Heri ya NOELI na Mwaka Mpya 2013 toka kwa babu ODM

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,015
95,369
Ndugu wajumbe na wadau wa jukwaa hili maalum la watu wasio na msongo wa mawazo,

Ninawaandikieni waraka huu kuwatakienyi nyote NOELI njema na heri ya mwaka mpya 2013. Nawaombeni safari hii tupeane heri na baraka kwa kutumia lugha yetu adhimu ya kiswahili bila kutohoa maneno kwenye lugha nyingine ikiwemo Kiingereza. Hii ni kutaka kumdhihirishia Yesu kuwa hata sie watanzania tunampenda na endapo kama angezaliwa Hospitali ya Barabara ya Bahari naye angekuwa mswahili mwenzetu.

Kwa muktadha huu basi naomba mnapobonyeza vitufe vya funguo ubao kwenye kutakiana heri ya Noeli basi tutumie lugha yetu adhimu walau kuonyesha mshikamano wa kitanzania.

Mimi na familia yangu tunawakaribisheni nyumbani kwa ajili ya kushehereka pamoja na baadaye tujiunge pamoja kwa umoja wetu katika maduka ya kuuzia vinywaji laini na vileo ili tugonganishe bilauri zetu na kutakiana afya njema.

Kila la kheri, na Mungu aendelee kuwabariki.

Msaada kwa waliosoma shule za watakatifu.
Msongo wa mawazo = Stress
NOELI = Christmass
Hospitali ya Barabara ya Bahari = Ocean Road Hospital
Vitufe = Buttons
funguo ubao = Keyboard
Bilauri = glasi

Atakayetumia lugha ya kiinglishi baraka zake zitapungua na anaweza asiurithi ufalme wa Mbingu.

Salamu za pekee kwa watoto wa shule za watakatifu; BiMtamu ( sweetlady), Bwana Mwamba ( Mr Rocky), Mwanamke Mweusi ( Blaki Womani), Hukumu ( Judgement), Binti Sayuni ( Zion Daughter), BiMcheshi ( charminglady), Arushamoja ( Arushaone), Ruhazwe Mdogo ( Ruhazwe JR) na wengine wote wenye majina yote yenye lugha ya Daudi Kameruni ambao sijawataja.

NB: Ntamuomba mwalimu wangu wa lugha hii adhimu Gaijin aje awacharaze bakora wote watakaokiuka masharti na kuichakachua lugha yetu. Pia wataohashuana kwenye huu uzi ntamwomba walimu gfsonwin, snowhite na SnowBall wachukue sheria mkononi.
 
Salamu zikitumwa kwa lugha ya taifa zinanoga ile mbaya :)

Kheri ya sikukuu nawe Babu yao

Ahsante mwalimu wangu. Jiunge nami kukienzi kiswahili. Vijana wa siku hizi awsipoweka maneno ya kiingereza kwenye maandishi au mazungumzo yao wanaona kama vile hawataonekana wasomi, japokuwa kiingereza chenyewe nacho pia hawajahitimu. Hili lipo sana hapa Foramu ya Jamii. (Foramu nimetohoa vinginevyo naomba tafsiri ya Forums kwa kikwetu, samahani kwa usumbufu mwalimu)
 
babu Asprin nakutakia heri na furaha ya sikukuu ya noel na mwaka mpya.

haya nina zawadi yako nitakupatiaje?? umesahau urafiki wetu unaona noeli ya kwanza sasa??
Hapo nilipopafumbata kwa rangi nyekundu unaona umeshaenda kinyume na masharti ya huu uzi? Hatuna neno NOEL kwenye lugha yetu adhimu. Kaongeze silabi "i" mwishoni mwa neno tafadhali.

Kuhusu zawadi, babu anapatikana wakati wowote. wasiliana nami kwa ujumbe binafsi au ujumbe mfupi kwenye kilongalonga changu
 
Last edited by a moderator:

haya bwana nimekupata.
sasa simu yangu haipigi kwenye simu yako sijui simu yako haina mtandao ama nini?
nilipomuuliza shoga yangu cacico akasema simu yake haina mtandao hata yeye mkeo huupata kwa tabu sana na alipomuuliza BADILI TABIA akasema ni kweli na ndio sababu Yummy akaamua kukaa pembeni kuepusha msongamano manake aliona mawasiliano yako na yake ni magumu. tufanyeje sasa babu??
 
Hahahahaha........... naona umeamua kumfanya babu mjomba wako. Muda si mrefu nimetoka kuongea na mzee mwenzangu Mtambuzi kuhusu maswala mtambuka ya kutathmini yatakayojiri kwenye sikukuu ya Noeli pale Leo Tuko Hapa.
 
kwa hiyo unataa kuniambia nini sas ababu?? je nikusubirie hadi noeli iishe unitafute mwenyewe ama??
lakin si ukweli unajua kwamba simu yak haina mtandao siku hizi?? kama ndio mara ya mwisho kumpigia cacico ni lini??
 
Last edited by a moderator:
Babu ODM a.k.a Asprin naomba niseme AHSANTE kwa kunitakia mimi na familia yangu HERI YA NOELI NA MWAKA MPYA 2013..Nikutakie na wewe pia...ila ngoja nikuulize (nakuong'oneza lakini)..hivi Madame B umemuonamo??

unamuulizia Madame B pande za dar leo??
yupo Arushaaa ataonekana dar mwakampya atii.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom