Mkurugenzi wa Sheria CDM ambaye pia ni mnadhimu mkuu wa Upinzani bungeni Tundu Lissu amempongeza Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa John Heche na kuunga mkono kauli yake thabiti kuhusu mbunge wa Maswa Mashariki John Shibuda.
Lissu alidai kushtushwa na tamko la Makamu Mwenyekiti BAVICHA Juliana Shonza kumpinga Mwenyekiti wake hadharani.Lissu alidai kilichofanywa na Shonza ni kichekesho na utovu mkubwa wa nidhamu ambao hauwezi kuvumiliwa.
Lissu alienda mbali zaidi na kusema kikatiba Heche ni msemaji mkuu wa Vijana na si lazima kila kitu kipitie kwenye kikao bali ana mamlaka ya kutolea tamko jambo lolote analoona linaathiri harakati za chama.Amesema wanaosema Heche aliongea kama Heche hawajui wanachokisema bali aliongea kama Mwenyekiti na analindwa na Katiba ya BAVICHA.
SOURCE:MWANANCHI UK 7