Helikopta ya Barrick yapigwa jiwe

ok, nadhani kuna tofauti ya ustaarabu na fujo. anyway mkuu, kwa kuwa umeomba hayo unayoomba Basi acha Mungu atekeleza maombi yako na ya wapinzani, lakini msije mkajuta tu hapo baadae maana leo hii mnaomba kesho mnapewa, be careful for what you wish for !
 
Mkuu hakuna binadamu anayeombea fujo lakini ni lazima ukumbuke serikali inayokumbatia MAFISADI ndio itakayoleta hayo ya fujo. Hakuna hata mtu anayetaka kuona hayo CCM ndio wako madarakani na ndio watakaoanza fujo. Angalia jinsi dhuluma inavyotendeka kwenye kuwafukuza wazawa katika migodi bila kuwalipa malipo yao sahihi. Leo hii wanachi wa Buzwagi kwa utajiri wa lile eneo walitakiwa kuwa mamillionea wa kutupwa lakini sisi tumekubali kuwapa watu wachache peremende ili wadhulumiwe na kupewa pipi ambazo hazina ladha yoyote.

Viongozi wamejinunulia shares kwa ajili ya watoto wao na familia zao kwa dhamira ya kujitajirisha na sio kuwawezesha WTZ kwa ujumla kujikwamua na umasikini. HII SI SAWA NA CCM LAZIMA WAKATE MZIZI WA FITNA NA KUWAONDOLEA UVIVU VIBAKA, Kuanzia Karamagi, Balali, EL n.k.
 
Sisi watanzania hatutakuwa watu wa kwanza Dunia kuchukua sheria mikononi mwetu.
Subbotage ndiyo silaha yetu ya mwisho mambo yote yakishindikana.

Wengi wa Polisi ni walala hoi wenzetu
FFU nao wengi ni walala hoi wenzetu
Wanajeshi mpaka wenye vyeo vya ukanali wengine ni walala hoi wenzetu
Usalama wa taifa, ukiacha wale wachacheni, karibu wote ni walala hoi wenzetu.
Watumishi very sensitive wa serikali wengi ni Walala hoi.

Hii ya mlalahoi kumpiga mlalahoi mwenzie ni sehemu ya kazi tu lakini si Life Time Commitiment.

Sisi Watanzania mali yetu kubwa na ya dhamani sawa na damu zetu tunayohofia kuipoteza ni nchi yetu.
Mafisadi wana pa kukimbilia mambo yakiwachahcia. Hatahivyo, wana mali nyingi zilizo shika utajiri wao mkubwa waambazo ni hawana budi kuzilinda kwa kutumia hao niliowataja hapo juu.

Muda wa kusabbotage ukifika wataliwa tu.
 
kada,
kwanza jua maana ya upinzani wa kisiasa,chama chochote cha siasa kazi yake kubwa ni kuikosoa serikali iliyopo madarakani,ndio maana hata bungeni kunakuwepo na kunakuwa na wasemaji wa kambi ya upinzani ktk kila bajeti ya wizara inayowasilishwa bungeni.

Kazi ya vyama vya upinzani sio kuipongeza na kuwapa sifa chama kilichopo madarakani.ccm kama chama tawala hakiko tayari kukosolewa hata kidogo na upinzani kwani kwao ni utamaduni mpya.
ccm imetufikisha mahali ambapo sasa inabidi tutafunane wenyewe kwa wenyewe,walilala usingizi wa pono baada ya kuamshwa wamekuta maji yamezidi unga.
chukua mfano mdogo tu,haspitali ambazo zilijengwawakati wa mkoloni ni nyingi kuliko ambazo serikali ya ccm imejenga tangu tupate uhuru
 
ok, nadhani kuna tofauti ya ustaarabu na fujo. anyway mkuu, kwa kuwa umeomba hayo unayoomba Basi acha Mungu atekeleza maombi yako na ya wapinzani, lakini msije mkajuta tu hapo baadae maana leo hii mnaomba kesho mnapewa, be careful for what you wish for !

du umeongezewa mshahara nini mbona uko on fire namna hii
 
*Yatua kwa dharura, rubani ajeruhiwa

*FFU watumwa kumsaka aliyerusha jiwe



Na Mathias Marwa, Tarime


HELIKOPTA ya mgodi wa North Mara imelazimika kutua kichakani katika Kijiji cha Kewanja, wilayani Tarime Mkoa wa Mara, baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wasiojulikana.


Helikopta hiyo mali ya mgodi huo unaomilikiwa na wawekezaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Tanzania, ilishambuliwa juzi kwa kupigwa mawe na kupasuliwa kioo cha upande wa na kumjeruhi rubani jicho.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, David Saibullu, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea majira ya alasiri katika Kijiji cha Kewanja, Kata ya Kemambo, wilayani Tarime.


Helikopta hiyo ilikuwa ikiendeshwa na rubani Charles Wassira, mkazi wa Ukerewe Mkoa wa Mwanza.


Jiwe liliovunja kioo hicho na kumjeruhi rubani huyo, lilirushwa kwa kutumia kombeo na mtu ambaye hajafahamika, ikiwa umbali wa takriban mita 50 usawa wa bahari.


Baada ya rubani huyo kujeruhiwa jicho lake la kulia, alilazimika kutua na kupewa msaada wa kupata matibabu katika hospitali ya Nyamongo iliyopo katika Kijiji cha Nyangoto, wilayani humo.


Kufuatia huduma ya kwanza, rubani huyo akiwa na mwenzake mzungu waliyekuwa pamoja nwakati shambulio hilo likitokea, walifanya marekebisho ya kioo kilicho pasuliwa kisha kuondoka kurejea jijini Dar es Salaam.


Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mawasiliano wa Mgodi huo, Emmanuel Nyasigo, alisema tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kijiji cha Kewanja Namongo wakati rubani akianza kurusha helikopta hiyo.


Nyasigo alisema kuwa helikopta hiyo ilishambuliwa wakati ikifanya doria katika eneo la mgodi huo na kudai kuwa aliyefanya kitendo ni miongoni mwa watu wanaodhaniwa kuwa wezi wa dhahabu na mafuta ambayo ni mali ya mgodi huo.


Alisema rubani huyo alitengeza kioo hicho kilichovunjwa kwa kutumia makaratasi meupe kuziba tundu na kurudi Dar es Salaam.


Kamanda Saibullu, alituma Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Tarime, kikiongozwa na mkuu wake, Costantine Bandola kumsaka mtu huyo au watu waliohusika na tukio hilo ili kuwakamata ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.


Hadi tunakwenda mitamboni hakuna mtu aliyekuwa amekwisha kukamatwa.


Katika eneo la mgodi huo wa Northen Mara kumekuwepo mgogoro kati ya kampuni ya Barrick na wananchi wa eneo hilo ambao wanadia fidia kwa maelezo kwamba kiasi walicholipwa hakilingani na thamani ya maeneo yao.


Kufuatia kutolidhika na malipo hayo baadhi ya waliokuwa wakazi wa eneo hilo waligoma kuchukua malipo hayo wakidai mikataba yao kurekebishwa kulingana na thamani ya maeneo yao.


Katika harakati za kudai haki zao waziri mkuu Edward Lowassa alipotembelea eneo hilo mwezi uliopita walimlalamikia na alipowaambia atamtuma Waziri wa Nishati na Madini, Naziri Karamagi kushguliki suala hilo, lakini walipinga kwa madai kwamba hawamtaki.

Comment:Kwa watanzania wenzangu tupunguze jazba
Kwa viongozi iyo ni challenge kuwa there is something wrong somewhere.
 
Back
Top Bottom