SoC03 Hekima ni mtaji wa mabadiliko ya kila nyanja Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

kennyshuaka

New Member
Jul 28, 2023
2
2
NDUGU watanzania tumempuuza Hekima tusiweze kubaini kati ya jema na baya.tusimpuuze Hekima kwasababu ni mng’ao wa mwanga wa milele, kioo Safi cha matendo ya Mungu na mfano wa wema wake .ingawa Hekima ni mmoja lakini aweza kutenda chochote kwakuwa habadiliki ,na hufanya upya kila kitu katika vizazi vyote rohoni mwa watu watakatifu na kuwafanya marafikii wa Mungu.

Ndugu Hekima ni mzuri kuliko jua na anapita makundi yote ya nyota ni bora kuliko mwanga wa mchana,maana baada ya mchana huja usiku lakini uovu hauwezi kumshinda Hekima kamwe.

Nguvu ya hekima huenea kila mahali duniani na kuweka kila kitu katika mpango mzuri
.matokeo ya hekima maishani ni ADABU NJEMA ,KUWA NA KIASI, MAARIFA,HAKI NA USHUJAA.

Maishani hakuna kilicho bora kupita hayo. Nani anajuta kuwa Mtanzania? Je ungekuwa wapi tofauti na hapa? Hekima ajua mambo yote haya, lakini Hekima ya Mungu imetuchagua kuwa watanzania tushukuru.

Ila usijiachilie huzuni moyoni mwako wala usijiumize mwenyewe kwa makusudi.kwasababu Furaha ya moyo ni uhai wa mtu na furaha ndiyo inayo mpa mtu maisha marefu, lakini Wivu na hasira hufupisha maisha ya mtu na mahangaiko nayo humfanya mtu azeeke upesi.

Mahitaji ya maisha ya mtu ni MAJI,CHAKULA, MAVAZI NA NYUMBA anakoweza kujificha ila Afadhali maisha ya masikini mwenye nyumba yake mwenyewe kuliko chakula cha fahari nyumbani kwa mwingine.kweli ni kwamba Ridhika na kidogo ulicho nacho kwa kuwa ulicho nacho pamoja na Shukran utapata unachotaka nawe hutakemewa kuwa unaishi kwa jasho la mwingine. utajiri ni mzuri kama hauhusiani na dhambi na umaskini ni mbaya kwa maoni ya wasio mcha Mungu.

Lakini hali ya mtu moyoni husababisha hali yake ya nje iwe huzuni au furaha maana yake unachotafakari moyoni mwako ndicho kinachosababisha hali yako ya nje iwe utajiri au umasikini.

Kwamaana Uso mkunjufu ni alama ya furaha moyoni na Utaonekana mwenye furaha hata nje.

Lakini kuvumbua methali kwahitaji kufikiria sana.mawazo yote yamo moyoni mwako na hutoka huko kwa namna nne huonekana WEMA NA UOVU, UHAI NA KIFO na mtawala wa hayo yote daima ni ulimi wako.

Busara iwe Ndio msingi wa kila tendo, na shauri hutangulia shughuli zote ili zikamilike kikamilifu. Mtu anapo mtegemea mwingine ampe chakula ataishi maisha ambayo hayastahili utu.

Ila tuki mtegemea Mungu tutapata maisha ya furaha. Nani awezaye kujua nia ya Mungu kwetu? Au Nani awezaye kufahamu matakwa yake?

Hekima ajua yote Ampendaye hekima anapenda maisha na wamtafutao hekima mapema watajazwa furaha .anaye ambatana naye atapata heshima na Mungu atapabariki mahali anapokwenda.

Watanzania tuchukue taadhari Wakati ufaao na kuepa uovu ili tusijiletee aibu wenyewe. Ndugu tumgeukie Mungu na kumtegemeza kwa kila kitu na kumtumaini yeye hatuta kuwa na woga kwani Mungu ni tumaini letu. Mungu atatuangalia kwa wema kwa kua tunampenda.

Yeye ni ngao imara na tegemeo letu thabiti, yeye ni kinga yetu mbali na upepo mkali, ni kivuli chetu wakati wa jua kali, yeye hutulinda tusiji kwae hutusaidia tusianguke kwa kuwa Mungu huijaza mioyo furaha na huyatia macho mwanga tukumbuke maana ya maisha yenye mafanikio ni kuwa na furaha ya moyoni.

Ndugu Tambua kwamba pombe na muziki hufurahisha moyo, lakini kupenda hekima ni bora zaidi tambua rafiki na ndugu hufaana sana lakini kupatana kwa mke na mume ni bora zaidi.pia Kuwa na ndugu na msaada Wakati wa shida ni vizuri lakini kuwasaidia maskini huokoa kuliko hivyo.

Pia Dhahabu na fedha humfanya mtu imara, lakini shauri jema lathaminiwa kuliko hivyo viwili.Mali na nguvu humfanya mtu thabiti lakini kumcha Mungu ni bora zaidi.hakuna dosari katika kumcha mungu na ukiwa na kipaji hicho huitaji msaada.

Kumcha Mungu ni kama bustani ya baraka, nayo humlinda mtu kuliko fahari yoyote. Hekima ni mtaji wa maisha ya mtu.

Uwepo wa wingi wa watu wenye hekima Tanzania kutaleta mafanikio na mabadiliko ya kila Nyanja ni kweli kuwa zawadi hupofusha macho ya wenye hekima na ni kizibo mdomoni cha kuwazuia wasikaripie ubaya.

Hekima ya kuficha na hazina iliyo fichika je vina faida yoyote ile? Afadhali mtu afichaye upumbavu wake kuliko afichaye hekima yake.


-0768785385
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom