ni watu wazima wanawake ndio tunawategemea kutusaidia kupata watoto na kulea familia. Hata leo hii bahati mbaya ukilazwa hospitalini nesi wa kike lazima atakuwepo pembeni yako kukusaidia. Hivyo tusipende kuiita jinsia ya kike kwa majina ya kihuni, hawa ni mama zetu, dada zetu, mashangazi, mama wa dogo n.k. Je, utajisikiaje ukimsikia mtu anamwita mama yako au dada yako jina la kihuni?